hapo step ya kwanza ni kujaribu kuihard reset, ku clear cache na dalvik ikiwezekana.
hakikisha imezima halafu bonyeza hizi button tatu kwa mpigo,
-cha kuwashia simu
-home button
-cha kuongezea sauti.
vibonyeze kwa pamoja hadi uone nembo ya samsung halafu achilia cha kuwashia simu huku unaendelea kushika home na cha kuongezea sauti.
atakuja robot wa android kisha utaingia recovery,
tumia cha kuongezea sauti na kupunguza kwenda juu na chini na cha kuwashia kuselect okay
-clear cache
-clear dalvik cache
-wipe device/factor reset
ukimaliza reboot device uone kama itafaa