Sio ngumu, mwambie amjaribu. Kwa ugonjwa alionao (Obsessive Compulsive Disorder - OCD), inatakiwa mshauri/mshauri nasaha afanye angalau vifuatavyo:
- Kumshawishi huyo kaka aamini kwamba lengo lake (goal) la kuwa na huyo dada kama mke haliwezi kutimia (it is impossible to meet the goal).
- Aamini kuwa kuendelea kufikiria kwamba lengo lake linaweza kutimia is irrational and unreasonable given his circumstances.
- Aamini kuwa si lazima kufikia malengo ambayo yapo nje ya uwezo wake. Ajifunze ku settle for lesser but satisfying goals ambazo zipo ndani ya uwezo wake.
Pia jaribu kumwambia rafiki yako awe very clear kwenye kauli zake kwa huyo kaka kwa sababu inawezekana naye pia anachangia kulikuza tatizo kama anatoa majibu ambayo yanamfanya huyo kaka aamini kwamba iko siku moja wanaweza kuwa pamoja. Kama hampendi, ni vizuri aliweke hili very clear kwa macho makavu kabisa na bila kuuma maneno!