Mpenzi wako akianza tabia hizi zinduka

Mpenzi wako akianza tabia hizi zinduka

Kibo10

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
11,278
Reaction score
8,868
Rafiki zangu, na wana jamvi wenzangu tujadili juu ya kauli ambazo zina ishara mbaya kwenye uhusiano tena za utapeli mtukufu.

Wakati mwingine unaweza kumsikia mpenzi wako akikuambia maneno ya ajabu sana, lakini si wote wanaweza kuelewa maana yake ni nini"MFANO"Mwenzi ambaye hana mpango tena na wewe,A.K.A (kukuchoka) anaweza kuanza tabia ya kukuonea kinyaa.

Na Maneno ya kejeli kwake yakawa si suala la kujiuliza mara mbili tena.

Ni rahisi sana kukuambia bila aibu unanuka.

Ebwanae unanuka jasho sana, hebu kaoge kwanza, iwe mwanamke au mwanaume anaweza kukuambia hivyo.

Katika hali ya kawaida kabisa hiyo ni dharau,Tena inawezekana labda mlikuwa katika hatua ya kuelekea kwenye mahaba, lakini ulipomsogezea kinywa chako, ukakutana na maneno haya:

"Aaaah! Mh...unanuka mdomo bwana, sitaki.

Hizi si kauli njema na bila shaka anajaribu kukuonesha jinsi ambavyo umepungua thamani kwake.(kakuchoka)Huwezi kunuka kwa mpenzi wako, siku zote huwa unanukia, lakini kama ameona dosari yoyote na yeye kama mwenzi wako wa karibu ana wajibu wa kuhakikisha anatumia lugha nzuri kukurekebisha.

Lakini kwa kuwa hana mapenzi ya ukweli na wewe tena hana haja ya kuonesha mapenzi yake kwako,anakubwatukia atakavyo ukiona mishe hizo zimeanza kuchukuwa nafasi kwenye mahusiano jiongeze mapema iwezekanavyo kabla mtu mzima hujaumbuka.

Kuchokana kwenye mahusiano ni hatari........sana..sana..sana.
 
Cha muhimu ni kuwa msafi tu, tusisingizie mapenz, hata kwa wanaume wengine tukikutana na harufu mbaya viungo vya uzazi lazima vilale. kikubwa kama unamjali ni kuelezana kwa lugha isiyoudhi. lakini uchafu utabaki kuwa uchafu tu hakuna cha mapenz wala nini
 
kazi ipo.

Mtanange ndio huo umeanza Asnam mambo ya kuchepuka then unakuja na visingizio vya kijinga sio kwa karine hii tena ilikuwa enzi hizo sasa hivi watu wanastukia dalili mapeemaa!!
 
Last edited by a moderator:
Wewe ni umwambie tu mpenzi wangu leo nataka nikutoe auti kwa hivyo nataka uzidishe usafi zaidi ili tung'are. Halafu akioga mwambie tu. Na hisi uchovu naona tutatoka wakati wengine.
 
mi nikishaonaga dalili za kuachwa mapema namtaimu kwa kumuacha yeye hata kama nampenda.... kuachwa ni fedheha sana
 
kunuka ni kunuka tu haibadiliki, sema tu ni namna na kauli atakayotumia mwenza wako kukwambia
 
Mhh inatokea na nature ya mtu bana..kwa sababu unaeza ukakuta nature ya huyo mwanamke au mwanaume ni kuropoka ovyoo bila stahaa so inaezekana akamwambia mwezi wake ajirekebishe kwenye kunuka..kwa kutumia lugha iyo kali..na si kwamba amemchosha la hasha ni kwasababu amezoea kuropoka ovyo kwa kila mtu..
 
dah ata kama ni ukweli mpenzi wako akikwambia unanuka itauma sana, yani sijui ntafanyaje siku hiyo...
 
mtu kama unanuka ni kero huwez kupigiwa gitaa kubembelezwa ukajisafishe mfano kinywa kikiwa kinatoa harufu hata hamu ya mapenz inaisha pia jasho linakera mpenzio akikueleza ukweli haimanish amekuchoka ila anataka awe free akupe penz
 
Kama unanuka jasho kweli asikwambie?!!!

Siku zote huwa unanukia?au uchafu ndio kauona ghafla?ndio maana nikasema kama ameona dosari yoyote na yeye kama mwenzi wako wa karibu ana wajibu wa kuhakikisha anatumia lugha nzuri kukurekebisha.
 
sasa kama kweli unanuka unataka akwambie mpenzi wng una harufu nzuri kama waridi? mimi nakuchana tu ukweli, au mtu soski na miguu akivua balaa, unataka akwambie miguu yako ina harufu kama karafuu? anakuonea huruma ubadilike.
 
me akinambia nanuka ..ntamwambua aniletee deodorant..kwisha kazi
 
Siku zote huwa unanukia?au uchafu ndio kauona ghafla?ndio maana nikasema kama ameona dosari yoyote na yeye kama mwenzi wako wa karibu ana wajibu wa kuhakikisha anatumia lugha nzuri kukurekebisha.

Hawezi kusema unanuka wakati haunuki, akikwambia unanuka jasho nenda kaoge haraka, kwani kuna tatizogani? Na yeye akitoa harufu mwambie aende kuoga, mkizoweana ndiyo uzuri wake hamfichani kitu tena!
 
Mi cdhani kama hiyo ni sababu kwa kweli eti ya kuchokwa. Kwani kila mnapotaka fanya sex ndio anakwambia unanuka? ukimaanisha yupo anayefanya naye?

Km unanuka/ninanuka sikatai mtu wangu akiniambia ukweli labda uniambie katumia lugha korofi. Mimi hata kama mtu si mpenzi wangu na nikajua ana harufu inayonikera aiseeeeeeeeeeeee ataishia kunisalimia kwa kiganja no hug at all najisikia kichefuchefu sanaaaaaaaa full kinyaaaa.

Hujui kuna viarufu vinavutia hadi mtu hataki utoke pembeni yake? Badilika bana, we kawoge ule mzigo au muulize baby nifanyaje ili harufu yangu isikukere tena?

Pole badilika na chukua hatua
 
Back
Top Bottom