ciproflaxin ni aina ya anti biotic ambayo inatumika kutibu magonjwa kama UTI,TYPHOID. Ni dawa ambayo kwa sasa bacteria wameshaanza kuidevelop resistance mfano MRSA bacteria.
mkuu hilo swali siyo rahis kama ulivyo uliza, ni bora ungeuliza ugonjwa halafu wadau wakushauri dawa.
na kama shule ya udaktari na ufamasia ingekuwa hivyo yaani mnataja dawa afu mnaorodhesha magonjwa ya kutibiwa na hiyo dawa. basi mambo yangekuwa simple saana na huenda watu wengi wangesomea..
Jibu sahihi ni kuwa hiyo ni antibiotic na inatibu magonjwa yatokanayo na aina fulani ya Bakteria.
mfano, Magonjwa ya zinaa kisonono , kimeta anthrax, homa ya matumbo typhoid, mifupa, magonjwa ya ngozi, kuhara, kuhara damu, magonjwa ya njia ya hewa,, unaweza ukataja mpaka kesho.
kumbe ukiona mtu anatumia hiyo dawa usikimbilie kutoa hitimisho lako kuwa ni dawa ya ugonjwa fulani.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.