famicho
JF-Expert Member
- Jul 29, 2015
- 2,191
- 2,852
Habari za jioni tulivu wanaJF,
Baada ya kupitia nyakati ngumu za kimahusiano, hatimaye nilimpata binti ambaye kwa kweli anaonesha ananipenda kwa dhati kwani amenivumilia mambo yangu mengi sana.
Nimejitokeza hapa kuomba ushauri wa namna gani naweza kumuacha pasi na yeye kujisikia vibaya kwa maana tunaishi vizuri sana na anatimiza wajibu wake kwangu ipasavyo.Sababu kubwa inayonipelekea kufikia uamuzi wa kumuacha ni kutokana kunikabidhi majukumu ya familia(kuna wakati mama yake alilazwa hospitali nikamhudumia mpaka akaruhusiwa) yake ilihali sijamuoa na wala kwao sifahamiki kwa sababu sipo tayari kufanya hivyo. Pia huyu binti hana kazi yoyote ila ana wategemezi(dependants) wengi ambao in turn mimi ndo mhusika wa hao tegemezi wake, achilia mbali nami pia nina wengi wanaonitegemea.
Naombeni ushauri wa namna ya kufanya, ila mpango wangu ni kumuacha tu huyu binti vinginevyo siwezi fanya lolote la kimaendeleo na tangu nmekuwa nae mipango yangu imepungua kasi kwa namna fulani hivi.
Karibuni kwa ushauri