Mrejesho: Ukiambiwa tuwe marafiki tu basi, maana yake nini?

Jurrasic Park

JF-Expert Member
Sep 13, 2013
3,792
6,768
Habari za humu wanajamvi,

Rejea uzi huu wa tarehe 2/8/2016

Nashukuru wale wote waliochangia na kunishauri katika uzi ule. Sasa naomba niwape muendelezo wa hili.

Mnamo tarehe 1 september siku ya 'kupatwa jua' nilipata likizo fupi ya kikazi. Basi kwa kuwa nilikuwa nawasiliana na huyu dada akanikaribisha niende kwao. Kwa kweli sikutaka sana kwenda kwao maana nia yangu ilikuwa nipite nisepe mbele basi nikawa mpole ikabidi nifikirie kwa kina.

Maamuzi niliyoyachukua niliamua kwenda kwao kama alivyoniomba. Basi nikapanga uongo wangu wote ukapangika na kwa kuwa nia yangu nit*mb# nikimbie basi nikawa mpole. Nikafunga safari huku mimi nikidanganya ni mwanafunzi nimemaliza chuo. Kweli nilifika kwao nikala nikalala.

Siku ya kwanza ikapita tukawa marafiki tu. Mama na baba yake wakatambulishwa na wakanipenda sana kwa kuwa mimi kimwonekano naonekana mtulivu. Basi maisha yakasonga huku najaribu kuwashawishi kwamba mimi ni mpole maana maneno yalienda na vitendo.

Sasa cha ajabu nikawa naitwa kaka japo nilikuwa sipendi sana kuitwa hivyo. Kama wiki moja kukaa kwao nikajikuta nimempenda yule dada kikweli. nampenda mpaka sasa. Nilivumilia hivyo hivyo kuitwa kaka nami naita dada.

Siku moja usiku nilikuwa nasikia akiongea na yule ampendaye. Dah japo nilisikia presha inapanda ikabidi nichukue earphone zangu nisikilize mziki ili nisiwasikie. Tukiwa tunakaa mezani na baba na mama yake yeye ni kuchat tu japo lilikuwa linaniuzi sana na nilikua nikishakula naamua kwenda kulala maana machozi yalikua yakinilenga. Wakiniuliza mbona machozi yanatoka nasema ni macho yanauma. Basi nilivumilia sana.

Siku moja tena akapigiwa simu na mpendwa wake katika maongezi nikajua kwamba jamaa yake analalamika anataka akamtembelee huko Shinyanga, sehemu flani (sitaitaja). Sasa kwa kuwa nilikua ndani nikatoka kwenda kuvunga huko nje. Na yeye alipotoka ndani akanikuta nje akaniangalia jicho flani la husda. Mi nikaelewa tu mambo ya kawaida. Asubuhi nikiamka naenda kumsaudia afungue biashara yake nakaaa hapo naye sema ana msimamo sana ndo nachompendea hapo.

Baada ya kukaa hapo wiki tatu huku akiendelea kuwasiliana na bwana ake. Kuna siku aliniambia anataka kwenda huko (huko shinyanga) nikajua anaenda kwa jamaa ake kutimiza haja zake (nadhani mmenielewa ). Siku hiyo dah aisehh nililia usiku mpaka nikajuta kwenda kwao. Asubuhi yaje nikawa nataniana na mama yake huku akiniambia nikimaliza shule anitafutie mke.

Basi nikapanga niondoke kabla yake. Siku moja usiku nikatia alarm simu yangu iite kama mtu ananipigia alafu niongee kama mama na baba yangu wananitaka nyumbani. Kesho yake akaniuliza vip mbona jana ulikuwa sio poa. Nikamjibu baba ananitaka nyumbani.

Jioni ya siku hiyo ikabidi nichukue tigo yangu nikapiga *35*0000# hivyo ukimpigie mtu voicemessage inasema simu imefungiwa. Baadaye nikamwambia tigo yangu imefungiwa kwa kuwa nilikua na tigo nyingine nikaivunja kama geresha mbele yake. Kweli akaifuta namba yangu akawa amebakiwa na voda zangu mbili. Siku iliyofuata nilikata ticket na usiku wake nikapiga simu voda nikawaambia funga line zangu. Alfajiri niliamka nikawaga nikasepa zangu.

Kinachoniuma nimepoteza mda wangu bora ningefanya mambo ya maana. Sasa likizo imeisha sijafanya chochote mpaka sasa. Na sitaki mwanamke aniambie niwe dada yake. Niameondoka roho inaniuma nilichokitaka sijakipata na bado nampenda.

Wewe S#### hutakaa unione tena wala kunipata ulitaka kunifanya asset ili kwa kisingizio cha kaka unimanipulate unavyotaka. Sasa nimekoma na nitakuchukia sana. Sasa hunipati kabisa ngoja nitengeneze maisha yangu kwanza. Hii inaniuma sana kujifanya mtakatufu kumbe mimi shetani.

Nimekoma na ole wake atakaye niita kaka sijui nini nini atanijua ntabaka ikiwezekana. Huwezi kunitumia utakavyo ukipata shida eti kwa kuwa ni kaka wa ku download ndo uniambie. Kama una mtu wako akutatulie shida zako zote sio unitese hivi. Umenifanya nakufikiria wewe kila muda.

Nimekoma na sirudii tena

Asante
 
Unachekesha wewe ndio umepatwa, sababu ulikuwa unataka kumdu na kukimbia. Tulia iwe funzo ya kutopanga mipango mapema kichwani mwako
 
huo ni udomo zege siku nyingine ukimpenda mtu kimapenzi usione aibu sema nae

Hivi inapokuja unaapproach demu alafu anakuweka friendzone hapo unafanyaje zaidi ya kuwa mpole. ukiona hasomeki unasepa tu pasipo shari.
 
Ila hukumpenda mwanzoni ulitaka kula na kusepa...

Na kweli kwa jinsi nilivyokaa naye nilimpenda automatical mpaka nikajishangaa but ndo ivyo tena amenitumia alivyotaka sasa nimeshaondoka huku nikimpenda lakini nishakata mawasiliano kabisa huu mwezi ushaisha but bado namkumbuka sana sema sina namba zake tena na sitarajii kumtafuta
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom