Mrejesho: Nimekuta vitu vya mwanaume chumbani kwa mpenzi wangu

Aventus

JF-Expert Member
Mar 8, 2013
2,011
2,165
Hivi karibuni nilileta uzi unaosema;

Nimekuta vitu vya mwanaume chumbani kwa mpenzi wangu, naomba ushauri tafadhali

Huu ni mrejesho bada ya kukuta vitu vya mwanaume mwingine imebidi niombe wiki ya mapumziko ili nifanye uchunguzi wa kina(usiniulize kwanini kila mtu anajua mapenzi yanavyouma baadae nitajibu kwanini moyo wangu umeumia) basi nikamwambia binti nina safari kama ya wiki mbili hivyo hatutaonana kama tulivyozoea ila kama atakua na tatizo atanijulisha, siku ya mwanzo nilifika mitaa ya binti saa moja jioni mpaka saa tano sikufanikiwa.

Ila mida ya saa tatu usiku alitoka nikaona bada ya dk 15 akirudi na shoga yake alipofika karibu na sehemu niliyojibanza akaanza kugeuka geuka sikuelewa ni kwanini, kesho yake alinipigia simu akaniambia amenikumbuka sana pia alisikia harufu ya marashi kama yangu amekumbuka mambo mengi, nikajua tatizo liko wapi, siku ya pili mpaka ya sita sijaambulia chochote nikawa nimekata tamaa lakini nikajipa moyo nimalizie siku ya saba mpaka saa tano hola ikabidi nijiondokee zangu taratibu nafika mitaa flani natega boda nipande.

Naona sijui niseme dogo ama mshikaji amevaa ile flana iliyokuwa ndani kwa binti nikashtuka sana, akili ya haraka haraka nikazuga naongea na simu akapita nikawa namfata nyuma nyuma mwisho akafunguliwa na mpenzi wangu kwa makiss moto moto daah sio siri mapenzi yanauma sana, tayari kwa mimi ushahidi ulikua umetosha sikua na haja ya kuhakikisha zaidi.nimeumia jamaa anifikii kwa lolote kwa muonekano wa sura, utanashati na kila kitu ni muhuni tu flani sijui niseme sharobaro ila hana vifaa yaani ni aibu kujifananisha nae.

Sikua na la kufanya nikajiondokea zangu pasipo ya kujua mchezo nimeujua.sikulala usiku wa tukio usiku ulikua mrefu waliotendwa wanajua asubuhi mapema nikampigia mwenye nyumba maana mimi ndio nilitafuta dalali na chumba nililipa so mimi ndio nilikua natambulika kwa miaka yote, kwa kuwa mwezi huu kodi ilikua ndo inaisha nikamwambia mwenye nyumba sihusiki tena kwenye ulipaji wa kodi wala maji na umeme.

Yeye bado haelewi chochote ila nimesitisha huduma zote kuanzia sasa itabidi ajitegemee kwa mshahara wake na nina imani maisha hayatamshinda, sina mpango nae tena ila sitamwambia chochote nitaongea nae kwenye simu vizuri tu, sitamnyanganya chochote nilichomnunulia kwa pesa yangu vyote ni mali yake namtakia maisha mema.

HISTORIA YA MIMI NA YEYE
Miaka 3 nyuma nilikutana na huyu binti akiishi kwa shangazi yake maana hana wazazi, sijui ila alianza kunionyesha dalili kama ananipenda kwa kuwa sikua katika mahusiano nilimtongoza akanikubali tukawa wapenzi.

Bahati mbaya alikua akiteswa ila asemi, siku nikagundua kupitia kwa watu anatumika kama mfanyakazi wa ndani na mateso mengi, nikambana sana akaniambia ukweli wa maisha yake na jinsi anavyoteseka.

Nikamwuliza unataka nikufanyie nini ili uwe huru na amani akakataa kata kata nikamwambia kaa fikiria kama ni shule ama kazi halafu utaniambia ila bado aligoma akadai yeye kunipenda na kupendwa na mimi ni faraja tosha haitaj kitu chochote isipokuwa ni mimi tu, nikaamua kumtafutia training sehemu kwa lazima kwa kuwa ananipenda ikabidi aende baada ya miezi kadhaa alimaliza.

Ila shangazi yake alizidisha chuki hadi akanitafuta kwenye simu akawa ananitishia sikufa moyo kwa kuwa nimeshapenda ikabidi nimtafutie kazi sehemu. Akaanza miezi mitatu mbele akafukuzwa kwa shangazi yake kwa kuwa mimi nimepatiwa room kazini sikuweza kumchukua kuishi nae.

Nikaingia mfukoni nikamtafuta dalali akatafuta chumba nikapa kila kitu nikanunua godoro na mashuka na mapazia.akaanza maisha yake katika makazi mapya vitu vingine nilimnunulia taratibu.

Nikawa nina jukumu la kulipa chumba, umeme na maji mahitaji mengine natoa ninapoona mambo hayako sawa ila huyu binti hana tabia ya kuomba kitu toka mwanzo hata kama yuko na shida na sielewi kwanini na vyote nilivyompa ni kwa hiyari yangu hakuniomba. Mimi ndo baba yake na ndo kila kitu kwake ila nashukuru KATOKEA MSELA WA KUNISAIDIA MAJUKUMU. Nimeamua kuandika uzi mrefu hivi maana kuna watu hawajui nimetoka wapi na huyu binti.

SABABU ZIMENIFANYA NISIWEZE KUMCHUMBIA baada ya mwaka alibadilika sana kila nikimwambia nakuja kwake anasema yuko kwa shangazi yake. Simu yake anaficha wakati sina tabia ya kuigusa wala kuipekua ingawa kila mara ni mimi ninayenunua hizo simu wakati mwingine anakwenda kupokelea simu zake nje nikimwuliza kwanini anasema anaongea na ndugu zake mambo ya kifamilia.daah!

Kweli mimi ni mvumilivu sana.Najiuliza hayo ni mambo gani? Na ni ndugu zake gani wakati mimi ndo babake nakumbuka alikua amenisave jina MPENZI ila sasa hivi nimeseviwa jina langu la ubatizo tena kwa herufi chache zinazopoteza mana.

Imebidi niwe nakagua simu yake mana niliona amebadilika sana nimemkuta na mabwana wengine wawili tofauti kwa wakati mmoja ila anakataa hawataki ila wanamtongoza. Ila sms zinaonekana yeye ndo anaanza "beib asubuhi njema" beb miss you "unajua nilishindwa kumuwacha sababu ukiwa inlove unaweza ukafumania ila ukapewa maneno matamu ukaridhika na ukasamehe na kusahau ila nafsi yangu ilisita kumuoa tokana na mapicha picha ila sasa inatosha. Kama unataka kuoa nakushauri mchunguze sana mwanamke miaka mitatu haitoshi kumchunguza mwanamke
 
6246ec9849e4882f144a474e323dccba.jpg
Mapenzi yanatesa sana.
 
Huu ni mrejesho bada ya kukuta vitu vya mwanaume mwingine Imebidi niombe wiki ya mapumziko.ili nifanye uchunguzi wa kina(usiniulize kwanini?kila mtu anajua mapenzi yanavouma.baadae nitajibu kwanini moyo wangu umeumia)basi nikamwambia binti nina safar kama ya wiki mbili hivyo hatutaonana kama tulivozoea ila kama atakua na tatizo
Pole bro na nakupongeza kwa kufanya maamuzi sahihi
 
Mapenzi sio muonekano kaka, wala sio utanashati. Mapenzi ni hisia kaka, kwani ww kuna mademu wangapi wana muonekano mzuri tu na hauna hisia nao. Kaka Kama utaendelea kuwasiliana nae ni kosa unaendelea kufanya na Kosa hilo litakurudisha kwenye mapenz tena na huyo Binti.. Jiulize..Kwa nn ukae kimya humwambii kosa lake wakati ushahidi unao? Halafu unataka kuendelea kuwasiliana nae. Inaonekana bado unampenda.. Na haupo tayari kumuacha. Na usipokua makini atakupa ugongwa wa moyo. Kama unataka kupona kweli fanya hivi.. Mpigie simu mwambie kila kitu ulichokiona na mpe msimamo wako kuwa hutaki kuwa nae tena.
 
Pole sana.. Wewe c wa kwanza kupitia kadhia hii.
Niliwah kwenda geto kwa dem bila taarifa.. Mlangoni nikakuta viatu vya kiume.. Ile kugonga dem katoka amechokaa afu akaniambia kwa wakati huo alikuwa na maongezi mhimu ivyo asingewwza kuniona...
Basi kwa unyonge mwingi nikajiondokea...
 
Back
Top Bottom