Msaada: Airtel wamegoma kunirudishia pesa zangu

Ukiambiwa 24hrs basi fanya angalau 72hrs na kuendelea. Hi ndio Bongo.
Pesa yako haitapotea
Nilishawai kupoteza 5000 kwa kujidanganya pesa yangu haitopotea ilikuwa kila nikipiga naambiwa subiri kisha wanatuma zile sms za "YOUR ISSUE WITH TICKET ID XXX HAS BEEN CREATED... baada ya siku 5 ndo nakuja kuambiwa hawawezi kurudisha sabb mtu niliemtumia kimakosa ameshazitumia .
Yaani siku zote hizo wanakusikiliza tu unavyolalamika huku wanajua kabisa hela yako haipo ishatumiwa mbona voda wanatuchana ukweli tu kama haiwezekani kurudisha.
Hawa wa mitandao mingine wananipa wasiwasi pengine wanataka tusubir mpaka tupotezee pesa zetu wazipige wenyewe maana hawaaminiki wakikwambia subiri sio uhakika wa pesa yako kurudishwa.
 
Habari zenu wakuu
Nimepatwa na haya matatizo ya kutuma pesa kimakosa
Imetokea nilikuwa natuma pesa kwa mtu 108,000 nikakosea nikatuma 180,000 kupitia AIRTEL -AIRTEL, baada ya kuona nimekosea nikazuia muamala ili pesa irudishwe then nirudie kutuma hela niliotaka kutuma .

Baada ya kuzuia muamala nimewapigia Airtel huduma kwa wateja wakanambia pesa itarudishwa badaa ya masaa 12.

Sasa tangu nimetoa taarifa mpaka leo zimepita siku mbili kila nikiwapigia kutaka kujua wamefikia wapi Kwenye kutatua tatizo langu wananiambia niendelee kusubiri.

Sijui nitaendelea kusubiri mpaka lini Nimejaribu kuwaomba waruhusu muamala umfikie niliekuwa namtumia wanasema nisubiri itarudishwa kwangu
Naombeni ushauri wenu ndugu zangu nifanye nini ili nipate pesa zangu
Nenda kwa sirro kawashtaki
 
Airtel ni tatizo sana…..kuna siku nilikua nafanya malipo zola kwa kutumia airtel app bahati mbaya nikachagua mobisol badala ya zola na nikaweka akaunti ya zola then nikalipia…..basdae nikaja gundua nimekosea baada ya kuona sipati msg ya token,nikawapigia airtel na kuwaleza wakaniambia watashughurikia,aisee mpaka leo miezi minne au mitano sasa hiyo hela hajarudi!nimepiga simu nikachoka….
Airtel ukifanya uzembe wa aina yeyote jua inakula kwako mazima wao hawanaga habari😅
 
Subiri watarudisha. Kati ya vitu ambavyo huwa sitaki kukutana navyo ni makosa ya utumiaji pesa kwa mifumo ya huduma zetu hapa Tanzania lazima jasho likutoke.

Niliwahi kukosea kutuma laki 6 niliipata ila zilipita siku kama 6.
Ukitafuta ugumu wa kurudisha fedha unaukosa. Alietuma ndie anaomba urudishwe, lakini inachukua muda mrefu. Hata mfumo wa kurudisha mwenyewe una mlolongo mrefu wa matarakimu, unakwaza. Hela hutumwa kutatua tatizo, kuzishikilia siku 6 ni kukwamisha mtu na shida au shughuli zake.
 
Tozo za kutuma 180k walikata, jamaa akaona bora arudishe mzigo wote wamkate tena tozo za kutuma 108k kuliko kukatwa tozo za kutumiwa 72k. Basi tozo ziendeleee.
Usitoe uamuzi ukiwa kwenye stress, itakugharimu. Angetulia njia ulioshauri ndio ilikuwa sahihi.
 
Airtel ni tatizo sana…..kuna siku nilikua nafanya malipo zola kwa kutumia airtel app bahati mbaya nikachagua mobisol badala ya zola na nikaweka akaunti ya zola then nikalipia…..basdae nikaja gundua nimekosea baada ya kuona sipati msg ya token,nikawapigia airtel na kuwaleza wakaniambia watashughurikia,aisee mpaka leo miezi minne au mitano sasa hiyo hela hajarudi!nimepiga simu nikachoka….
Miaka 5 nyuma nililipia TCU ada ya maombi ya vyuo kupitia Airtel, hela ikaenda. Nilisubiri code kimya. Kuwasiliana nao wakasema hawana mfumo huo, hela zitarudishwa, mpaka leo.
 
Wasumbue kila baada ya masaa matatu nenda kwenye page yao Airtel nenda kalalamike pesa yako itarudi ukikaa kimya imekula kwako.
 
Airtel ni wapumbavu sana wiki 2 zilizopita nilikuwa napeleka hela kwenye Tpesa muamala ukagoma nilianza kuambiwa nisubiri masaa 24 ya kazi nimesubiri yakaisha kila siku napiga simu tu hamna cha maana cha kunisaidi kuna siku nimelitukana lijamaa la customer care
 
na hao customer care wana majibu ya hovyo sana kama una hasira lazima mpishane kauli
 
Back
Top Bottom