Msaada kuhusu Masters Dissertation

mteule senior

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
296
Reaction score
197
Habari zenu wadau,

Naomba kufahamu kutoka kwa wale waliowahi kusoma masters UDSM, SUA, MU, UDOM, EASTC na kwingineko hapa Bongo.

Mfano, kozi ya masters ikiwa ni miaka miwili, na prospectus ikaonyesha kuwa mwaka mmoja ni coursework na mwaka wa pili ni dissertation.

Je, huo mwaka wa pili ni lazima utafute sehemu ya official ya kufanyia huo utafiti na ukae kwa masaa yote ya kazi ktk hiyo taasisi (I mean kama inavyofanyika ktk undergraduate fields) au unaweza endelea na utafiti wako huku ukifanya kazi zako za kawaida mfano kama kama ww ni mwajiriwa, unakuwa unaendelea na kazi yako na kuifanyia kazi hiyo dissertation.

Naomben mwanga katika hili.
 
Research component hugawanywa sehemu kuu tatu ukiachilia mbali proposal development: (1) Data collection- kwenye proposal yako utakuwa umeeleza hii itafanyika wapi, hivyo kama hakuna mabadiliko utakwenda huko kukusanya data. (2) Data Analysis and write up: kwa research nyingi hii hufanyika baada ya kukusanya data na mwanafunzi anahitaji uongozi wa msimamizi wake hivyo kawaida hufanyika chuoni. Sasa kuna vyuo huelekeza kabisa kuwa hii ifanyike chuoni kuna vingine hunyamaza kimya. Hivyo usishangae kusikia mtu anafanya analysis na kuandika akiwa mbali na chuo. Kuna degree za part time na hizi kawaida hufanyika nje ya chuo. Unaonana na supervisor wako kwa makubaliano na unaendelea kuchapa kazi kutokana na maelewano yako na mwajiri.
(3): Submission and defence: Vyuo vingi siku hizi wanataka dissertation au thesis iwe defended, hapo lazima urudi chuoni for defence na corrections na mwisho final binding.
 
thanks boss
 
kwa UDSM hiyo stage 2 huwa wameelekeza ifanyike chuo au wananyamaza tu ?
 
Dissertation ni tofauti na field attachment ambayo inakutaka ushinde field. Kwenye dissertation utaenda field kukusanya data tu, ambayo itategemea na method ulioichagua and it can be less than a week unless method ulioichagua ni observation (which is rare) ndio utakaa kitambo
 
Issue kubwa ktk dissertation ni proposal development ambayo mnaweka na supervisor wako ikiisha hiyo na imebeba blue print ya dissertation unaweza kuanza kufanya sherehe hata kama hujawahi kwenda field yoyote. Kuna data collection methods zinakutaka utumie reports and trends, hizo unafanyia library ya chuo au digital library ukiwa hata nyumbani, so unaweza usiji attach na taasisi yoyote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…