MSAADA: Juzi namba nisiyoijua ilinirushia TZS 740, 000/= bila maelezo yoyote

Mara simu ya baba,aisee hiyo hela ya mdogo wako kwaajiri ya ada,itunze nitachukua shule zikifungua,ohoo
 
Mkuu hio ni missposting fanya tu usamaria wema wasiliana na mtandao husika au na aliekutumia...Hakuna pesa inayoweza kupatikana bila kuifanyia kazi.
 
Wakuu salam nyote.

Juzi kuna namba mpya imenirushia TZS 740000 bila maelezo yoyote kimakosa na mpaka sasa haijanipigia simu wala kampuni husika haijairudisha hela hiyo.

Ipo tu toka juzi nami naicheck tu ila leo nilijaribu kuchomoa kaelfu 50 nikanunua nyama kidogo na mahitaji mengine kwa ajili ya familia. Nataka nikakate kiu kidogo hata Lite baridiiiii 4 hivi maana leo ni weekend.

Namba yenyewe sijaipiga wala nini. Wote tumeuchuna.

Hii ni miujiza au bahati au chumaulete au masonic?

Sina deni wala simdai mtu wala sijafanya biashara na mtu kabisaaa. Kifupi simdai mtu.

Naombeni mwongozo
nirushie laki moja number angalia PM
 
Kaka ni yakwangu hiyo naomba nirudishie nilituma kimakosa kaka, naomba nirudishie tafadhari Sana, kna mtu nlimtuma nikampa namba ili atume kwa jamaa angu nahisi alikosea namba , asante kwa wema wako, nirudishie kwa mamba hii 0764175188
 
Wataarifu watu wa mtandao husika kua huutambui muamala huo. Usishawawishike kutoa au kutumia hela hizo wala usizirejeshe direct kwenye namba iliyokutumia, waweza ingia kwenye matatizo ya kosa la wizi wa mtandao. Pia kurudisha hela kwenye namba iliyokupigia waweza kua ni watu wanataka kutakatisha pesa kwa hiyo wanatuma kwa watu wengine pesa kidogo ili wazuge
 
Kaka ni yakwangu hiyo naomba nirudishie nilituma kimakosa kaka, naomba nirudishie tafadhari Sana, kna mtu nlimtuma nikampa namba ili atume kwa jamaa angu nahisi alikosea namba , asante kwa wema wako, nirudishie kwa mamba hii 0764175188
Daaaah...
Mkuu naona unamaanisha!.
 
Back
Top Bottom