Hello Wandugu,
Sorry ni mara yangu ya kwanza kuandika hapa so ntaomba radhi kama kuna namna ntam bore mtu Recently nimegundua rafiki yangu ana tatizo la endometriosis yaan nimeshindwa cha kufanya. Sana sana ninaomba kuelimishwa kuhus process za IVF pamoja na gharama
N:B Endometriosis - Ni wakati mwanamke akiwa katika siku zake, ndipo madhara hujitokeza katika mishipa ya ukuta wa mji wa uzazi na damu hiyo ya hedhi kumwagika nje ya mishipa hiyo,” Hivyo madhara yake huathiri maeneo yote ya mishipa ya uzazi yaani fallopian tubes, uteras na mji wote wa uzazi na hii inaweza ikapelekea mpaka tatizo la ugumba.
IVF (In vitro fertilisation) - Ni taratibu zinazotumika katika utungaji wa mimba Wakati wa IVF, mayai yaliyokomaa hukusanywa (kutolewa) kutoka kwa ovari na kurutubishwa na manii kwenye maabara. Kisha yai lililorutubishwa (kiinitete) au mayai (kijusi) huhamishiwa kwenye mji wa mimba. Mzunguko mmoja kamili wa IVF huchukua karibu wiki tatu.
Thanks in Advance