Mrema aibuka na Kikwete!

Mrema aibuka na Kikwete!

sokoinei

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2012
Posts
1,832
Reaction score
566
Mwenyekiti wa TLP na Mbunge wa Vonjo Mh Agustino Liatonga Mrema amekosoa hotuba ya Rais Kikwete aliyoitoa Jijini Mbeya katika Kilele cha maadhimisho ya siku kuu ya Wafanyakazi Meimosi siku ya Jumatano.

Akizungumzia Hotuba hiyo ya Rais Kikwete alisema kwamba haina la maana la kumsaidia Mfanyakazi,zaidi sana imejaa NADHARIA badala ya Vitendo!!

Sourc: Gazeti la Majira.
 
Vitendo atavipata wapi wakati yeye ni mtu wa nadharia?
 
Mzee Mrema ulikuwa wapi? Yaani huko bungeni hatukusikii kabisaab? Sijajua tatizo ni nini? Mrema wa leo sio kama wa zamani? Mrema wa 95 alikua akikohoa wananchi wameshahoji kuna nini,akienda vjijini anawekewa kanga chini anapita? Lakini leo wananchi wanamashaka na uwepo wake bungeni? Yupo kwa maslahi yake mwenyewe? Wananchi wa jimbo lake? Au kwa niaba ya serikali ya kikwete.
 
Mwenyekiti wa TLP na Mbunge wa Vonjo Mh Agustino Liatonga Mrema amekosoa hotuba ya Rais Kikwete aliyoitoa Jijini Mbeya katika Kilele cha maadhimisho ya siku kuu ya Wafanyakazi Meimosi siku ya Jumatano.

Akizungumzia Hotuba hiyo ya Rais Kikwete alisema kwamba haina la maana la kumsaidia Mfanyakazi,zaidi sana imejaa NADHARIA badala ya Vitendo!!

Sourc: Gazeti la Majira.
Mrema kweli sasa ameanza kuchoka na akili baada ya kuchoka mwili
 
Sisi wafanyakazi tuna imani naye na tunaona anafanya kwa vitendo. Viongozi wa upinzanindo wapo kinadharia zaidi

Sema mimi mfanyakazi sio sisi Wafanyakazi. Kama ni kweli anawathamini kivitendo ilikuaje basi akawaambia hata hizo kura zenu haziitaji?

Tatizo la watu wanaotumika kama Mipira ya Kiume [Kondom] utawajua tu! Kila likija la kumkosoa Kiongozi wa ccm hata kama ni la ukweli utamjua tu kwa Matapishi yake.

Alichosema Mzee Mrema ni ya kweli tena kweli tupu.ila kwa kua wewe ni Gamba lazima umtetee Gamba mwenzio Kikwete!
Alituahidi maisha bora je sasa kuna Maisha bora au ni BORA maisha?

CCM HAIKUBALIKI SOTE TUSHIRIKIANE KUITOKOMEZA!!!
 
Back
Top Bottom