GE2025 Mpina ni "Right Person in The wrong Political Party"

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Wolle Melkas Fernando

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2016
Posts
279
Reaction score
389
Mpina kuvaa Tshirt yenye picha ya hayati Magufuli anaweza kuwa ni 'Right Person in the wrong Party'

Luhaga Mpina ni mgombea Urais kwa Chama Cha ACT wazalendo. Tangu akiwa Mbunge Mpina ni mtu aliyejitanabahisha kuwa ni mfuasi wa falsafa za uongozi wa Magufuli.

Sidhani Mpina kama amepata muda wa kusoma itikadi na falsafa za Chama chake kipya Pamoja na kupitia misimamo ya viongozi wake wa Chama kuhusu utawaka wa Serikali ya awamu ya Tano mbayo iliongozwa na Dr. Magufuli.

ACT ni Moja ya Chama kilichokuwa mstari wa mbele kupinga vikali misimamo ya Magufuli na namna yake ya Uongozi.

Ni ACT hiyo hiyo iliyokuwa ikipinga msimamo wa Magufuli kuwachukulia hatua Mafisadi Kwa kusema Serikali ya Magufuli ilikuwa inakiuka Haki za Binadamu.

Ni ACT hiyo hiyo ambayo ilipinga vikali zoezi la Serikali ya Magufuli kuwaondoa wafanyakazi waliokuwa wameajiriwa kwa mbinu za kughushi vyeti vya taaluma ambapo lengo la Magufuli lilikuwa ni kuboresha weledi na ufanisi wa utendaji wa kazi Katika kuwahudumia Wananchi.

Ni ACT hiyo hiyo iliyopinga msimamo wa Magufuli wa kutokusafiri nje mara kwa mara kwa lengo la kubana matumizi.

Na hata baada ya Kifo Cha Magufuli, Kiongozi wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe ambaye pia ni muasisi wa hicho chama alinukuliwa akisema "Kama Kuna watu walimpenda sana, na wao waende kaburini wakazikwe naye"

Leo hii Mgombea Urais wa ACT mwenye itikadi za uongozi wa Magufuli aliyepigwa vita na Chama hichohicho, amevaa T-shirt yenye picha ya Magufuli.

Hii kwetu sisi Wahafidhina inatupa tafsiri kwamba Mpina anaweza kuwa ni mtu Sahihi aliyepotea Chama. "Right Person in The Wrong Political Party"
 
Mwanasiasa yeyote kama Mpina ambaye anatumika na watawala kufubaza upinzani wa kweli si wa kuchekewa hata kidogo. Ni adui namba 1 wa demokrasia. Kama alivyo Mbowe na genge lake na wahuni na madalali
 
Mpina kawasrpa manyumbu Sasa yamebaki kutapatapa tu na ramli chonganishi. Mpina ni mjanja, ana akili na busara na kubwa zaidi ni mtu mwenye akili huru hivyo hawezi kwenda Chama km chadema ambacho lazima uwe zuzu wa kumnyooshea nyoosha tu vidole juu na kupigwa tone tone.
Kwa kifupi mpina amewaumbua chadema.
 
Mpina ni aliona kwa kuwa chadema hawaingii kwenye uchaguzi, basi wale wanaomuunga mkono lissu, watahamia kwake sababu alionesha UZALENDO kwenye ishu ya bashe, akaina heri ACT kuliko chadema ambao hawashiriki uchaguzi.. hsjui kuwa kuishinda CCM kwa uchguzi huu usio huru na hako ni HAIWEZEKANI
 
Mpina kuvaa Tshirt yenye picha ya hayati Magufuli anaweza kuwa ni 'Right Person in the wrong Party'

Luhaga Mpina ni mgombea Urais kwa Chama Cha ACT wazalendo. Tangu akiwa Mbunge Mpina ni mtu aliyejitanabahisha kuwa ni mfuasi wa falsafa za uongozi wa Magufuli.

Sidhani Mpina kama amepata muda wa kusoma itikadi na falsafa za Chama chake kipya Pamoja na kupitia misimamo ya viongozi wake wa Chama kuhusu utawaka wa Serikali ya awamu ya Tano mbayo iliongozwa na Dr. Magufuli.

ACT ni Moja ya Chama kilichokuwa mstari wa mbele kupinga vikali misimamo ya Magufuli na namna yake ya Uongozi.

Ni ACT hiyo hiyo iliyokuwa ikipinga msimamo wa Magufuli kuwachukulia hatua Mafisadi Kwa kusema Serikali ya Magufuli ilikuwa inakiuka Haki za Binadamu.

Ni ACT hiyo hiyo ambayo ilipinga vikali zoezi la Serikali ya Magufuli kuwaondoa wafanyakazi waliokuwa wameajiriwa kwa mbinu za kughushi vyeti vya taaluma ambapo lengo la Magufuli lilikuwa ni kuboresha weledi na ufanisi wa utendaji wa kazi Katika kuwahudumia Wananchi.

Ni ACT hiyo hiyo iliyopinga msimamo wa Magufuli wa kutokusafiri nje mara kwa mara kwa lengo la kubana matumizi.

Na hata baada ya Kifo Cha Magufuli, Kiongozi wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe ambaye pia ni muasisi wa hicho chama alinukuliwa akisema "Kama Kuna watu walimpenda sana, na wao waende kaburini wakazikwe naye"

Leo hii Mgombea Urais wa ACT mwenye itikadi za uongozi wa Magufuli aliyepigwa vita na Chama hichohicho, amevaa T-shirt yenye picha ya Magufuli.

Hii kwetu sisi Wahafidhina inatupa tafsiri kwamba Mpina anaweza kuwa ni mtu Sahihi aliyepotea Chama. "Right Person in The Wrong Political Party"
Kwanini iwe Mpina ndio yuko sahihi na sio hicho chama? Au ww unampenda Mpina hadi unadhani yeye ndio yuko sahihi tu? Nijuavyo mimi, Mpina ni mgombea mwenye mvuto kwa wapiga kura, hasa wa kanda ya ziwa kwakuwa ni msukuma, na kwa nyakati kadhaa amepigania maslahi ya umma.
 
mpina wamteue tu viti maalum anachangamsha sana genge
 
Back
Top Bottom