Msaada: Hotel ya bei ya chini Morogoro

Nashukuruni sana ndugu zangu. Mmenisaidia sana. Ndo ninaingia Moro sasa.
 
huu ndio ushauri wa mwisho tena bodaboda wa hapo town wako poa kama vipi uwaambie wakulete aika lodge hapa..

Aika imetulia sana na hata kama unampango wa kujiupdate itakufaa dana,ipo kama unaenda kigurunyembe chuo lakin hufiki huko,ni sehemu huwez potea,napapenda sana usalama mzur ipo karibu na manispaa hata unaweza enda kwa daladala
 
ukishuka stand(msamvu) panda daladala ya town,shuka masika then uliza guest house inaitwa ASSA ipo karibu na kona bar karibu na CRDB bank.

Ili hata usiku akizidiwa ashuke tu hapo kahumba kwa mguu apate chake sio awe mwepesi
 


kuna guest 1 karibia na stand ya mabus yanayokwenda Dodoma madereva wengi wanapenda kulala hapo bei yake ni elfu 10 tu... Ipo maeneo ya Msamvu
 
Huku hatufanyi booking we ukishashuka Msamvu, kamata daladala ingia town, uliza top life bar utapata room nzur na misos hapo hapo katikati ya Mji

Wasije wakampeleka toplife karibu na keepleft cha sua chumba kinaanzia 30000 wakat mwenzio kasema ana 15000 si atafua mashuka ya hotel
 
ukifika town kaka mwambie dereva akupeleke sweet africa ni lodge fln iko poa tu! iko misufini bei 12,000/= fuata ayo maelekezo kaka usisikilize ushaur wa mtu yeyote maana naons kama watu wengi wanakuzingua tu wakati ww uko serious! ukishukia msamvu kwenda uko sweet africa nauli ya pk pk 2000 na ukishukia town nauli 1000! narudia tena ni sweet africa ipo misufin
 

Misufini awe makini.maana jirani tu pale kuna mtaa wa vibaka.MANZESE/SABASABA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…