Ndugu zanguni wana jukwaa poleni na mishughuliko ya mwanzo wa mwaka na hongereni kwa kuumaliza mwaka. Ndugu zanguni naomba ushauri, mtoto ana miezi tisa na mama ni mjamzito tena, je nifanyaje? mtoto akiachishwa kunyonya haitomuathiri kiakili na ukuaji? natanguliza shukrani zangu za dhati ndugu zangu
Anyway, kwa mm naona hakuna namna. Muachisheni kunyonya na kumuanzishia maziwa mbadala ili mama mtu ajiandae kwa kijacho mtarajiwa. Ila itapendeza sana baadae coz watoto wanakuwa kama mapacha flan ivi na watakuwa marafiki sana japo ni mtu na mdogo.
Nenda kwa daktari atakupa A to Z epuka utalaam wa kidaktari kuupokea kijiweni au bar maana juzi kuna li mtu linaniambia eti balimi inaongeza nguvu za kiume.
nawashukuru ndugu zangu imetokea tu bahati mbaya maana sikuwa na nia hii ya kuwazaa kwa ukaribu na nilifuata kalenda vizuri sijui hata nini kimetokea nawashukuru kwa ushauri wenu mbalikiwe lkn bado nakaribisha ushauri zaidi
Nenda kwa daktari atakupa A to Z epuka utalaam wa kidaktari kuupokea kijiweni au bar maana juzi kuna li mtu linaniambia eti balimi inaongeza nguvu za kiume.