mpendwa, sijui kama wewe ni muumini wa dhehebu gani, lakini mie nina ushauri hapa......................
1.
yeye kaomba umchangie-kama una uwezo wa kuchanga, mchangie kwa msingi wa ombi lake na kulingana na uwezo wako, usije ukalaza watu wa nyumbani mwako na njaa kwa sababu ya kuchangia harusi hii, kumbuka kila aombaye hupokea, je tukiwasaidia wale tu walio wapenzi wetu, tutapata ama kustahili thawabu gani ya ziada? mafarisayo na wenye dhambi na watu wa mataifa nao hawafanyi hivyohivyo? hakika haki yetu lazima ipite haki ya mafarisayo, watoza ushuru na wenye dhambi, vinginevyo hatuwezi kuurithi ufalme wa Mungu.
2.
ushinde ubaya kwa wema-kwa kuwa unakiri kuwa hukumkosea, lakini bado Mungu anampa fursa na ujasiri wa kukutafuta na kuomba umuunge mkono au umsaidie, kumbuka unapaswa kuushinda ubaya kwa wema. kwa wema wako atatambua kosa lake la kumkataa mke mwema na pamoja na kuwa huna tena nafasi kwake, lakini atayasimulia matendo yako makuu siku zote za maisha yake na kufanyika baraka mlangoni mwako maisha yake yote na hivyo Mungu kutukuzwa kupitia maisha yako.
3.
kushiriki ama kutoshiriki harusi nashauri usikilize dhamiri yako inataka nini. mimi ningeshauri ushiriki kama na nafasi na usiwe kwazo katika shughuli yao ile kwa namna yoyote bali ufanyike baraka. si mbele yake bali mbele za Baba yetu aliye mbinguni. atakapoziona baraka kupitia kwako, atamshukuru Mungu na kumuinua siku zote za maisha yake na ataamini kuwa kweli wewe ni mtoto wa Mungu kwani unakata mashauri kwa jinsi ya Mungu na si kwa jinsi za wanadamu. kumbuka tena mpendwa kuwa haki yako mbele za Mungu lazima ipite haki ya afarisayo na wenye dhambi ili kustahili thawabu
thamani ya ushauri huu itategemea imani yako na kiwango cha uchaji wa Mungu ulichonacho.............ni hayo tu mpendwa........................... unarikiwe na Bwana