Msaada: iPhone 4s keeps restarting

Strictly Syrup

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2013
Posts
1,228
Reaction score
1,831
Habari zenu ndugu zanguni,
Nina iPhone 4s yenye iOS 8.3. Siku mbili zilizopita nilikuwa ninaitumia vizuri tu, lakini ikaisha charge, nilivyochomeka chaja, ikaonyesha apple logo halafu ikazima. Baada ya hapo huo ndiyo ukawa mchezo wake, kila nikiwasha inaishia apple logo na kuzima. Tatizo ni nini?? Mawazo yoyote yataheshimiwa.
 

Download ios ipsw file la iphone 4s la cdma + gsm toka hapa https://ipsw.me
Then uwe na comp yenye itunes latest .
Chukua usb ya simu ichomeke kwenye comp yako then press home ukiwa umeishikilia chomeka simu bila kuachia home key kaa umeshikilia simu itawaka ikiwa kwenye dfu mode kwenye screen utaonyesha alama ya usb na neno itunes achilia home key subiri simu itakuwa detected kwenye itunes
Then nenda kwenye itunes bonyeza shift key kwenye keyboard bila kuachia shift key click restore kwenye itunes, utaambia uselect ipsw file lako ulilodownload liselect then kaa na utulie simu itaanza kuwa restored so sit and relax mpaka inaliza usiiguse we iache mpaka imalize.
 

Shukrani kaka itabidi niirestore, je kuna uwezekano wowote wa kuhamisha data, kwa sababu hii ndiyo iPhone yangu ya kwanza kabisa, ndiyo maana sina uzoefu na vitu vingi.
 
Shukrani kaka itabidi niirestore, je kuna uwezekano wowote wa kuhamisha data, kwa sababu hii ndiyo iPhone yangu ya kwanza kabisa, ndiyo maana sina uzoefu na vitu vingi.

mimi pia sina uzoefu na iphone ila niliwahi kurestore moja ya ndugu yangu, itune inafanya backup ya vitu vyako hutapoteza kitu.
 
Shukrani kaka itabidi niirestore, je kuna uwezekano wowote wa kuhamisha data, kwa sababu hii ndiyo iPhone yangu ya kwanza kabisa, ndiyo maana sina uzoefu na vitu vingi.

Yah ikisha kuwa detected kabla ya kurestore click back up itafanya back up then ndio uirestore ikimaliza kurestore kwenye simu kuna wakat itakuuliza set as a new phone au back up from itunes chagua from itunes itakwambia ichomeke kwenye pc icjomeke then process nyingine utaziona kwenye itunes uzifuate
 
ni kweli ipo sehemu ya backup


Shukrani sana
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…