Habari za jioni,
Band cells ni chembechembe changa za seli nyeupe za damu ''white blood cells i.e Neutrophils''. Kazi kuu ya seli nyeupe ya damu ni kupambana na magonjwa. Kwahiyo hizo band cells zikionekana kwa wingi inaweza kuwa dalili ya mwili unapambana na ugonjwa japo sio mara zote. Ni vizuri kama unaonyesha dalili zozote ukarudi kwa wataalamu kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Nikutakie jioni njema.