Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali kwa hili umechemka

Mnyamahodzo

JF-Expert Member
May 23, 2008
1,932
987
Ofisi ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali ndiyo yenye jukumu la kuchapisha nyaraka mbalimbali za Serikali ikiwapo Sheria mbalimbali na Gazeti la Serikali. Machapisho yake huyauza kupitia Maduka ya Serikali (Government shops).

Maduka hayo yalikuwapo katika mikoa mbalimbali ikiwa Mwanza, Arusha, Dodoma na Dar.

Kwa kile kinachodaiwa kupunguza matumizi/gharama za uendeshaji Ofisi hii imefunga maduka yake ya Mwanza, Arusha na lile la Dar imelihamisha kutoka Mtaa wa Jamhuri (mkabala na parking ya Benjamin Mkapa tower) na kulipeleka kule kilipokuwa kiwanda cha KIUTA (Barabara ya Nyerere eneo la Darajani, mwanzo wa barabara ya kwenda Keko Mwanga)

Matokeo ya maamuzi haya ni watu wa mikoani kukosa huduma muhimu na kama wakiipata kwa gharama kubwa. Watu wa Dar kusumbuka sana ili kuzipata huduma za Ofisi hii.

Lakini kama haitoshi, mapato ya Serikali kupitia mauzo ya Nyaraka mbalimbali yatapungua sana.

Vinginevyo nia ni kuwafanya watu wasisome nyaraka mbalimbali ambazo ni halali kuwa nazo yaani Sheria, Kanuni za Sheria, Hutoba za Marais n.k.

Nawasilisha.
 
Hii idara iangaliwe vizuri kuna urasimu mkubwa sana wa upatikanaji wa nyaraka za serikali hasa kwa tuliopo mikoani. Mbaya zaidi inapelekea baadhi ya taasisi kwenda steshnari binafsi kuprint na ku-bind nyaraka muhimu za serikali na nyingine sensitive

Inaendeshwa kizee na kizamani sana. Inahitaji mabadiliko. ukiweka oda inakuja baada ya miezi sita utafikiri unaagiza Ali express toka China.
 
Back
Top Bottom