Mrema amuomba Magufuli atimize ahadi ya kumpa kazi kama alivyomuahidi kipindi cha kampeni

Mtarban

JF-Expert Member
Jan 14, 2015
3,846
5,057
Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP) taifa, Augustine Mrema amemuunga mkono Rais John Mgufuli kwa kasi yake ya kupambana na ufisadi na kumuomba ampe kazi ili amsaidie kutekeleza jukumu hilo.

Mrema alimuomba Rais Magufuli atambue uzoefu wake kwa kukumbuka jinsi alivyopambana na mafisadi wakati akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Naibu Waziri Mkuu.

Huku akieleza CV yake hiyo, Mrema alimkumbusha Rais kuhusu ahadi aliyompa wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka jana, ya kumpa kazi katika Serikali ya Awamu ya Tano ikiwa atashinda na kuwa Rais.

Akizungumza na waandishi wa habari kijijini kwake Kiraracha mkoani Kilimanjaro, Mrema alisema kuwa anasikitishwa na ukimya wa Rais Magufuli kwa sababu aliamini kuwa angetekeleza ahadi hiyo ya kumpa kazi muda mfupi baada ya kutangaza Baraza la Mawaziri, jambo ambalo hadi sasa hajalifanya.

Alisema, alikutana na Rais Magufuli mwaka jana katika kampeni jimboni Vunjo kwenye eneo la Njia Panda lililopo ndani ya mji mdogo wa Himo na kuambatana naye kwenye mkutano wa hadhara, ambapo alimwombea kura kwa wafuasi wake na kuahidiwa ajira.

“Katika kampeni, Dk Magufuli alifika kwenye mkutano wangu nikamwombea kura kwa kuwaambia watu wangu wamchague kwa kuwa ni mchapakazi na mwadilifu. Aliahidi kunipatia kazi katika Serikali na sasa namkumbusha na kumuuliza mbona yupo kimya?” Mrema alieleza na kuhoji.

Alipoulizwa ni kazi gani inayomfaa katika Serikali ya Magufuli, alisema yeye alishawahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Naibu Waziri Mkuu hivyo yuko tayari kufanya kazi yoyote itakayomfaa ila alitamani zaidi kupangwa sehemu nyeti ili amsaidie kutumbua majipu.

Mrema alimpongeza Rais Magufuli kwa jitihada binafsi za kutumbua majipu anazozifanya na alijigamba kuwa yeye ndio mwenye uzoefu wa kupambana na mafisadi kutokana na rekodi yake nzuri ya kipindi cha Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi.

Katika hatua nyingine, Mrema alikanusha taarifa ya kuhongwa fedha ili kufuta kesi ya kupinga matokeo aliyoifungua dhidi ya Mbunge wa jimbo hilo, James Mbatia.

Alisema, taarifa hizo ni za kupuuzwa kwa sababu zinalenga kumpaka matope kwa wananchi wake wa Vunjo.

Mrema alieleza kuwa walifikia maridhiano ya pamoja kuhusu kuondoa kesi hiyo mahakamani na kwamba, hilo lilifanywa kwa kuzingatia maslahi ya wananchi.

Pamoja na hayo, alikiri kumlipa Mbatia Sh mil 40 ikiwa ni sehemu ya kupunguza gharama alizotumia katika kesi hiyo, ikiwemo malipo ya mawakili wake.

Chanzo: Mpekuzi
 
Na dialo amkumbuke kama alivyosema. Lakini hata ombi la jk kuwa pombe awakumbuke vijana wa mitandaoni nalo alikumbuke.
 
Atampa ajira kwa kulipana fadhili kwa gharama ya walipa kodi alafu atuambie anaokoa gharama.
 
Mrema labda asaidiwe tu akatibiwe India na akirud Magu amlipie deni la 40m anazodaiwa na Mbatia.
 
Huyu mzee anahangaika sana kwa kutumiwa na CCM.sasa CCM yenyewe wamechoka kumbeba.
 
Mrema wa TLP Amuomba Rais Magufuli Atimize Ahadi yake ya Kumpa KAZI Kama Alivyokuwa Amemwahidi Wakati wa Kampeni | MPEKUZI.

Najua Magufuli amesikia kilio cha huyu mpinzani feki, na natumai kuwa atamuonea huruma ili aweze kumpa hata kanafasi kadogo kama alivyomuahidi. RAIS mwenzako wa Zanzibar amemtumia hamad na amemkumbuka kwa kumlipa fadhila, hivyo na wewe muoneee huruma huyu mzee vinginevyo atakufa kwa presha
tatizo kazeeka sana, yaani kakongoroka mno ukimuangalia, so Magufuli ameona hilo ndio maana hajampa kazi
 
a417c2cfc89f87da7a5f3cfc3a80a80e.jpg

Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP) taifa, Augustine Mrema amemuunga mkono Rais John Mgufuli kwa kasi yake ya kupambana na ufisadi na kumuomba ampe kazi ili amsaidie kutekeleza jukumu hilo.

Mrema alimuomba Rais Magufuli atambue uzoefu wake kwa kukumbuka jinsi alivyopambana na mafisadi wakati akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Naibu Waziri Mkuu.

Huku akieleza CV yake hiyo, Mrema alimkumbusha Rais kuhusu ahadi aliyompa wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka jana, ya kumpa kazi katika Serikali ya Awamu ya Tano ikiwa atashinda na kuwa Rais.

Akizungumza na waandishi wa habari kijijini kwake Kiraracha mkoani Kilimanjaro, Mrema alisema kuwa anasikitishwa na ukimya wa Rais Magufuli kwa sababu aliamini kuwa angetekeleza ahadi hiyo ya kumpa kazi muda mfupi baada ya kutangaza Baraza la Mawaziri, jambo ambalo hadi sasa hajalifanya.

Alisema, alikutana na Rais Magufuli mwaka jana katika kampeni jimboni Vunjo kwenye eneo la Njia Panda lililopo ndani ya mji mdogo wa Himo na kuambatana naye kwenye mkutano wa hadhara, ambapo alimwombea kura kwa wafuasi wake na kuahidiwa ajira.

“Katika kampeni, Dk Magufuli alifika kwenye mkutano wangu nikamwombea kura kwa kuwaambia watu wangu wamchague kwa kuwa ni mchapakazi na mwadilifu. Aliahidi kunipatia kazi katika Serikali na sasa namkumbusha na kumuuliza mbona yupo kimya?” Mrema alieleza na kuhoji.

Alipoulizwa ni kazi gani inayomfaa katika Serikali ya Magufuli, alisema yeye alishawahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Naibu Waziri Mkuu hivyo yuko tayari kufanya kazi yoyote itakayomfaa ila alitamani zaidi kupangwa sehemu nyeti ili amsaidie kutumbua majipu.

Mrema alimpongeza Rais Magufuli kwa jitihada binafsi za kutumbua majipu anazozifanya na alijigamba kuwa yeye ndio mwenye uzoefu wa kupambana na mafisadi kutokana na rekodi yake nzuri ya kipindi cha Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi.

Katika hatua nyingine, Mrema alikanusha taarifa ya kuhongwa fedha ili kufuta kesi ya kupinga matokeo aliyoifungua dhidi ya Mbunge wa jimbo hilo, James Mbatia.

Alisema, taarifa hizo ni za kupuuzwa kwa sababu zinalenga kumpaka matope kwa wananchi wake wa Vunjo.

Mrema alieleza kuwa walifikia maridhiano ya pamoja kuhusu kuondoa kesi hiyo mahakamani na kwamba, hilo lilifanywa kwa kuzingatia maslahi ya wananchi.

Pamoja na hayo, alikiri kumlipa Mbatia Sh mil 40 ikiwa ni sehemu ya kupunguza gharama alizotumia katika kesi hiyo, ikiwemo malipo ya mawakili wake.

6d5a55636807884df91439fca33812f2.jpg
 
Back
Top Bottom