MREJESHO TOKA TAHLISO

MREJESHO TOKA TAHLISO

moyafricatz

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2015
Posts
2,905
Reaction score
4,928
Tarehe 14/11/2018 Mwenyekiti wa Tahliso ndg George Mnali akiambatana na kamishna idara ya mikopo na udahili Tahliso ndg Leckton Moris walifanya ziara ya kutembelea bodi ya mikopo na kuweza kukutana na viongozi wa bodi ya mikopo ambapo waliwasilisha changamoto kadhaa zinazowakabili wanafunzi wanufaika wa mikopo katika vyuo vyetu ambapo tuliweza kupata mrejesho kama ifuatavyo.

Kuhusu suala la kuchelewa kwa malipo ya fedha ya kujikimu kwa baadhi ya vyuo tumeweza kuliwasilisha na kufanyiwa kazi ambapo malipo hayo yatafanywa ndani ya batch ya pili inayolipwa kuanzia tarehe 15/11/2018.

Kuhusu suala la kupunguzwa kwa viwango vya mkopo kwa baadhi ya wanufaika katika vyuo kadhaa kwa mujibu wa malalamiko tulizozipata mpaka sasa na suala hilo limepewa majibu na director wa allocation, Dr.Veronica aliyesema kuwa mchakato huo utafanyiwa marekebisho na viwango hivyo vitarudishwa katika viwango vya awali .

Kuhusu suala la wanufaika wa batch ya kwanza mwaka wa kwanza ambao allocation zao hazijafika vyuoni nalo limepewa maelezo ambapo wanafunzi hao wanapaswa kurekebisha taarifa zao aidha kupitia kwa loan officers wa vyuo vyao au kupitia dirisha la kukata rufaa litakalofunguliwa wiki ijayo kwa wanafunzi wote watakaohitaji kukata rufaa hiyo.

Tuliweza pia kusisitiza bodi kufanyia kwa haraka kazi zoezi la malipo kwa wanafunzi wanaoendelea pamoja na kutoa majina ya wanufaika wa batch ya nne mwaka wa kwanza, tuliwaomba pia waweze kutoa majina ya wanafunzi wanaoendelea walioomba mkopo kwa mwaka wa masomo 2018/2019 ambako bodi ilikiri kufanya hivyo mapema iwezekanavyo.*

*Imetolewa na kamishina idara ya Mikopo na udahili Tahliso ,Leckton Moris*
 
Kwa waliopata batch ya kwanza taarifa gani wanatakiwa kurekebisha? yaani mpaka jina linatoka taarifa zilikua na shida? walifanyia kazi na kujiridhisha kwamba anastahili mkopo tena batch one kwa taarifa ambazo hazikukamilika? Only in Tanzania
 
Kunauzembe wamrfanya TCU amabo unagarimu watu bila sababu za msingi....walituma codes ili mtu afanye confirmation ya chuo kimoja kwa wale waliokuwa na multiple selection. Sasa ajabu inakuja mtu amecormfirm chuo kimoja lakini vyuo vyote vinapeleka jina lake loans board. Cha kusikitisha zaidi mkopo unaenda chuo kingine na siyo kile ambacho alichagua mwenyewe
 
Back
Top Bottom