Msaada: Files zilizo katika flash disc hazionekani

Katavi

Platinum Member
Joined
Aug 31, 2009
Posts
42,099
Reaction score
12,932
Heshima yenu wakuu.
Flash disc yangu inakataa kusoma mafaili yaliyopo ndani. Nimejaribu kutumia katika kompyuta zaidi ya moja lakini inaonekana haina faili lolote. Nikiwa naiscan mafaili yanaonekana ila nikiifungua inaonekana haina kitu. Naogopa kuiformat kwa sababu kuna mafaili ya muhimu sana. Naombeni msaada namna ya kurecover hizo faili.
 
Ndugu Katavi Hizo files zipo hidden kwa sababu kuna malware walio-infect pc yako ama pc ulipochomeka flash disk yako. Malware hao wakiinfect PC wanakuwa na uwezo wa kubadili atribute ya files zako. Kwa mfano wanaweza kubadili files lako kuwa Read Only au Hidden.
Cha kufanya, chukua flash disk yako na uichomeke kwenye computer. Bonyeza Start na herufi "R". Itatokkea dialog katika dialog hiyo andika cmd halafu bonyeza "Enter". Itafunguka program yenye interface nyeusi na maandishi ya kijivu. Ukifika hapo type command hii:
"attrib -h -r -s /s /d F:\*.*" halafu bonyeza "Enter"

Kumbuka hapo kwenye F: ni drive letter so kama flash yako ni H badili F kwa kuweka H. Baada ya hapo utaweza kuona kwamba files zako zimekuwa unhidden.
 
Last edited by a moderator:
Fuata njia zifuatazo ili kufungua flash yako iliyo HIDE files ndani yake:
1.Chomeka flash husika ktk computer yeyote mradi tuu iwe inatumia OS ya windows 7 au 8/8.1 (Na njia hii inatumika hata kwa windows xp japo hapa nitatoa maelezo kwa windows 7 au 8/8.1)
2.Fungua windows explorer (Yaani pale palipozoeleka kama my computer) na usome drive letter iliyopo katika flash husika. Drive letter ni ile herufi inayoandikwa mbele ya jina la flash yako au zile partition za Hard Disk ya computer.mf: Removable Disk (F) hapa drive letter ni F. Hivyo note down flash yako itakuwa na herufi gani kwan ukichanganya na hard disk ya PC hatutafanikiwa chochote hapa.
3.Bonyeza alama ya start (Windows logo) alafu andika pale kwenye search box neno 'CMD' (bila hizo quotes)
>Kisha utaona CMD katika ulivyo search, sasa click hapo kuifungua. Itafunguka box leusi lenye maneno C:\user...>\ _
na cursor inayo blink kumaanisha unatakiwa kuandika kitu.
4.sasa andika ifuatavyo bila kukosea
attrib -s -r -h /s /d G:\*.* alafu bonyeza enter.
..Sasa ngoja nitafsiri jinsi ya kuandika hizo code hapo kwani ukikosea kidogo tuu command hii haitafanya kazi,
Ipo hivi: ukishaandika "attrib" weka nafasi alafu ndo uandike -s then weka nafasi andika -r then nafasi tena andika -h then nafasi tena andika /s (yaan kati ya / na s hakuna nafasi) alafu kutoka /s kuja slash (/) ya pili weka nafasi (yaani hivi /s /) Again baada ya slash iliyombele ya s andika /d (yaan hapo usiweke nafasi kati ya / na d, then weka nafasi kisha andika drive letter ya flash yako..mimi nimeandika G kama vile ndio flash yangu, then weka alama za Semi-colon mbele tu ya drive letter yako (G🙂 then weka back slash ikifuatiwa na nyota,nukta na nyota bila kuweka nafasi kati yao (yaan hivi G:\*.*) baada ya hapo bonyeza ENTER na usubiri hadi uone yale maneno yaliyokwepo tangu mwazo kabla hatuja andika chochote katika cmd yetu yamerudi ambayo yalikuwa ni C:\USER\....>\
5.Ikiwa uliandika command hii kiusahihi basi rudi kwenye flash yako ifugue utakuta folder moja lisilo na jina mbele yake, then lifungue hilo na humo ndani utakuta vitu vyoteee.

Njia hii hutumika pia kufungua flash iliyo pigwa shortcut...yaan unakuta flash ukiifungua inakuwa na kishortcut kimeandikwa jina la flsh kama hivi "Removable disk (G)"
Siku njema!
 
Na kama flash ina movies na unataka kuzitazama kwenye Tv utafanyaje ??hii imenitokea leo.Movies zinaonekana 3 tu lakini kuna movies zaidi ya 10.Thanks
 
Hapo inategemea movie zako zipo katika FILE TYPE gani kulingnisha na Tv yako ina support file tyoe zipi.
Mara nyingi movie/video ikiwa katika hali ya AVI basi huwa inaplay katika TV mbali mbali au deki mbali mbali (Hasa za kichina)
Kwahyo angalia hizo zilizo onekana na u note zipo katika file type ipi then ukishajua njoo kwenye computer uangalie zile ambazo hazijaonekana then utakuta zipo katika file type tofauti na zile zilizo onekana.
Njia unayoweza kufanya ni kuzibadili hizo ambazo hazijaonekana kwenda mfumo wa zile zilizo onekana.Mf: Zile kama zilikuwa AVI basi na hizi zingine zifanye kuwa AVI.
Kuzibadilisha unatumia tu Video converters kama vile "AnyVideo converter" au "Factory Fomart".
...Thanks..
 

Upo vizuri kaka mambo yapo safi sasa ni kweli file zilikuwa tofauti...Thanks a lot
 
Mkuu asante kwa darasa,hivi external hard disc inagoma kufungua unatumia procedure hizo kama flash?files zipo uki scan ila haifunguki.Asante mkuu
 
Mkuu asante kwa darasa,hivi external hard disc inagoma kufungua unatumia procedure hizo kama flash?files zipo uki scan ila haifunguki.Asante mkuu

Hiyo external inaleta error yoyote au inagoma je
 

Mimi nilikua nabadili setting za explorer kwenda show hidden files na system files!!!
Asante nimepata njia muafaka.
 
dah nimenot pemben hayo maujuzi nasubiri flash yangu inizngue tu niifanyie utundu fasta..HESHIMA KWENU WATAALAM"
 

Mkuu heshima kwako.

Nina external disc, niliiprotect kwa kutumia "BitLocker Recovery Key", lakini kwa sasa inagoma kufunguka.

Baada ya kuingiza hizo keys inaniandikia "BitLocker Drive Encryption (G): not responding.

Naomba msaada wa kuifungua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…