PreGE2025 Mradi wa upimaji wa ardhi unatarajiwa kuwezesha uboreshaji wa jiji la Mbeya kuwa la kisasa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Nipe Maji

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2025
Posts
335
Reaction score
190
Serikali ya Mkoa wa Mbeya imeanza kutekeleza Mpango Maalumu wa upimaji maeneo ya Shirika la Utangazaji Tanzania TBC lililopo katika jiji la Mbeya, Utengule na Nsalala yaliyopo halmashauri ya wilaya ya Mbeya Vijijini kwa ajili ya Ujenzi wa Miji ya kisasa.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dkt. Juma Zuberi Homera amesema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake ambapo amesema mradi huo wa upimaji unatekelezwa na Chuo cha Ardhi cha mkoani Morogoro.

Pia soma Pre GE2025 Miradi kuelekea Uchaguzi Mkuu: Mhandisi Kundo akagua mradi wa maji unaonufaisha zaidi ya wakazi 200,000 Chalinze

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Dkt.Juma Homera amemshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa namna ambavyo amekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa Mkoa wa Mbeya unapata fursa za kipekee, na kuwa miongoni mwa mikoa ya mfano katika upimaji wa ardhi. Hii ni ishara tosha ya dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kuleta maendeleo ya kweli kwa Watanzania wote bila kumwacha mtu nyuma.

Dkt.Homera amesema Kupitia mradi huu, Mbeya itazidi kuwa kitovu cha fursa, maendeleo na ustawi wa jamii, na itaimarisha mnyororo mzima wa uchumi kuanzia kwa wananchi wa kawaida hadi kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.

Dkt.Homera ametoa wito kwa wananchi wa mkoa huo na wale wanaoishi maeneo jirani kutoa ushirikiano kwa wataalamu wanaotekeleza mradi huu na kuhakikisha kuwa wanazitumia fursa zitakazopatikana kwa manufaa yao na kizazi kijacho
Your browser is not able to display this video.
 
Mama anaendelea kuupiga mwingi Kwa kutafuna mifupa iliyowaahinda wengine.

Stori za Mbeya kuwa Kijiji kikubwa zitaisha Sasa
 
Tatizo la Mbeya ni ULOZI
 
Mama anaendelea kuupiga mwingi Kwa kutafuna mifupa iliyowaahinda wengine.

Stori za Mbeya kuwa Kijiji kikubwa zitaisha Sasa
Natamani watekeleze kweli isiwe tu maneno, Mbeya ikianza kufuata mpango mji nitafurahi sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…