Msaada juu ya VW Passat- engine AZX - V5

Babu Danny

Member
Apr 2, 2020
5
4
Wakuu! bila shaka mambo yako sawa! naombeni msaada ni Injini gani naweza kufunga kwenye VW Passat ya Mwaka 2002 na ikafanya Kazi vizuri?

Hii gari kwa sasa inatumia Injini Yake AZX -V5 lakini inasumbua sana spare na imeanza kuwa na leakage, nataka kufanya modification ili nifunge Injini ya Toyota au nyingine itakayoweza kukaa vizuri kwenye hilo Bodi kama linavyoonekana kwenye picha!

Msaada tafadhari wakuu.

20190526_160531.jpg
 
Kama unataka fuel consumption funga injini ya 3s,4s-fe au 1g-fe ila ziwe Vvti.

Kama unataka mbio funga 3s-gte au 1jz-gte. Kuna BMW series 3 nimeona Geartech Tz wameifanyia modifications wameweka 1jz-gte, unaweza ukawatafuta ili wakushauri kama unataka ufunge mashine za mbio na mod kwenye gari.
 
Kama unataka fuel consumption funga injini ya 3s,4s-fe au 1g-fe ila ziwe Vvti.

Kama unataka mbio funga 3s-gte au 1jz-gte.
Kuna BMW series 3 nimeona Geartech Tz wameifanyia modifications wameweka 1jz-gte, unaweza ukawatafuta ili wakushauri kama unataka ufunge mashine za mbio na mod kwenye gari.
Nashukru sana, ila sehemu ya kukaa Injini ni ndogo sana kuweza kukaa 3S. na tatizo sio ulaji wa matuta ila ni usumbufu tu wa Injini yenyewe. Nashukuru sana kwa ushauri wako Mkuu.
 
Wakuu! bila shaka mambo yako sawa! naombeni msaada ni Injini gani naweza kufunga kwenye VW Passat ya Mwaka 2002 na ikafanya Kazi vizuri? Hii gari kwa sasa inatumia Injini Yake AZX -V5 lakini inasumbua sana spare na imeanza kuwa na leakage, nataka kufanya modification ili nifunge Injini ya Toyota au nyingine itakayoweza kukaa vizuri kwenye hilo Bodi kama linavyoonekana kwenye picha! Msaada tafadhari wakuu.View attachment 1407467
Kwanini usiagize Engine yake. Modification kwenye gari za Europe zitakusumbua sana....
 
Nashukru sana, ila sehemu ya kukaa Injini ni ndogo sana kuweza kukaa 3S. na tatizo sio ulaji wa matuta ila ni usumbufu tu wa Injini yenyewe. Nashukuru sana kwa ushauri wako Mkuu.
Jaribu 5A au 7A, hila performance haitokuwa kubwa sana maana hiyo gari ina uzito mkubwa. Engine inaweza ikawa inapata tabu unapotaka kufika haraka kuanzia speed kubwa, kwa kuwa uwiano wa uzito na nguvu ya injini ni mdogo.
 
Kwanini usiagize Engine yake...... Modification kwenye gari za Europe zitakusumbua sana....

Ni wazo ambalo nilifikiria mkuu lakini kuna changamoto sana kwenye kuagiza, hiyo gari ilikuwa Auto ikaleta tatizo la kutokubadili gia, nikahangaika nayo nikaona itanifirisi, nikaamua kuibadili kutoka Auto kwenda manual na nikaagiza gearbox ya Manual E-bay kutoka uingereza, bei haikuwa kubwa pamoja na usafiri.

Tatizo ilipofika kuanzia kodi na mpaka gharama za clearance nilikuta imekula kama 1.6 Milion! Hivyo shida ni gharama na mafundi wetu, maana hata baada ya kuipokea baada ya kumpelekea fundi ndio akaiharibu na Injini kabisa.

Kwani timing Yake inasetiwa kwa nyuma, hivyo yeye takati anafunga freewheel akafunga bolt ndefu zikapitiliza zikakata timing chain pamoja na tensioner zake na wakati wanalazimisha kuiwasha ikakata valve. Hivyo ikaanza tena Kazi upya kutengeneza Injini na ndio tatizo lilipoanzia.
 
Jaribu 5A au 7A, hila performance haitokuwa kubwa sana maana hiyo gari ina uzito mkubwa.
Engine inaweza ikawa inapata tabu unapotaka kufika haraka kuanzia speed kubwa, kwa kuwa uwiano wa uzito na nguvu ya injini ni mdogo.

Mkuu, 5A na 7A haziwezi kuvuta hilo bodi ni zito sana. Kitu ambacho kinanifanya nifikirie kubadili injini ni ubora wa bodi lake, yani mkiwa Wawili kuisukuma hiyo gari ni shida sana, kwani ni nzito na ina system kubwa za usalama tofauti na gari zengine za kawaida ikiwa barabarani ikiwa ni pamoja na Airbag kila kona.
 
Mkuu kama upo Dar watafute Geartech Tanzania wapo Kijito nyama. Au chukua mawasiliano yao kwenye page yao Instagram "Geartech Tz".

Ukiwapa gari watakufanyia modifications bila kujali ni gari ya mzungu,mjapani au mmarekani.
Kila kitu kinawezekana.
 
Hizo gari ni nzito na body yake ni imara sana, usiache mali hiyo.
 
Mkuu kama upo Dar watafute Geartech Tanzania wapo Kijito nyama. Au chukua mawasiliano yao kwenye page yao Instagram "Geartech Tz".

Ukiwapa gari watakufanyia modifications bila kujali ni gari ya mzungu,mjapani au mmarekani.
Kila kitu kinawezekana.

Asante sana Mkuu, ngoja niwatafute
 
Mkuu pole sana. Hizo gari mafundi wachache na normal zinaua sensors tu. Kama uko dar nenda mwembechai ulizia babu fundi wa magari. Gereje iko upande wa kushoto kama unaelekea Manzese, unaingilia hapo Mwembe Chai straight na vumbi then unaizia kwa babu.
Wakuu! bila shaka mambo yako sawa! naombeni msaada ni Injini gani naweza kufunga kwenye VW Passat ya Mwaka 2002 na ikafanya Kazi vizuri?...View attachment 1407467

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu, 5A na 7A haziwezi kuvuta hilo bodi ni zito sana. Kitu ambacho kinanifanya nifikirie kubadili injini ni ubora wa bodi lake, yani mkiwa Wawili kuisukuma hiyo gari ni shida sana, kwani ni nzito na ina system kubwa za usalama tofauti na gari zengine za kawaida ikiwa barabarani ikiwa ni pamoja na Airbag kila kona.

Hata bajaj ni nzito lkn once ile engine ya cc 200 imewaka bajaj huwa nyepesi sana...kwan kwan hiyo gari inauzito kiasi gani ishindwe pelekwa na 5A
 
Mkuu, 5A na 7A haziwezi kuvuta hilo bodi ni zito sana. Kitu ambacho kinanifanya nifikirie kubadili injini ni ubora wa bodi lake, yani mkiwa Wawili kuisukuma hiyo gari ni shida sana, kwani ni nzito na ina system kubwa za usalama tofauti na gari zengine za kawaida ikiwa barabarani ikiwa ni pamoja na Airbag kila kona.
boss...unapima uwezo wa engine na body kwa kuangalia HorsePower sio watu wangapi wanaweza kulisukuma gari n.k
angalia engine iliyokuja na gari ina hp ngapi? kama ni 100hp, means hata 1nz yenye hp 105 inaweza kukaa hapo bila shida na ikakupa performance ile ile.., mfano 1hz ile ile ambayo ipo kwenye landcruiser vx unaikuta pia kwenye coaster inayobeba abiria..,
sasa kwa akili yako unaweza kusema uzito wa coaster unafanana na landcruiser v8? . ...ukihitaji msaada zaidi ni PM
 
Back
Top Bottom