Msaada kuhusu GPA

upeo

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2013
Posts
369
Reaction score
222
Habari wakuu,

Kuna mdogo wangu amefanya first degree ya nursing (GPA 3.6),halafu akafanya masters ya public health (haijawekwa kwa GPA, just grade ya kila somo), na PhD ya reproductive health. Kwa sasa yupo chuo anafundisha program ya nursing undergraduate.na aliajitiwa mwaka 2010.

Alikua anafikiria kuhama chuo na kwenda chuo kingine, sasa amesikia kwa utaratibu mpya wa TCU lazima awe na GPA ya 4 at master level. Wakati yeye anaajiriwa katika chuo hapo zamani waliangalia GPA ya first degree tu ambayo ilitakiwa iwe above 3.5.
Swali:
Ikiwa anataka kuomba kazi upya chuo kingine, atatakiwa pia GPA yake ya master ifikie 4 au kwa vile tayari ana PhD haitoangaliwa?
Na vipi ikiwa master yake haijawekwa kwa GPA, afanye nini kuweza kujua GPA yake?
Asante
 
Nchi nyingi Ulaya hawatumii huo mfumo wa GPA wanaandika grade tu.
 
Kama master level hawajaweka ktk mfumo wa GPA basi lazima waweke overall grade either A,B+,B,C.

Kuajiriwa kufundisha chuo mara nyingi huwa wanachukua kuanzia wenye B+ au B.
 
Mtu mwenye doctorate hilo swala ni dogo sana kwake, lazima ameishalipatia ufumbuzi huko aliko.
 
Kama master level hawajaweka ktk mfumo wa GPA basi lazima waweke overall grade either A,B+,B,C.

Kuajiriwa kufundisha chuo mara nyingi huwa wanachukua kuanzia wenye B+ au B.
Ni kweli, wanaandikaga "B+ grade for unclassified degree"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…