Msaada je lulu ni nini?

Chinona

Member
Joined
Jul 14, 2017
Posts
53
Reaction score
44
Wana jamii forum wanzangu habarini za saizi

Kama swali swali linavyo jieleza hapo juu nimekua nkijiuliza sama maswali mengi kuhusiana na lulu.
Ili kupata jibu nikajaribu kuuliza watu wengi tena wa rika tofauti kuanzia wazee, umri wa kati pamoja na vijana wenzangu. Wengi wamekua hawana uelewa na hiki kitu ni nini na wengine wamenipa majibu ya wanavyo dhani ila hawana uhakika.

Labda niweke sawa kwenye mazungumzo ya kawaida tumekua tukisikia mtu akisema hichi kitu kina ng'aa kama lulu na wengine kusema hichi kitu ni adimu kama lulu sasa huwa najiuliza lulu ni nn?

Baadhi ya watu waliniambia lulu ni aina ya dini tena lipo chini ya bahari na lina ng'aa sana wengine wakasema ni malaika
Kwakweli bado nahitaji msaaada wa hili swali wadau

Asanteni naomba kuwasilisha
 
Yuko jela bhana
 
Lulu ni kitu cha thamani.... Hakuna madini yenye hilo jina.
 
Lulu ni yule aloua bila kukusudia ila haikuchunguzwa vizuri naye alibakwa mi simo ila afande sele vision!
 

Lulu ndio Pearl kwa Kiingereza, na inapatikana kwenye aina ya Makonokono yanayoitwa Chaza kwa Kiswahili,

Nenda google kaSearch hilo neno Pearl na kwa uhakika utapata elimu unayoitaka

Hiyo ndio picha ya Chaza pamoja na Lulu yake hicho kama kigololi

 
Asante sana bwana kituko kwa jibu lako [emoji122]nimeelewa
 
Sikupingi mheshimiwa,ila mimi nilidhani ni "oyster"na maelezo ndiyo hayohayo ila nafikiri ni katika pweza ndiyo hupatikanaga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…