Msaada: Mbona niki login TCU inakataa?

Msaada: Mbona niki login TCU inakataa?

Ototo

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2016
Posts
1,260
Reaction score
1,167
Wanajamvi Kuna kitu kinanichanganya kichwa toka jana.

Nimejisajili jana tcu ili nipate kuapply chuo. Nikalipia pesa nikaletewa transaction ID vizuri tu. Nikaji register nikajaza baadhi information zangu Lakin sikuchagua vyuo nika log out ili nije nilog in kuendelea na kumalizia kujaza vyuo.

Lakini kila niki login inakataa nikaamua kureset password lakini napo inagoma naambiwa hawaitambua transaction ID wakati ndio niliitumia kujisajili.

Nikaamua kuchukua namba zao ili niwapigie lakini hawapatikani.
Mpaka sasa niko dilemma kwa wale wenye uzoefu na mambo haya naombeni msaada wenu jamani...
 
Itakua mtandao unasumbua.. Au wasiliana nao tcu na huo mtandao uliotumia kununua
 
Itakua mtandao unasumbua.. Au wasiliana nao tcu na huo mtandao uliotumia kununua
TCU hawapokei simu ila mtandao niliotumia kununua tayari tulishamalizana maana mwanzo ilikubali registration
 
TCU hawapokei simu ila mtandao niliotumia kununua tayari tulishamalizana maana mwanzo ilikubali registration

Bado inakusumbua hadi leo? Je, kabla ya kurest password ulipo log in ilikuletea ujumbe gani?

Ikiwa tayari ulikwishalipia na kuanza kuchagua course, unahitaji kuingia kwa mara ya pili kutazama au kufanya mabadiliko ya selections zako usiingie kama New Applicant bali ingia sehemu ya Registered Applicant.

Aidha, kuwa makini unapoandika username na passwords. Andika kwa usahihi wake na zingatia herufi kama ni kubwa ama ndogo. Ukishindwa wasiliana na TCU kwa kuwapigia simu mara nyingi kisha eleza tatizo lako watakusaidia.
 
Wiki hii inayoanzia 25/7/2016 website ya tcu iko busy vibaya sana - ni overloaded! Errors ni nyingi sana. Ingia muda wa lowtide, usiku saa nne au asubuhi saa 12.Hata mimi nilikumbana na tatizo lililofanana na lako jumatatu tarehe 25. Nikaingia asubuhi saa 12 tarehe 26 mambo yote waaaa! Nimemaliza kuchagua kozi nasubiri kwenda chuoni.
 
Back
Top Bottom