Msaada: Majibu ya kipimo cha Ultrasound

kilamba lamba

JF-Expert Member
May 27, 2020
367
679
Natumai hamjambo humu ndani.

Nilikuwa na Swali kidogo hapo. Kwa mwenye kufahamu hili msaada kidogo. Hivi kipimo cha Ultrasound kinaweza kukupa majibu sahihi ya Umri wa mtoto, kwa Mfano labda una muda gani wik ngap Au Miezi mingapi?

Je Ultrasound inasoma kuanzia Siku ya mwisho mwanamke kuziona siku zake Au toka siku ya mimba kutunga?
 
Itakua inaweza japo nahisi changamoto ni watoa huduma wetu , mimba ya mwez mmoja niliambiw inamiez mi2 na siku 1 , hivyo name nikabaku kua na swali kama lako
 
Yani hapa nina maswali mengi sana. Kwa sababu siku nazozijua mimi nimeambiwa tofauti kabisa. Mimba ya wiki 6 nimeambiwa Ina wiki 8 na masiku kadhaa

Kipimo kizur na cha uhakika kujua umri wa mimba n tarehe zako. Kama hukumbuki ndo tunatumia ultrasound. Ultrasound inachofanya inakadiria umri wa mimba kwa kutumia dimensions za kiumbe, ambapo kwa mimba changa inakadiria karibia na usahihi ukilinganisha na mimba kubwa. Watu wengi wanachanganya kwenye kutafsiri hivi vipimo.
 
Natumai hamjambo humu ndani.

Nilikuwa na Swali kidogo hapo. Kwa mwenye kufahamu hili msaada kidogo. Hivi kipimo cha Ultrasound kinaweza kukupa majibu sahihi ya Umri wa mtoto, kwa Mfano labda una muda gani wik ngap Au Miezi mingapi?

Je Ultrasound inasoma kuanzia Siku ya mwisho mwanamke kuziona siku zake Au toka siku ya mimba kutunga?

Habari!

Kipimo cha Altrasound kinaweza kutoa majibu ya umri wa mimba kwenye mazingira yafuatayo:

1: Kwa kupima ukubwa wa mfuko wa uzazi, ambao pia hutafsiriwa kwenye umri wa ujauzito(kwa mimba ambayo viungo havijatengenezwa). Vipimo vya mlinganyo huwa vimeshawekwa kwenye mashine husika.
Mfano: kipenyo cm ? = wiki ?

Miezi mitatu ya mwanzo huwa na majibu halisia/hakika zaidi.

2: Kwa mtoto ambaye ana viungo kamili, hii huitaji kutafuta wastani wa:

A: Ukubwa wa mzunguko wa kichwa(head circumference)

B: Ukubwa wa tumbo(abdominal circumference)

C: Urefu wa mfupa kuanzia kwenye nyonga mpaka kwenye goti(femur length).

D: Urefu wa kutoka upande mmoja wa sikio mpaka upande wa pili(biparietal diameter).

NB: Wastani wa haya yote ndo huleta umri.

Majibu yake huweza kuathiriwa na mambo mbalimbali kama:

1: Lishe kwa mtoto vs mama mjamzito.

2: Afya ya mama vs mtoto

3: Vinasaba vya urefu
Nk.

Hivyo, hapa altrasound hukubarika kuwa +-wiki mbili.

Majibu pia yanaweza kutegemea:
1: Aina ya mashine/teknolojia(uwezo).
2: Uwezo wa mtumiaji mashine/competence.
 
Itakua inaweza japo nahisi changamoto ni watoa huduma wetu , mimba ya mwez mmoja niliambiw inamiez mi2 na siku 1 , hivyo name nikabaku kua na swali kama lako
Mkuu na mimi nimepata same issue. mimba ya miezi miwili naambiwa ina miezi mitatu sielewi
Naomba msaada kwa wataalam
 
Huwa inatoa majibu ya kimakadirio sio sahahihi kwa 100% ndomana hata siku ya kujifungua huwa inatajwa kimakadirio
 
Back
Top Bottom