Habarini wanajamvi,
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 19 na nina kipaji cha mpira na kutokana na kufanya sana mazoezi nipo vizuri sana kuhusu kiwango na ndoto yangu ni kuja kuwa mwanasoka mkubwa wa kimataifa baadae.
Ushauri niombao kutoka kwenu ni je ni njia gani nitumie katika kupata timu hapa bongo nijijinge zaidi na pia iwe ndiyo sehemu yangu ya kupitia katika kutimiza ndoto zangu.
Je nikaombe msaada kwa akina Shaffih Dauda na Edo Kumwembe?
Msaada tafadhalini.