TAECOLTD
JF-Expert Member
- Mar 2, 2013
- 1,051
- 1,836
Nimekuwa nikisikia uvumi kuhusu kuchoka kwa huyu msanii wa muda mrefu na kudai amekwisha na wengine kudai amekamata umeme (ukimwi) yote ni maneno na huwezi kumziba mtu mdomo asiongee. Leo katika angalia yangu miziki ya bongo nikaunyaka wimbo wa kioo wa Mr Nice..
Kwanza moja nimpongeze kwa ujumbe mzuri uliosheheni katika wimbo wake ambao unatufunza mengi sana.
Binafsi sikuwahi wala sio shabiki wa miziki ya namna ile ila ujumbe ulinigusa, ila niliguswa zaidi na muonekano wa msanii huyo. Anaimba mpaka anatia huruma kwakuwa anachokiongea ni halisia ya maisha yake.
Ila nikaishia kushangaa quality ya video na studio aliyorekodia sijui ni za uchochoroni maana kwa msanii aliyevuma sana hata kama ni kuporomoka ile ni too much.
Kwa mtu ambaye sio mpenzi wa bongo fleva anaweza kusema ni underground anatafuta kutoka. Ujumbe wa nyimbo ni nzuri ila director alikosea kila kitu kuanzia location, story ilivyotakiwa iendane na ujumbe halisi, quality mbovu ya video, kiitikio chake sio kibaya sana ila ilitakiwa kifanyiwe marekebisho.
Kwa nyimbo yake hii Nadhani Mr Nice anazidi kujidhalilisha zaidi na zaidi na sio kurudi kwenye game bali ni kupotea kabisa..kama director alikuwa mbovu angeomba hata ushauri kwa watu mbalimbali ili story iliyokuwa kwenye video ibebe ujumbe halisi wa nyimbo.
Nyimbo ya kioo ni nzuri lakini ina makosa mengi sana ambayo hayakupewa kipaumbele.
Asante.