Msaada. Maumivu ya kiuno.

Samboko

JF-Expert Member
Oct 30, 2011
5,417
7,731
Habari zenu wana jf. Nina tatizo la maumivu ya kiuno hasa nnapokua nafanya kazi inayonlazimu kuinama kwa zaidi ya dakika 15 baada ya hapo naskia maumivu ambayo yamaweza kuendelea kuuma mpaka ntakapolala au kuisha baada ya saa kadhaa, naomba kujuzwa nina tatizo gani, kwenu madokta wa jf mnijuze.
 
Mimi nakupa Dawa lakini nenda hospitali kamuone daktari atakupa maelezo zaidi Jaribu Dawa yangu hii Dawa ya Kiuno

1.Uwatu kijiko kimoja kikubwa.
2.Zaatari vijiko vitatu vikubwa.
3.Ubani (Dhukr)mweupe chembe saba.
4.Maji chupa moja.
unachemsha pamoja .
Matumizi: Kunywa Robo gilasi kutwa mara tatu.​
 
Mkuu Mzizi Mkavu hivi vitu vinapatikana ktk maduka gani maana naona kama hayo majina yanaonekana kama maneno ya Kiarabu
 
pole. unamatatizo ya neva katia uti wa mgongo kutokana na kazi ngumu. kamuone neurologist au neurosurgeon haraka. tumia brufen kupunguza maumivu. wahi unaweza kufa miguu(paralyse). ni ugonjwa hatari
 
Asante kwa maelekezo yako mkuu, ntatafuta hivyo vitu mkuu.
 
pole. unamatatizo ya neva katia uti wa mgongo kutokana na kazi ngumu. kamuone neurologist au neurosurgeon haraka. tumia brufen kupunguza maumivu. wahi unaweza kufa miguu(paralyse). ni ugonjwa hatari

Asante kwa ushauri mkuu, hao wataalam wanapatikana wapi? Nijuze tafadhali.
 
Mkuu Mzizi Mkavu hivi vitu vinapatikana ktk maduka gani maana naona kama hayo majina yanaonekana kama maneno ya Kiarabu
Kama upo Dares-Salaam nenda Kariakoo Sokoni kuna maduka ya wauza hizo dawa ninafikiri watakuwa ni waPemba kaulizie watakupa hizo Dawa ni za kiarabu zina manufaa mengi mwilini.
 
Ahsante mkuu kwa majibu ila mie niko MIKOA YA KASKAZINI, Je niende mji upi kati ya Arusha na Moshi?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom