Msaada kusajili clinic | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada kusajili clinic

Discussion in 'JF Doctor' started by CHE GUEVARA-II, Aug 8, 2011.

 1. CHE GUEVARA-II

  CHE GUEVARA-II JF-Expert Member

  #1
  Aug 8, 2011
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 531
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Kuna mtu anaomba msaada, ushauri kuhusu requirements za clinic registration:
  Ka-clinic anakotaka kukasajili kana Daktari (MD) mmoja na clinical officer mmoja. Na hawa nd'o kila kitu (kazi za nurse na za maabara zile ndogondogo kama kupima malaria kwa RDT siyo microscope, typhoid, syphilis, blood sugar, urine,wanafanya wao)
  Katakuwa kanatoa primary health care ambapo mgonjwa hatakuwa anakaa clinic zaidi ya saa 24 kama atahitaji hospitalization.

  So, anauliza afanyeje au ni vitu gani anatakiwa awe ameshakamilisha kwanza ili aweze kufuatilia registration mpaka Wizarani (MoHSW).

  Natanguliza shukrani za dhati kwa msaada wenu!
   
 2. Ozzie

  Ozzie JF-Expert Member

  #2
  Aug 8, 2011
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 3,234
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Mkuu kuna vitu vinne ambavyo huyu mtu anatakiwa ajue.
  1. Anataka kufungua dispensary, health center, specialized clinic au hospitali? Kwa jinsi ulivyosema nadhani atahitaji kufungua dispensary. Ila naamini staff uliowataja ni wachache, la sivyo afungue maabara tu.
  2. Anataka kufungua wapi? Nijuavyo ni kwamba kituo cha tiba kipya kinatakiwa kiwe na umbali usio chini ya km 5 toka kilipo kituo kingine cha tiba.
  3. Kabla hajajenga au kufanya ukarabati, lazima aende kwanza kwenye ofisi za daktari wa wilaya au manispaa au jiji ili waweze kukagua eneo na kukupa ruhusa ya kuendelea na mipango ya ukarabati. Hii ni muhimu sana, maana ni kawaida kwa watu kukataliwa eneo walilojenga au kuambiwa wafanye marekebisho makubwa kwa sababu tu hawakuchukua ushauri kabla ya kuanza ukarabati.
  Hapa pia kuna umuhimu wa kufikiria disposal ya taka. Vituo vingi vya tiba huingia mikataba na hospitali kubwa katika kuteketeza taka. Hili ni jambo la muhimu sana. Na huyo mtu lazima identify mahala atakokuwa ana dispose taka zake au kama atajenga 'insinereta'.
  4. Kila kituo cha tiba sawasawa na mnyumbulisho huo hapo juu namba 1, huwa na mahitaji ya chini ya aina ya wafanyakazi, majengo na vifaa. Hivyo ni vyema uende ofisi zilizotajwa hapo namba 3 ili uweze kuelezwa mahitaji ya chini ya rasilimali watu, vifaa na majengo na hata taratibu za usajili ambazo pia huanza hapohapo namba 3.
  N.B
  Ukishamaliza ukarabati, kuna fomu nne wazijaza na kuzitengeneza kama kitabu, ambazo zitapelekwa wilayani, mkoani, na wizara ya afya hatua kwa hatua. Copy moja itarudi kwako.
   
 3. CHE GUEVARA-II

  CHE GUEVARA-II JF-Expert Member

  #3
  Aug 8, 2011
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 531
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Nashukuru sana kwa ushauri wako.
  Sehemu anayofanyia ni mgodini (yeye ametakiwa afuatilie taratibu zote zinazotakiwa ili clinic iwe registered). Thanks
   
Loading...