Mrejesho: Amesomea mineral processing anatafuta kazi

vidudi

Member
Jun 28, 2016
76
125
Ndugu wana JF,

Poleni kwa majukumu na hongereni kwa kuendelea na majukumu hayo.
Kipindi kama cha mwezi mmoja hivi niliwahi kuleta ombi na kuhitaji msaada kwa dada yangu ambae alikuwa anahitaji nafasi ya kazi katika maeneo ya migodi au viwandani kutokana na taaluma yake aliyoipata.

Kwa kukumbuka wema na ushirikiano mulionipatia kipindi kile ninashukuru sana kwa msaada wenu. kwani kuna mdau mmoja wa humu JF lakini kwa kipindi hicho alikuwa nje ya nchi, yeye alinisaidia sana katika ombi langu hilo kwani alinielekeza kampuni mpaka contact za wahusika wa hiyo kampuni.

Jambo la kushukuru zaidi ni kwamba yule dada yangu kapata kazi katika kampuni hiyo ambayo nilielekezwa na huyo Mheshimiwa baada ya kuni PM namuombea sana kwa Mwenyezi Mungu awe na moyo huo huo wa kusaidia wengine pia Mwenyezi Mungu amjalie kila la kheri na amuepushe na kila la shari duniani na kesho Akhera na apate mafanikio zaidi katika mambo na shughuli zake zote zilizo halali.

Na wana JF wote tuige mifano kama hiyo na Allah atujaalie nasi tuweze kusaidiana na kufikia malengo yetu.

Mwisho niwashukuru wote ambao mulinipa ushirikiano katika masuala yangu na yetu mbalimbali.

AHSANTENI SANA.
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
102,000
2,000
Hongera na shukrani kwa kuleta mrejesho. Hii inatoa moyo kwamba unaweza kupata msaada mkubwa sana hapa JF. Wengi wakija kuomba msaada hapa hawarudishi mrejesho kama wamefanikiwa au la. Mrejesho hasa kama huu unatia moyo sana na kuwahamasisha wengine kusaidia pale wanapoweza kufanya hivyo. Kila la heri Mkuu.

Ndugu wana JF
Poleni kwa majukumu na hongereni kwa kuendelea na majukumu hayo.
Kipindi kama cha mwezi mmoja hivi niliwahi kuleta ombi na kuhitaji msaada kwa dada yangu ambae alikuwa anahitaji nafasi ya kazi katika maeneo ya migodi au viwandani kutokana na taaluma yake aliyoipata. Kwa kukumbuka wema na ushirikiano mulionipatia kipindi kile ninashukuru sana kwa msaada wenu. kwani kuna mdau mmoja wa humu JF lakini kwa kipindi hicho alikuwa nje ya nchi, yeye alinisaidia SANA katika ombi langu hilo kwani alinielekeza kampuni mpaka contact za wahusika wa hiyo kampuni.Jambo la kushukuru zaidi ni kwamba yule dada yangu kapata kazi katika kampuni hiyo ambayo nilielekezwa na huyo Mheshimiwa baada ya kuni PM namuombea sana kwa MwenyeziMungu awe na moyo huo huo wa kusaidia wengine pia MwenyeziMungu Amjalie kila la kheri na amuepushe na kila la shari duniani na kesho Akhera na apate mafanikio zaidi katika mambo na shughuli zake zote zilizo halali. Na wana JF wotetuige mifano kama hiyo na Allah atujaalie nasi tuweze kusaidiana na kufikia malengo yetu.Mwisho niwashukuru wote ambao mulinipa ushirikiano katika masuala yangu na yetu mbalimbali.
AHSANTENI SANA.
 
CleverKING

JF-Expert Member
Apr 24, 2014
8,520
2,000
Hongera na shukrani kwa kuleta mrejesho. Hii inatoa moyo kwamba unaweza kupata msaada mkubwa sana hapa JF. Wengi wakija kuomba msaada hapa hawarudishi mrejesho kama wamefanikiwa au la. Mrejesho hasa kama huu unatia moyo sana na kuwahamasisha wengine kusaidia pale wanapoweza kufanya hivyo. Kila la heri Mkuu.
Uko sahihi kabisa mkuu BAK
 
  • Thanks
Reactions: BAK

Chillah

JF-Expert Member
Oct 12, 2016
5,501
2,000
Hongera na shukrani kwa kuleta mrejesho. Hii inatoa moyo kwamba unaweza kupata msaada mkubwa sana hapa JF. Wengi wakija kuomba msaada hapa hawarudishi mrejesho kama wamefanikiwa au la. Mrejesho hasa kama huu unatia moyo sana na kuwahamasisha wengine kusaidia pale wanapoweza kufanya hivyo. Kila la heri Mkuu.
Tuna andaa orodha yao wale wote waliokuwa wanapiga dili 2016 kupitia JF.... tuta anza na hao... maana walitoa ahadi alafu wakapiga kimya ukiwatafuta kimya hawana majibu ila walitumia wengine kujinufaisha wao binafsi....
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom