Msaada kuhusu kuboresha akaunti yangu ya Instagram

Msaada kuhusu kuboresha akaunti yangu ya Instagram

elvis richard

Senior Member
Joined
Dec 6, 2014
Posts
195
Reaction score
208
Jamani ndugu zangu ..
Nimewakutanisha hapa ili tujadili kitu kimoja ambacho nahisi nahitaji msaada wenu wa hali na mali...

Mimi ni kijana ambaye nimejikita katika kujenga brand yangu kupitia mitandao hasa mtandao wa Instagram.

Kikubwa ambacho nimekikusudia na naendelea kufanya sasa hivi ni kukuza brand kupitia video za vichekesho pamoja na memez .

Lengo langu hasa ni kutaka kuikuza page yangu kupitia vichekesho kama nilivyosema hapo awali. Kupitia page yangu, nataka niwe na uwezo wa kutangaza biashara za watu na hatimaye kuwa ambasador wa bidhaa za wafanya biashara mbalimbali na hivyo kujiongezea kipato.

Lakini shida inakuja kwamba imekuwa ngumu sana kwa page yangu kukua. Namaanisha followers pamoja na views zimekuwa chache sana kwa kila post ninayo ituma.

Katika videos zote nilizopost ni moja tu ndiyo iliyopata views 2000 tu na si zaidi.

Pia napata followers kwa uchache sana.

Sasa hivi nina followers 624 tu ...kitu kinachoniumiza sana .

Wataalamu naombeni mnipe shule ya maana ili niweze kutoboa kupitia Instagram ili niweze kufikia lengo langu.

So far ninachokijua ni kwamba ili post ziwafikie wengi zaidi ni kwa kutumia hashtags peke yake.

Naombeni mnijuze ni kwa namna gani naweza kuongeza followers pamoja na views kwenye page yangu.

Natanguliza shukrani zangu za dhati kwenu wataalamu.
 
Imeandikwa
"Kila mwanaume atakula kwa jasho..." Hasa ww unaetaka kupost tu kisha ule ngoja kwanza tupo bize tunavuja jasho wenzio. Njoo usaidie fundi mkuu!!
 
Imeandikwa
"Kila mwanaume atakula kwa jasho..." Hasa ww unaetaka kupost tu kisha ule ngoja kwanza tupo bize tunavuja jasho wenzio. Njoo usaidie fundi mkuu!!
Hahahah
 
Tanzania we dili na umbeya na ujinga ujinga ndio utavutia watu mitandaoni ukileta ustaarabu hautafanikiwa
 
Imeandikwa
"Kila mwanaume atakula kwa jasho..." Hasa ww unaetaka kupost tu kisha ule ngoja kwanza tupo bize tunavuja jasho wenzio. Njoo usaidie fundi mkuu!!
hii pia inahusisha jasho, ndiyo maana nahangaika kutafuta maarifa mpaka huku
 
  • Thanks
Reactions: hnp
Tanzania we dili na umbeya na ujinga ujinga ndio utavutia watu mitandaoni ukileta ustaarabu hautafanikiwa
pamoja kaka, lakini mimi nataka kutambulika mwenyewe kwanza kabla ya kuanza na huo umbeya, kama ambavyo watu tunamjua mkude simba au mchekeshaji mwingine
 
Inaweza kukuchukua muda ninakushauri uza maudhui jina kitakufuata tu
Work hard hakuna kinachoshibdikana
pamoja kaka, lakini mimi nataka kutambulika mwenyewe kwanza kabla ya kuanza na huo umbeya, kama ambavyo watu tunamjua mkude simba au mchekeshaji mwingine
 
Back
Top Bottom