Lavit
JF-Expert Member
- May 16, 2011
- 14,756
- 32,344
Wadau habari zenu,
Poleni na majukumu ya kila siku,
Leo nimeamua kushare na nyie tabia ambazo naona zimeendelea kukita mizizi katika maisha yangu ya kila siku. Nimekuwa mtu wa kutokujali mambo yanaondelea iwe kwa ndugu ama jamaa, hata ikitokea msiba umetokea huwa naona kitu cha kawaida sana wala huwa sishtuki, hata nikihudhuria ni pale tu mazingira yanapokuwa yamenibana.
Siyo misiba tu hata sherehe kuhudhuria huwa naona napoteza muda wangu tu, hivyo hata michango huwa sitoi na mara ya mwisho kutoa mchango ilikuwa 2013 kuna mahali nilikuwa nafanya kazi, staff mwenzetu akawa anaolewa hivyo ikanilazimu kutoa. Mbali na hapo taharifa za michango huwa nazipotezea na wala sizipi umuhimu wowote.
Napenda kukaa mwenyewe na mpaka sasa nina 30+ na naishi peke yangu mtu akija kwangu hata akae siku moja huwa naona ananitinga tu, hata kipindi ninapokuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanamke akaanza kuniganda yani hapo ndo huwa anaharibu kabisa, akija kwangu eti ashinde siku nzima huwa naona kero kubwa akilala ndo kabisa naweza nikaanza kumchukia! Hivyo basi kipindi ambacho nakuwa single huwa nainjoi maisha sana.
Kuna muda huwa nawaza, sijui hata huyo mke nitaishi naye vipi, what if akianza kujaza ndugu zake au ndugu zangu wakianza kujazana kwangu nitakuwa kwenye hali gani? Natamani sana kutoka kwenye hii hali, maana najiona ni mtu katili na nisiyejali kabisa hapo nilipo nina ndugu zangu watatu wamepata watoto, sijaenda kuwaona wala sijaona umuhimu wa kwenda maana taarifa hawajanipa.
NB; Sina wazazi, nimeanza kuishi peke yangu toka std 5, hivyo kipindi chote hicho nimewahi ishi kwa watu kwa miezi 6 tu. Nimewahi penda twice nikaumizwa hivyo siamini kama kweli kuna mapenzi ya dhati.