Mpenzi wangu wa zamani ( ex - girlfriend ) ananilaumu na kunipa lawama kwa matendo niliyomfanyia

goldie ink

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
5,634
9,149
Habari zenu wapendwa & memba wote wa jf.
Nina matumaini wote ni wazima wa afya na tumshukuru mungu kwa mema & uweza wake kutupa pumzi & kutulinda mpaka leo hii.

ndugu zangu wa jf,
Kama kichwa cha habari husika kinavyo jieleza hapo juu ya husu
kulalamikiwa na kupewa lawama zisizo isha na mpenzi wangu wa zamani tulioachana miaka mingi iliyopita na kisa chenyewe cha kunipa lawama na kulalamika ni kama yafuatayo katika mkasa huu.........

Mnamo mwaka 2011 niliwahi kuwa na mpenzi ambaye kwa kipindi hicho alikuwa ni mwanafunzi wa chuo fulani maarufu kilichopo mkoa wa dar es salaam inayojulikana kwa jina la I. F. M ( the institute of finance management ) huyu binti nilimpata kipindi yupo mwaka wa pili ( 2 ) chuoni hapo, lakini kwa bahati mbaya hakufanikiwa kumaliza masomo yake ila alifukuzwa chuo kwa utovu wa nidhamu na maendeleo yake katika kiwango chake cha masomo kushuka kwa wastani mbovu,

Na kilichopelekea haya yote kumkuta ni kutokana mimi nilivyokuwa namshawishi kufanya matendo machafu na yasiyofaa kimaadili hasa kwa yeye mtoto wa kike, kati ya hayo matendo ni ikiwemo,
uvutaji wa sigara,
f0b31e9b5493ec29a0166c36770b1003.jpg

2e49ac8af7cfed103932a20eb7bec1e0.jpg

f0a0d12ecd3e04fcfdc6e1f6c0279e38.jpg


Uvutaji wa bangi,
acf00f781b883a7a220f4c843b93de8e.jpg

e4fca1a1fdcd97500407ee38d045646f.jpg


Unywaji wa pombe na hata pia
Uvutaji wa sigara zenye tumbaku kali na zenye nicotine kwa wingi inayojulikana kama CIGAR au COHIBA CUBAN CIGAR.
0138496d1871ce38d8f51614356f5ee6.jpg

06cd79ea0e060296c6e26ba8707231ae.jpg

3a8d90c7b5adfddc907d5a4947085653.jpg

d78a924fcf44e7a48c1e784f624f78aa.jpg


Mfano wa mwanamke akivuta COHIBA CUBAN CIGAR.
94a68d2e84d37d894dbc017b4eeb104f.jpg


hii tabia ya kutumia sigara, bangi, na pombe yote nilimfundisha mimi lakini mwanzo alikuwa hapendi nitumie hivi vitu lakini nilimpinga na kumshawishi aweze kutumia sigara, pombe na bangi.

Nilifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuweza kumshawishi atumie hivi vitu, na hatimaye alikuwa mtumiaji mzuri kuzidi mimi.
Na katika mahusiano yetu tulidumu mwaka 1 tu..!!
tuliachana na kila mtu alifanya mambo yake, kila kukicha nilisikia maneno kwa marafiki zangu ambao walikuwa wanamfahamu kuwa huyo mwanamke amekuwa muhuni kupitiliza, la hasha hakuishia hapo mwaka 2014, aliolewa na kuanza maisha yake ya ndoa & maisha ya kifamilia,
Kwa bahati mbaya hajafanikiwa kupata mtoto mpaka sasa,
Nikiwa na maana ya kwamba amekuwa mgumba hawezi kuzaa.

Baada ya kukaa kwa muda na hili tatizo lake aliamua kunitafuta kwa udi na uvumba akiomba tukutane kwa mazungumzo, nilimtii na nikakutana nae some where cool place, tukazungumza lakini huyu binti alizungumza kwa hisia na kuanza kulia huku akinipa lawama kuwa mimi ndiye niliye msababishia awe mgumba, pia ana saratani katika mfuko wa uzazi, ( cancer of uterus ) sauti yake pia imefifia haisikiki vizuri, anapata magonjwa ya kifua, mara kwa mara yote haya ni kwa sababu ya uvutaji wa sigara na kunywa pombe kwa muda mrefu na ukizingatia yeye ni mwanamke,

Kwa kweli nimeumia sana kusikia haya na nimemuahidi nitampeleka hospitali kurekebisha afya yake, lakini alikataa na kusema anamuachia mungu kwani malipo ni hapa hapa duniani. Sipendi ateseke nimeumia mno moyoni.

Ndugu zangu,
Nashindwa kuelewa nimsaidiaje huyu binti,
Naombeni msaada wa mawazo yenu, au naomba mnielekeze nifanyeje.....??
Ushauri hapana
Nielekezeni nifanyeje kwa hili jambo zito mbele yangu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom