Msaada kuhusu sheria za Barabara.

Kasomeko

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2018
Posts
627
Reaction score
1,215
Habari zenu wakuu!

Nimekutwa na mkasa unaohusu eneo langu la biashara lililo kando ya barabara. Nina nyumba ambayo kwa mbele kuna vyumba vya biashara (frame) ambazo zina wapangaji.

Zipo frame tatu, mbili zilikua na wapangaji tangu zamani, na moja (ya katikati) haikuwa ikitumika. Sasa kwa mbele ya hiyo frame iliyokua haitumiki pakawa wazi tu hivyo wafanya biashara ndogo ndogo (wauza matunda, karanga n.k) wakawa wanauzia hapo mbele bila malipo.

Wiki iliyopita kuna mtu kanifata anataka nimpangishe hii frame ila nikaona kwanza niongee na hao wanaouzia matunda hapo mbele ya frame ili kuwapa tarifa kua ninalipangisha hilo eneo. Niliwaambia hii frame naipangisha elfu 60 kwa mwezi. Kwavile wameuzia hapo kwa mda mrefu na wateja wao wamepazoea wakakubali kunilipa hiyo elfu60 kwa mwezi ili nisipangishe frame. Wao walitaka hilo eneo la mbele tu maana biashara yao haihitaji frame.

Sasa haikuisha wiki wakaniambia niwapunguzie bei iwe 30 kwa mwezi eti biashara zao sio kubwa kwahiyo hakuna faida kubwa. Nikawapunguzia. Baada ya siku nne tu wakagoma kulipia kwa madai kwamba hilo eneo ni barabara kwahiyo ni Mali ya serikali. Niliamua kuwafukuza na nikapangashipo mtu nwingine.

Hawa watu sasa wamekwenda kulalamika ofisi ya mtendaji wa kijiji. Nimepokea barua Leo inayonitaka nifike ifisi ya mtendaji wa kijiji kesho asubuhi. Hivyo naomba kujua kama nilikosea kuwafukuza. Na je ni sahihi mtu aweke biashara take mbele ya biashara ya mtu mwingine kwasababu tu eneo lipo barabarani?

MUHIMU. Sikutumia nguvu wala matusi kuwaondoa. Nilisubili wakiwa hawapo nikaweka mtu kwahiyo waliporudi kuweka biashara zao walikuta tayari kuna mtu hivyo wakatafta maeneo mengine.
 
Kwa mujibu wa picha uliyoiweka hiyo barabara inaonekana Ni barabara ya mtaa au ya kijijini na kama ni hivyo huna makosa.

Na kwa muonekano wa hizo Frame zinaonyesha kuwa ni za muda mrefu sana hivyo huna makosa kiongozi haki iko upande wako. Inawezekana hata barabara ndio ilizifuata frame
 
Huenda wanakuita ili mkayaweke sawa na labda wanataka kukusaidia ,kikubwa hiyo mahama ihamie eneo la tukio ndio mjadala utanoga
 
Ni kweli mkuu ni barabara ya kijiji/ mtaani hata gari mbili haziwezi kupishana kwa urahisi. Na frame za jirani hakuna hawa wauza matunda maana wakiweka tu mbele ya frame watakua wanaziba biashara ya aliepanga ndani ya frame.
 
Ni kweli mkuu ni barabara ya kijiji/ mtaani hata gari mbili haziwezi kupishana kwa urahisi. Na frame za jirani hakuna hawa wauza matunda maana wakiweka tu mbele ya frame watakua wanaziba biashara ya aliepanga ndani ya frame.
Una haki hakuna wakukupa shida itikia huwo wito na ikibidi wakulipe gharama za kukupotezea muda wako
 
mara nyingi watendaji hafuati haki na ubaya upo kijijini watakuonea tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…