Wanajamii nawasalimu.
Kila mtu huwa na Ndoto na njozi.Kwa Muda wa wiki mbili sasa
nimekuwa nikiota ndoto ya ajabu.Ndani ya ndoto hiyo namuona binti mrembo akiwa amesimama kando ya bahari huku gauni lake la samawati likipeperushwa na upepo mwanana wa bahari.Sura yake ni ya mviringo na yakuvutia.Macho yake yanaita vilivyo.Vidani vyake vinawaka mithili ya nyota.Hereni masikioni,mkufu shingoni,bangili mikononi na vikuku miguuni.Mara nyingi namuota akiwa anacheza taratibu na kwa mahaba.Mara nyingine huwa amesimama tu akiangalia baharini huku upepo ukipuliza nywele zake za singa.Kila napojaribu kumgusa ndo huwa nashtuka nakujikuta niko mwenyewe kitandani.Sura yake sijawahi kuiona sehemu nyingine zaidi ya kwenye hiyo ndoto.Kinachonishangaza ni kwamba ndoto hii hujirudia mara kwa mara.
Jamani naomba wenyekujua kutabiri ndoto wanidadavulie maana naanza kupata woga.Au ndo jini mahaba huyu?