Msaada mnyoo wa safura

Msaada mnyoo wa safura

obi's

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2011
Posts
233
Reaction score
40
wapendwa amani ya mungu itawale juu yenu. Naam, kwa wale mwenyezi mungu kawajaaria kupata elimu ya utabibu, naoba kujua juu ya huyo mnyoo, chanzo chake, dalili za ugonjwa, vipimo pamoja na tiba. Nitashukuru sana kama ntapatiwa majibu yaliyo sahihi asante.
 
​Salam , naomba nikujibu suala lako kama ifuatavyo hapo chini

MNYOO:
Kuna minyoo ya aina nyingi , lakini inayosababisha safura kwa binaadam ni aina mbili, ambao wanaitwa Hook worms,
kitaalamu 1. Necator americanus na 2 . Ancylostoma duodenale wameitwa hook worm kwani wanandoana ambayo hujipachikia kwenye utumbo
CHANZO:
Hali mbaya ya usafi wa kuhifadhi Kinyesi, hupelekea mtu mwenye uambukizo kuacha mayai au larva anapojisaidia ovyo, ambapo kinyesi hicho huchanganyika na udongo na inapotokea kuchezea udongo, kutembea bila viatu na kutokunawa vizuri, kula mboga mboga zisokoshwa vizuri ndipo unapokula mayai au kutobolewa na minyoo kwenye ngozi na kuingia mwilini.
DALILI:
Kikawaida kama umepata kiwango kidogo, unaweza usihisi dalili yeyote lakini kama larva aliingilia kwenye ngozi unaweza kuwashwa, hata kumuona juu ya ngozi hususan kwa watoto na ngozi huwa inawasha (cutanious larva migrane)
Kama unaminyoo mingi unaweza kukohoa kohoa, kujisikia maumivu ya tumbo kuchefukwa, kutopata choo au kuharisha kuchoka na kupungukiwa damu, kutokua vizuri (kudumaa) na kuathirika kiakili hasa kwa watoto na waja wazito.
VIPIMO:
Ni kuangalia mayai ya minyoo kwenye choo kikubwa (unapeleka kinyesi hospitali kwa kupimwa kitaalam)
TIBA:
kuwatoa minyoo mwilini kwa kutumia dawa maalumu kama Albendazole na mebendazole
Lakini vile vile ni pamoja na kutibu athari nyengine kama tulizo zitaja mfano, anemia, kukohoa na etc

Angalizo:
Licha ya yote tuloeleza hapa juu suala muhimu ni usafi, kunawa mikono baada kushika udongo, kuosha mboga vizuri, kutumia vyoo wakati wa kujisaidia kuvaa viatu, kupima choo kila baada ya mda fulani, hata kuna programe za kutumia dawa za minyoo kwa kinga
Topic ni ndefu lakini nimejaribu kwa yale yalo muhim na ufupi kama hujaelewa tafadhali usione taabu kuuliza zaidi
Karibu
 
Salam , naomba nikujibu suala lako kama ifuatavyo hapo chini

Je dozi moja tu inatosha kuondoa hao minyoo mwilini?
 
Back
Top Bottom