kidadari
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 8,647
- 9,601
Toka mradi wa dart umeanza kwa ujenzi wake kulikuwepo na changamoto nyingi zikionyesha dhahiri kuwa hakukuwa na matayarisho ya kutosha kabla ya kuanza rasmi mradi huo.
Yafuatayo ni mambo yanayoonyesha udhaifu huo.
Kuanza kwa mradi huu baada ya kutumika kwa nguvu za ziada ziara za kushukiza,kutumbuliwa kwa baadhi ya vigogo wa mradi huo, hii ina maana mradi huu ulikuwa bado kuanza ila umeanza kwa nguvu ya ziada.
Upana wa barabara unatia shaka kwa kile kinachoitwa mradi wa mwendo kasi ili hali upana wa barabara hizo haumruhusu dereva kutembea kwa 100km/hr huo ni mwendo kasi gani???
Ubora wa magari bila shaka yana kiwango kinachotiliwa shaka. Kwa ajali chache tena sio za kutisha magari haya yameshindwa kabisa kuonyesha ubora wake, hapa tunaona lifespan ya mradi huu utavyokuwa Mdogo! bora Eicher kuliko haya.
Sheria kibao na matamko yanayoashuria kujihami kwa watawala utadhani mradi huu ni Mkubwa kuliko yote nchinj hata ule wa gasi asilia, mara ibeni tairi za magari yanayokatiza barabara hizo, Sasa kuna sheria inayoletwa ukiingia barabara hizo fine ni 300,000 ila haisemi chochote endapo magari kasi yakigonga magari binafsi, wala kama gari ina comprehensive insurance. Hii ina maana gani? Unfair
Magari kasi hayana Breki? nimeshuhudia ajali kadhaa ambazo kweli gari moja dogo liliingia barabara ya mwendo kasi ila kwa kiburi dereva wa gari kasi hakuhangaika kufunga breki mpaka ajali inatokea. Hii itachangia uharibifu wa magari haya na kuathiri mradi huu!
Huu ni mradi wa serekali au mtu binafsi? Maana kama ni wa serekali tulitegemea namba za magari zisimeke STK au SU.
Hapa panatia shaka endapo ikitokea mgongano wa kimashali au kubadilika kwa utawala!
Ongeza changamoto nyingine.