Nimefanya mapenz leo mpira ukapasuka nina hofu asije pata ujauzito bado hatujajipanga naomba kujua nifanyeje kuzuia hiki kitu
Pole sana lakini usiwe na hofu inaweza kumtokea mtu yeyote yule.
Njia ya kuzuia mimba ziko mbili.
1) kama umefanya mapenzi ndani ya masaa 72 basi unaweza kutumia njia ya kuzuia yai lisitoke, na kama lilikua limeshatoka wakati unafanya mapenzi basi lisikutane na mbegu ya kiume.(Yai huishi masaa 24 tu baada ya kutoka) Njia hii hutumia dozi kubwa ya homoni za kike kuzuia mimba,nayo ni;
kutumia Emergency contraceptive pills ambazo zinapatikana pharmacy kubwa mjini. Zina bei kiasi unaweza kuuziwa kati ya elfu nane mpaka ishrini.Utapewa maelekezo ya jinsi ya kutumia na pharmacist.
Lakini pia unaweza kutumia vidonge vya uzazi wa mpango ambao hupatikana pharmacy zote za mjini na vijijini. Bei ni nafuu sana ukilinganisha na zile ready made za Emergency Contraceptive ila dozi ni ngumu kukupa maana hizi dawa zinatofautiana - kwa kifupi unaweza kunywa vidonge vitatu au vinne (inategemea) muda huo huo utakaoipata alafu baada ya masaa ishrini na nne. Inaweza kukuleta kichefu chefu na hata kutapika kutoka na wingi wa hizo homoni. Haina madhara maana si unatumia kwa kipindi hiki tu cha bahati mbaya- yaani ndo isiwe mchezo wako wa kila siku kunywa dawa za homoni nyingi...siku nyingine tumia dawa na dozi ya kawaida ya uzazi wa mpango.
*Angalizo kwa COC kama hiyo nilioeka kwa picha,changua vidonge kutoka mistari mitatu ya mwanzo ya pakiti na sio ule mstari wa mwisho ambao vidonge vyake havina homoni mbali vina sukari au dawa ya kuongeza damu.
2) Ndani ya siku tano baada ya kufanya mapenzi unaweza kwenda hospitalini wakueka Intra uterine contraceptive device kwenye mfuko wa uzazi...nisaidieni jina la kiswahili nimesahau kidogo. Hizi IUCD huzuia mimba iliotungwa isiji attach na kuta za nyumba ya uzazi...
Nitatoa somo Instagram...Nifollow kwa account @ daktari_sundae