Msaaada jamani ndoa iko hatarini kuvunjika

Mimi ni mwanamke kaka.

Okay, jivalishe viatu vya huyo mke, mume wako kila siku anaongea na mwanamke anayemwita rafiki (sio mfanyakazi mwenake, of course hata kwa mfanyakazi mwenzake kuna limit), ungefanyaje? Manongezi yenyewe dk 5 kwenda juu.
 

Hamna watu nawachukia kama wanaodai eti wanalinda ndoa kwa ajili ya watoto wao huo ni upuuzi na uwongo uliopitiliza. Upo hapo kwasababu bado unampenda jaribu kumbadilisha, ikishindikana basi kubaliana na ukweli ndio tabia ya mwenzi wako na maisha ya endelee.
 
Huyo MKEO anakupenda saana na analinda maisha yako. Shukuru Mungu kwa kukupa mke mwema kama huyo. Ingekuwa huyo mke si mwema kwako, angekuwa akiona unaongea na mwanamke nayeye anatafuta kidumu pembeni. Kwa mtazamo wangu kaa na mkeo muzungumze na kama haitoshi jaribu kushirikisha wakubwa wenu wamkalishe mkeo nazani atakuelewa na atabadilika. Hilo wazo lako la kumwacha sikushauri tena never usijaribu hicho kitu ni hibilisi hilo, utatesa watoto.

Hongera kwa kupata mke mwema tena MWAMBIE MUNGU ASANTE KWA KUKUPA MKE MWEMA.
 
Inawezekana wewe ulikuwa mtu wa kuchepuka hapo awali ndio maana hana imani na wewe tena

Wanasema ukiumwa mara moja na nyoka ......
 
Hao 'marafiki' na Wife,kipi bora?...........Acha kabisa kuwasiliana nao bila sababu za msingi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…