SaaMbovu
JF-Expert Member
- Oct 8, 2013
- 6,028
- 5,355
Habari wana JF.
Kulingana na ugumu wa maisha kumezuka kila aina ya mbinu ili mtu aweze kuingiza pesa kwa njia halali au haramu. Back to topic kuna mdogo wangu alikuwa anahama chumba baada ya mkataba kwisha maeneo ya Kinondoni B. Baada ya hapo akawa kapata chumba maeneo ya Kinondoni Studio baada ya kumtumia dalali ambae wanaofisi yao ya udalali pale Mkwajuni.
Kwa mujibu wa maelezo ya mdogo wangu ni kuwa alionyeshwa chumba na akaridhika tarehe 22/12/2014 na kutokana alivyoambiwa kuwa chumba wameonyeshwa wengi ikabidi akalipia siku inayofuata kwa makubaliano ya 50, 000/= kwa mwezi na alilipa miezi 6 pamoja na ya dalali jumla 350, 000/=.
Wakati wa malipo walikubaliana kuhamia pale tarehe 1/1/2015 kwakua mpangaji aliyekuwepo ndio alikuwa anaondoka siku hiyo na mdogo wangu alikubaliana na hilo kwakua alipokuwa anakaa mkataba ulikuwa unaisha tarehe 8/1/2015. Malipo yalifanyika kwa kuandikishana kwenye karatasi kama kawaida.
Baada ya hapo mwenye nyumba ambae anaitwa Andrea Michael Mkude na ndio mhusika mkuu alipokea fedha hizo na kutoa ahadi hiyo na huku wakiwa wamekubaliana. Ilivyo fika siku hiyo mdogo wangu akampigia simu baba mwenye nyumba na kumwambia leo nakuja tarehe imefika. Yule mzee alicho jibu ni kwamba mpangaji bado hajatoka mpaka tarehe 6 kwakuwa amepata shemu nyingine kwahiyo mpaka tarehe 6 ndio ahame. Ilivyofika hiyo tarehe mzee akipigiwa simu hapokei na akitumiwa sms hajibu.
Baada ya kwenda kwake mdogo wangu alimkuta mwanae na alivyoelezwa akasema hii nyumba hapangi mtu wala hakuna hilo na huyu baba yangu ni tapeli na hatujui yuko wapi na sisi tukimpigia simu hapokei ana zaidi ya wiki hajafika nyumbani na hata hicho chumba alichokuonyesha ndio chake.
Baada ya hapo tuliendelea kumfuatilia bila mafanikioa mpaka ilivyofika tarehe 8 akanza kutuma sms za kuomba msamaha ambazo zilikuwa 4 na hakuendelea tena kutuma sms wala kupokea simu. Baada ya kurudi kwa mwanae akasema kuwa hiyo ni tabia ya baba na kuna wengine anawapangisha nyumba nzima wewe unabahati chumba kimoja lakini mzee huwa anarudisha pesa baada ya mwezi. Kwahiyo huwa anakopa kwa kulazimisha.
Tulijaribu kwenda kituo kidogo cha polisi Kinondoni wakasema hizo kesi ni mpaka uende Polisi Osterbay baada ya kwenda pale Polisi wakasema hilo uanatakiwa uende kwa mjumbe wa mtaa. Baada ya kwenda mjumbe hakuwepo na baadhi ya majirani wanasema mjumbe ndio wako njia moja kwani kila mtu anajua tabia za huyo mzee.
Msaada tufanye nini?