Msaada: Mke wangu hashiki ujauzito

Mtandaoni

Senior Member
Jul 22, 2013
132
64
Nawasalimu kwa upendo mtakatifu
Jamani wapendwa nina tatizo kwenye ndoa yangu takribani miezi sita sasa tangu kufunga ndoa mke wangu hajabahatika kushika mimba nimejaribu kufanya tendo la NDOA kwa nyakati halisi ila hatujafanikiwa pia mke wangu mzunguko wa siku haunana idadi ya siku maalumu Maana ziko aina tatu ambazo ni siku 26,27,28 haya ni mabadiliko ya kila mwezi, Je inaweza changia tatizo la kushika mimba ama nifanye tendo la NDOA kwa siku ipi kwa mizunguko hiyo naomba msaada asanteni
 
Hilo sio tatizo ni changamoto kwako inayokusukuma kuvumilia na kuzidi kumwomba Mungu upate haja ya moyo wako.

Isitoshe ni mapema sana kulament kuhusu mkeo kutoshika ujauzito.Pia ndoa umeingia si kwa nia ya kupata mtoto tu,naamini yapo mengi ishi vyema na mwenzio mambo yatakua bam bam
 
Vumilia, bado sana usiweke hofu kwako na yeye. siku akimaliza period tu fanya kila siku (bao moja asubuhi kwenye saa 11-ili alale tena kidogo) kwa wiki mbili mfululizo. Pumzika mpaka atapoanza na kumaliza period. Wengine inawachukua miaka 2, 5, 8 hadi 10 kupata mtoto, uvumilivu ni muhimu
 
Nawasalimu kwa upendo mtakatifu
Jamani wapendwa nina tatizo kwenye ndoa yangu takribani miezi sita sasa tangu kufunga ndoa mke wangu hajabahatika kushika mimba nimejaribu kufanya tendo la NDOA kwa nyakati halisi ila hatujafanikiwa pia mke wangu mzunguko wa siku haunana idadi ya siku maalumu Maana ziko aina tatu ambazo ni siku 26,27,28 haya ni mabadiliko ya kila mwezi, Je inaweza changia tatizo la kushika mimba ama nifanye tendo la NDOA kwa siku ipi kwa mizunguko hiyo naomba msaada asanteni
Jaribu na wewe kufanya sperm analysis, usimlaumu mkeo, lakini pia mpeleke naye kwa gynacologist ingawa miez sita si mingi ya kukupa presha.
 
Nawasalimu kwa upendo mtakatifu
Jamani wapendwa nina tatizo kwenye ndoa yangu takribani miezi sita sasa tangu kufunga ndoa mke wangu hajabahatika kushika mimba nimejaribu kufanya tendo la NDOA kwa nyakati halisi ila hatujafanikiwa pia mke wangu mzunguko wa siku haunana idadi ya siku maalumu Maana ziko aina tatu ambazo ni siku 26,27,28 haya ni mabadiliko ya kila mwezi, Je inaweza changia tatizo la kushika mimba ama nifanye tendo la NDOA kwa siku ipi kwa mizunguko hiyo naomba msaada asanteni

Kwa akili zangu za kibinadamu, Nenda naye mfanye check up hospitali, halafu apate na tiba ya MP.
Lakini pia aseme ukweli aliwahi kutoa mimba????
Katika mambo ambayo mwanaume na mwanamke wanapaswa kuambiana ni haya yafuatayo!
1. Je msichana aliwahi kutoa mimba?
2.Je mna magonjwa ya kurithi????
3. Je kuna matatizo mengine ya kufahamishana?
hii inanisaidia mimi na yeye kuwa na position nzuri ktk mahusiano,
Wanawake watakubaliana na mimi kwamba wanapoolewa na wanaume wenye watoto halafu hawakuwahi kuambiwa, vurugu lake siyo la kitoto.
 
Miezi 6 mbona mapema?

Next time nunueni ovulation kit mpime kuona anaingia lini.

Lakini je mlishaenda na mwenza wako kupima? Wote wawili mnatakiwa mchekiwe
 
hio ovlution kit kinauzwa maduka ya madawa(pharmacy) au kinapatikan wap kinauzwaje bei na kinatumiwaje
 
kama anapata siku zake bila shida may be problem is you kwamba gametes zako hazina nguvu na pia nakushauri upate ushauri wa kidoctor
 
Dah aisee miezi sita michache sana kikubwa hapo kama wadau walivyosema inabidi wrote mkachekiwe kukua tatizo lipo wapi
 
Wewe vumilia tu, iga mfano bora wa mkuu wa Mkoa ambaye amejipatia mtoto mwaka huu
 
Back
Top Bottom