Mrisho Gambo atema milioni moja ya Mkurugenzi wa jiji la Arusha

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Mbunge wa Arusha Mjini Mrisho Gambo amegoma kupokea sh,milioni 1 aliyopewa kama zawadi na halmashauri ya jiji la Arusha kutokana na mchango wake katika sekta ya elimu, badala yake ameelekeza fedha hizo zitumike kuondoa changamoto za wananchi katika sekta ya elimu.

Hivi karibuni Gambo aliibua madudu ya mkurugenzi wa jiji hilo,Dkt John Pima akimtuhumu kutumia ovyo fedha za umma.

Gambo akiongea na wafanya biashara katika soko la Krokon alidai kuwa Dkt Pima ametumia mamlioni ya fedha kuwawekea kwenye akaunti baadhi ya watendani wa halmashauri hiyo kinyume cha sheria wakati wananchi wa halmashauri hiyo wanakabiliwa na changamoto lukuki za afya na miundo mbinu duni .

"Naomba hiyo milioni 1 mliopanga kunipatia mimi ipelekeni kwenye ujenzi wa vyoo na choo cha wanafunzi wenye mahitaji maalumu na mimi nitachangia "alisema Gambo.

 
🤣🤣🤣nafsi imemsuta.

Huyu 2025 lazima ahamie Chadema
 
Huyu 2025 asahau kabisa hilo jimbo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…