Crispin Nyoni
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 413
- 90
Wakuu,nilikuwa natoka Mshangano hapa Songea kwenda mjini kwa daladala.Nilikaa na mtu mmoja ambayo alikuwa na biblia.Akajitambulisha kwangu kuwa yeye ni mtumishi wa Mungu.Kiukweli aliongea mengi kunihusu.Akasema katika simu yangu kuna M PESA TSH LAKI MBILI.Na kweli ilikuwa hiyohiyo.Akasema anataka kunisaidia nikatoe hela ili aziombee ziwe nyingi zaidi.Akili yangu ikafungwa na sijui ilifungwaje.Tukafika mjini nikatoa akanisubiri.Nikampa akazipokea mikononi akaziombea akanipa hakuchukua hata shilingi akasema nikazitunze niwe na imani zitaongezeka yeye ni nabii.Naandika kwa masikitiko,ile nafika nyumbani kuangalia hela zote zimekuwa karatasi zina harufu ya uvumba.Wakuu hivi nimefanyiwa mchezo gani na nitawajuaje matapeli tena wengine wanasema ni manabii?Mlioko Songea mtu huyu amejitambalisha kwa jina la nabii Olomi.Imeniuma sana kwa kweli inauma sana.