Mpenzi Msafiri

Slim5

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2014
Posts
28,374
Reaction score
38,248
Kwa kawaida, mtu anaporukwa na akili, anaweza kuitwa Zuzu. Anaweza kuitwa Punguani. Katika hali ambayo nipo nayo sasa, una haki ya kuniita mo ya majina hayo, kwa wasamariwema wenye huruma, labda kwao ni kama kusema nilikuwa katikati ya Zuzu na Punguani. Kifupi ni kwamba nilishabinafsisha akili zangu na kumpa mrembo Milgo, mrembo wa kisomali aliweza kuiteka akili yangu katika namna ambayo hata ukiniuliza ilikuwaje, sijui!

MSAFIRI QAFIRI Msemo ulunijia akilini, ukagonga, ukarudi. Nishasahau kuwa nipo safarini, nishasahau kuwa nipo katika safari ya siku 4 ama 5 kutokana na yatakayojiri njiani, nishasahau kuwa nilipewa somo zaidi ya somo kuhusu maswahibu ya safari kama hizi, nilishasahau kuwa, nilionywa kuwa karibu na watu nisiowafahamui, na hasa wa jinsia ya Milgo! Aaaaah wapi, akili haikuwa yangu, nilishakubali kubinafsisha akili yangu, na kumuacha Milgo afikirie kwa niaba yangu! Sikutaka kujipa mawazo, safari yenyewe ndefu, hata Tunduma hatujafika ilishaonyesha dalili ya kuniboa, kazi na dawa! Ndio, MSAFIRI QAFIRI, yote yangu, ya ndani ya safari na ya nje ya safari!

Yote kwa yote, mtoto wa kiume unakuwaje na ujasiri mbele ya mtoto wa kike ambaye hata wanaokutazamawanakuonea wivu, mate yanawatoka! Wanaokutazama wanatamani hadithi iwe tofauti, bint awe dada ili upate shemeji miongoni mwao! Shabash! Kiuno kimebinuka, ndani ya buibui lakini rasilimali inajionyesha kuwa yaliyomo yamo! Kuhusu urefu sisemi kitu, kiukweli mimi sijawahi kuona Mmasai mfupi, achilia mbali Msomali! Nywele zimesukwa kisafari safari tu, nimezoea kuona TATU KICHWA kwa dada zangu, hii ni MBILI KICHWA, nyeusii, zimemwagika sikio la kushoto, sikio la kulia! Kuanzia juu, mtoto mwembamba, wembamba wa kuvutia, kabla hujafika chini, hapo katikati, pametanuka!Macho, ni macho ya kike kweli, sio mara zote watoto wa kike hupata macho ya kike, huyu ni msichana aliebahatika kuwa na macho ya kike. Macho kama unaonewa huruma kabla hata ya hatia! Rangi sasa, daaah!

Nikavutwa! Nikavutika! Kizuri hapa ni kwamba, wakati mimi nishapenda, Milgo nae alikuwa na hisia zote za kunambia hivi wewe kijana huoni dalili zote za pendo langu kwako! Mimi na Milgo kwa hatua ile, ilikuwa ni kama chupa na kizibo, uwepo wa mmoja haukamiliki mpaka uwepo wa mwenza! Ahsante moyo, ahsante moyo wa kupenda. Sio tu kwamba nilijilegeza wakati navutwa, bali pia nilizidisha spidi ya kujipeleka karibu na Milgo kiasi asingeni-hug nilikuwa napitiliza (nilikuwa napitiliza kweli basi, walah)! Nikakumbatiwa! Nikakumbatika! Mungu wangu! MSAFIRI QAFIRI! Akili ikasafiri, ikaenda mbali zaidi, ikaenda mpaka kwa Yule ambae miezi mitatu kabla ya safari nilitibuana nae!

Ndio! Mpaka nafanya safari hii kibuyu kilikuwa full. Niliemuamini, Yule ambae aliniapia kuwa kile alichonacho ni kwa ajili yangu tu, hatampa mtu mwingine, nilishaachana nae, kiapo chake kilishindwa. Tuliachana nikabaki mwenyewe, hasira na maumivu, nikaapa sitaki tena mahusiano, nikatumia muda wangu wote kupiga kazi na kujiaandaa na safari. Ndio kusema sina kumbukumbu nzuri, ni lini hasa mara ya mwisho mimi kukumbatia ama kukumbatiwa na sio tu kukumbatiwa na binti, ni binti mrembo!

Mchanganyiko wa kitu kama shoti ya umeme au kitu kama mchirizi wa barafu inayoyeka! Nilihisi ukinitambaa mwilini, sijui hata ulipoanzia, lakini kila kiungo changu cha mwili kiliuhisi, ilikuwa ni experience nzuri sana kwangu, nilitamani kudumu katika hali ile hata kwa muda mwingi zaidi! Ilikuwa ni experience yenye mchanyato wa kuvutia sana! Kwa mbaali sana, mithili ya mgonjwa anaezinduka kutoka katika nusu kaputi, nilimsikia Milgo akitoa maneno mdomoni mwake, mengine ni ya kiingereza na baadhi ya Kiswahili, akili haikutaka na wala haikuwa na muda wa kung'amua uelewa wa hoja, lakini katika maneno yale ya Mrembo wangu, nilisikia akitajwa John, na kila alipotajwa nilitakiwa kujibu ndio au hapana, nikutaka kuupa kazi mdomo wangu, kichwa kilitumika kumaanisha NDIO ama HAPANA, na mara zote ambazo nilijibu kwa kichwa, ilikuwa inakula kwake John, mshkaji wangu!

Kwa kifupi Milgo ni kama hakupenda uwepo wa John katika kundi letu pale, ni kama vile alikuwa anatafuta namna ya kumuengua, kwa sababu ambazo alizijua yeye mwenyewe! Kwangu alitaka kujua uhusiano wangu na John, kwamba nimetoka nae wapi John? Kama huko mwisho wa safari nitakuwa na John? Majibu yangu kwa maswali hayo yalimridhisha, japo na yeye akaingia katika mkumbo ule ule wa kuwatisha wasafiri, kuwa wanatakiwa kuwa makini safarini hasa dhidi ya watu wasiowafahamu1 Ni kwamba Milgo nae alishachizika, na amesahau kuwa katika sisi kama kuna watu wanafahamiana basin nii yeye na nduguye tu, kwamba hata mimi tumefahamiana ndani ya basi tu, yaani barabarani!

Hii ni kwa mara ya kwanza kujiona walau fahamu zinanirudia, kutambua kuwa sipaswi kumtosa John, kwa sababu tu Milgo ametaka. Na ndio hofu kuu ya John. Na haya yakitendeka, John wa watu hana raha, maskini, alikuwa zaidi ya mnyonge, ile taswira yake ya awali ilipotea kabisa, akiamini mtu aliemtarajia kuwa best friend wake, anageuka msaliti mapemaaaaaa, tena kwa maelekezo ya mrembo flani hivi!

John hakuweza kununua chakula, si kwamba hakujiskia kula, No, hamu ya kula ilikatikam baada ya kugundua kuwa yupo karibu na kusalitiwa! Wakati Fatma na John wanarudi kupanda basi, niliona uso wa huzuni wa John, nikahisi hatia! Nikamuomba Milgo aende na aniletee Biskut tu (mimi ni mmoja wa watu wasiopenda kula kula safarini, nikiamini kula kula safarini kuna kero zake!) Ni Milgo akamchukua Fatma kutoka kwa John, na kwenda nae ndani hotelini kununua chochote kitu, John akatumia fursa hiyo kuniomba tuingie ndani ya basi fasta. Tulipofika katika siti zetu, John alianza kuongea katika style ambayo alinya sawa sawa na mabingwa wa kuchana, yaani alikuwa anaflow!

Kwa maelezo yake ni kwamba hafurahishwi na namna ninavowababakia watoto wa kisomali na kumuacha yeye peke yake. Nilijiskia vibaya kwa tuhuma zile. Nikajitetea, nikamueleza kuwa mimi na yeye sio marafiki, ni ndugu wenye malengo sawa, safari ya aina moja, asiwe na wasi wasi na mimi hata, na nikamuomba radhi kama nilimtenda1 Bila kujali kama warembo wale walisharudi na walishakaa katika siti zao, John nae aliniomba msamaha kama alichokifanya hakikuwa sahihi, alinieleza kuwa safari kama zile zina Baraka nyingi, kwa hiyo kila kitu nikiangalie kwa mapana yake!
Sikupenda mjadala uwe mrefu tena mbele ya mabinti wale, hivo John alikubali kuukatisha, safari inaendelea!
Nimekabidhiwa Biskut zangu, pakti moja nikampa "ndugu" yangu John, tunatafuna na huku story za hapa na pale zikiendelea. Mara nyingi John alikuwa akionyesha kuvutiwa na mandhari ya mapori na misitu tunayoipita, na mara chache akitaka kujua Majina ya maeneo kadhaa! Ni kwa mara nyingine tena, namuona John akiwa katika hali kama ile iliokuwa kabla ya kufika hotelini!

Safari ilikuwa nzuri, stori zimechanganya hasa, sasa kila mtu anapiga story na kila mtu zilikuwapo story kati yangu na Fatma, zilikuwapo story kati yangu na Milgo, zilikuwapo story kati John na Fatma, na pia zilikuwapo story kati ya John na Milgo! Kwa kifupi, lait ungebahatika kutuona, ungejiaminisha kuwa hizi ni pea mbili ambazo zipo katika mahusiano mapya, kama ilivo kawaida ya wapenzi wapya, dalili zao ni viherehere na kujishow!

Hatimaye tukaingia Mbeya mjini, wa kushuka wakashuka! Wa kupanda wakapanda, hususani wafanyabiashara wa Kizambia waliokuja kufanya manunuzi Mbeya! Safari ikaendelea na mpaka inatimu saa kumi na mbili za jioni, tulikuwa tunashuka Tunduma, mpakani. Kwa muda tulioingia Tunduma, hatukuweza kuvuka border kwenda upande wa pili wa Zambia, Nakonde. Tukaelezwa kuwa, yatupasa kulala hapo na asubuhi process zote za kugonga passports zitafanyika na jioni yake tutavuka kuendelea na safari kuelekea Lusaka!

Sasa kazi iliyopo mbele yetu ni msako wa Guest House, ndio cha kwanza cha muhimu, huku tukiwa na hofu ya wingi wa wasafiri eneo lile usijesababisha tukakosa vyumba. Huku kigiza giza kikiwa kinachanganya, na kibari chake, mchakato wa kutafuta Guest ukaanza! Mimi kushoto, Milgo kulia!

Waione wote pamoja na: chiko18 NYANYADO Aristidi selestin Milugwi Heaven Sent icca peterchoka Gobe loveissweet miss nuru Ngosha ze Dong Lee Cho in whitedoug3 pius manasse vesta bertha micheal HARUFU HALELUYA MOSHI


Sasa kazi iliyopo mbele yetu ni msako wa Guest House, ndio cha kwanza cha muhimu, huku tukiwa na hofu ya wingi wa wasafiri eneo lile usijesababisha tukakosa vyumba. Huku kigiza giza kikiwa kinachanganya, na kibaridi chake, mchakato wa kutafuta Guest ukaanza! Mimi kushoto, Milgo kulia!

Kama kawaida, John, rafiki yangu wa Kiganda ambae mpaka sasa, ameshanikubali kwa sifa zote kuwa, sasa urafiki wetu umevuka mipaka, ni ndugu sisi, na mimi huku nikijua misingi ya safari ukiwemo ule wa "MSAFIRI KAFFIRI", bado niliendelea kuwa na imani juu ya ndugu yangu huyu wa hiyari.

Ni jioni. Mji wa Tunduma upo busy, watu ni wengi, kuna kagiza fulani hivi, na pia kuna kaubaridi chenye upepo. Watu ni wengi, wametoka Dar es salaam na wengine Mbeya Mjini, wapo waliotaka kuvuka boda kama sisi, wapo pia walotaka kulala katika hotel chache za mji ule na kisha kukicha waendelee na haraka ti zao. Alimradi hapakuwa na utulivu eneo lile. Milgo aliitumia fursa hii, kunidhihirishia namna ambavyo anaifurahia safari hii na hasa kwa kigezo kwamba, imempa mpenzi ambae kwake yeye ni kama kuwa na bahati ya MTENDE (Kumbuka nilishakueleza tangu awali kwa namna gani, mtende una bahati) Hakuruhusu kuwepo kwa umbali wowote ule baina yetu, ilikuwa ni kama ULIPO NIPO! Milgo hakutaka mtu wa tatu aingilie kile kinaendelea baina yetu, mimi na yeye.

John.
Anaonekana kwa nyuma yetu, kwa aliebahatika kumuona John katika mandhari ile ni sawa na kusema, ilikuwa bendera fuata upepo, muda wote alifanya kile ambacho mimi na Milgo tulishauriana na kufikia maamuzi. John hakupendezwa na kupotezwa kwa hadhi yake na mie afiki yake. Nililijua hilo. Nikajua kuwa kwa mara nyingine tena, namtia majaribuni John, mtu ambae kwangu ni ndugu, sio rafiki tena.

Kama ilivokuwa pale awali, John hafurahiii hali hii, hali ya mimi kumpa kipaumbele mtoto wa kike mbele yake. Kwake yeye John, hataki kukubali kuwa, kulikuwa na umuhimu wa mimi au hata sisi sote kuwa karibu na mabinti wale.

Hatukuzunguka sana. Hatimaye tuliingia ndani ya nyumba moja ya kawaida tu, wenyewe wakiwa wameipa jina kuwa ni hotel, ni mfano wa guest house za uswahilini kama vile Tandale, Buguruni au Mbagala kwa Dar es salam, au sawa na Unga Limited na Matejoo kwa kule Arusha, au Pasua – Moshi!

Chumba kikapatikana.
Milgo akashauri chumba kikaguliwe kabla ya kulipiwa. Tukakikagua. Milgo akakiri kinafaa. Ni raha ilioje kuambatana na mtoto wa kike hotel, kisha awe wa kwanza kuridhika na mandhari ya chumba kama sio hotel!
Chumba kikalipiwa papo hapo.

MAAJABU.
Nikatua begi langu. Kugeuka nyuma, zamani Milgo alishajitupia juu ya kitanda. Ni kweli huyu bint ni mzuri, lakini macho yangu hayaamini kuwa muda wote nliokuwa nae, nilichoona ilikuwa ni robo tu uzuri wake, sasa nakiri ninachokiona ndio uzuri halisi! Kitanda kimefanya uzuri wa bint huyu wa Kisomali uonekane kwa mapana yake.

Milgo akafurahi kuona angalau hatua ya kwanza ya safari yetu, imefika salama, kwake yeye na Fatma, na nafsi zao, ule ulikuwa ni ushindi, yaani kufika border ya Tanzania na Zambia, salama salmini. Vichwani mwao bado kulikuwa na kumbu kumbu za masaibu yaliowakuta wakati wanajaribu kuvuka Namanga, kutokea Kenya kuingia Tanzania, anasema Milgo, walioyaona border ya Kenya na Tanzania, wakifanyiwa wakimbizi wa kisomali, ni kinyume na ubinaadamu. Usisahau. Milgo. Fatma. Ni wakimbizi wa kisomali.

Nikamskia akinipa pole za uchovu wa safari ya kutwa nzima, Ubungo, Dsm mpaka Tunduma, kauli ile niliitafsiri kama kukaribishwa kitandani, kupumzika, yaani kuondolewa uchovu wa safari (akili haikukumbuka kuwa hata na yeye ana uchovu wa safari)

Sikujiuliza mara mbili. (udadisi ni kitu kizuri, lakini kuna maeneo usilete udadisi, utaonekana una matatizo kichwani). Nlichofanya ni kama kujitupa kitandani. Ghafla milgo wangu akasimama. Nikashtuka. Akaniita. Nikaitika. Nikavutwa kama kusaidiwa kusimama, nikasimama, nikashikwa mabega kwa mikono miwili, mimi nikashika kiuno chake kwa mikono yangu! Nikakumbatiwa. Vifua vikanasiana. Nikawa naskia mapigo ya moyo, yanadunda kwa kasi, sikuweza kujua kama yale mapigo ya moyo ni ya kwangu au ya mpenzi wangu, kitu mfano wa mawimbi ya joto yakawa yanazunguka katika mwili wangu, akili yangu ikapata kazi ya ziada kutafsiri hatua ambayo mabadiliko ya mwili yanapitia muda huu.
Ni kama sijitambui. Kwa mbali nikahisi maumivu maeneo ya zipu ya suruali yangu aina ya jinsi! Cha ajabu maumivu yale nayajua yalisababishwa na nini, na nakijua kiungo cha mwili wangu kilichokutwa na dhahama ile, lakini sikujali! Daaaaah!

"Eeeeh my boy,lets get out….!" Please, tutoke nje (katika lafudhi ya mtu asiejuwa vizuri Kiswahili) Ghafla milgo akaamrisha kuwa tutoke nje. Nikawa kama sikuelewa vile. Akarudia tena. Nikaona namna uso wa mtoto wa kike ulivokuwa ukimaanisha kuwa yuko serious!

Nikaacha kila kitu changu ndani, nikafunga chumba na kutoka nje. Mseto nliokuwa nao kichwani ni kama vile mtu aliepatwa na mshangao uliochanganyika na taharuki pamoja na sintofahamu! Unyonge ulinijaa! Nje tukawakuta Fatma na John wanaongea, sikutaka kujua wanaongea nini, ila tu nliskia Milgo akiwaomba turudi wote ndani. Huko ndani Milgo alikuwa ndio msemaji mkuu, aliskika akitoa maelezo kuwa Mimi na John tutalala pale, ndani ya chumba kile, na kwamba anatutakia usiku mwema, na kwamba asubuhi watawahi kuja kugonga mlango kutuamsha, yaani tusitoke mpaka wao watufuate asubuhi!

Kwangu yaliingilia kushoto yakatokea kulia. Sina nlichomuelewa Milgo. Hasira. Kwa mara ya kwanza Milgo ananikwaza. Anauchooma moyo wangu kwa maumivu ambayo yananipa wakati mgumu sana kuyapoza.
Wakati mimi naugulia maumivu ya kulazwa na John, sio tu chumba kimoja, bali kitanda kimoja, John alikuwa busy kupanga na kupangua vitu vyake alivokuwa navyo ndani ya begi na hasa hasa nguo. Ilionekana wazi kuwa John alishachoshwa na drama kati yangu na Milgo.

Nlipokuja kushtuka ni pale John aliponisihi tufanye mpango wa kutafuta chakula, nikakubali lakini nilitoa rai kuwa, tuanze na zoezi la kuoga kwanza kisha lifuate zoezi la chakula. John alinielewa. Ndani ya dakika fupi John akawa na bukta na singlend. Nikamuomba john akaanze yeye kuoga. John akakubali. Wakati mimi najiandaa kubadili nguo, mpaka namaliza nikiwa na pensi chini tshirt juu, bado John hajaenda kuoga, yuko busy lakini sikuelewa anafanya nini!

Nikamuuliza John: "mbona huendi kuoga, muda unaenda na baridi linazidi kuwa kali?" badala ya kwenda bafuni, John akanambia nikaanze mimi kuoga.
Mabishano yakaanza rasmi, nani akaanze kuoga. Tayari akili zangu za awali zimeshanirudia kuwa MSAFIRI KAFFIRI, na kwamba katika safari hupaswi kumuamini kiumbe wa aina yoyote ile. Na kwamba safarini, muda wote ni muda wa tahadhari. Hapa sasa nipo tayari kusimamia misingi hii. Simuamini John. Ajabu ya binadamu, nilikuwa radhi kumuamini Milgo, hata kwa gharama ya kulala nae usiku kucha. Lakini ghafla nashindwa kumuamini Mwanaume mwenzangu, John, ambae nafsi ilishakiri kuwa ni ndugu yangu, ndugu wa hiyari.

Ni kama ugomvi. Sitaki kwenda kuoga. John nae hataki kutangulia kuoga yeye kabla yangu. Ni vita ya maneno, kila mmoja anatetea msimamo wa kuwa wa mwisho kwenda kuoga. Hisia kwamba huyu John tumekutana ndani basi Ubungo Dsm, tena kwa bahati mbaya, zinazidi kunipa ujasiri wa kusimamia hoja yangu kuwa yeye anapaswa kuwa wa kwanza kuoga. Ni utata kati yangu na John. Ugomvi. Ugomvi juu ya nani wa kwanza kwenda kuoga. Imani zimetutoka. Hatuaminiani.

Hatimaye nikakubali yaishe. Nikaenda kuoga. John akanisubiri. Nilienda kuoga kwa sharti kwamba funguo ya mlango wa chumba naenda nayo bafuni. Nikarudi na John nae akaenda kuoga, bila hata ya kudai funguo ya chumba. (nilihisi ujinga). Baada ya muda mfupi tukawa tayari kwa kwenda kutafuta chakula.

Nje huko tukawa tunatafuta sehemu nzuri ya kupata chakula na angalau kuvuta muda ili angalau mpaka saa 4 usiku turudi hotelini kwetu kulala. Tukabahatisha mgahawa mmoja. Tukaingia na kuomba huduma ya chakula. Tukaanza kupata chakula huku tunazungumzia safari yetu kwa maana ya tathimini mpaka hapa tulipofikia na yaliojiri ndani ya safari.

Mara ghafla Milgo huyu hapa! Milgo mbele, Fatma nyuma. Waione wote wakiwemo: chiko18 NYANYADO Aristidi selestin Milugwi Heaven Sent icca peterchoka Gobe loveissweet miss nuru Ngosha ze Dong Lee Cho in whitedoug3 pius manasse vesta bertha micheal HARUFU HALELUYA MOSHI
 
Last edited by a moderator:
Patamu hapo.

Ngoja nisiongee sana nisikie kilichotokea kwenye harakati za kutafuta nyumba ya wageni huku kigiza kikiwa kimeshaingia
 
Hizi tamthilia huwa zinasababisha wake zetu wahisi barua toka kwa mchepuko...
 
aah nimechelewa kutokea ila daah n nouma,,,,,,enhee vp mmepata gest kama bado mie nipen fatma maana gheto kwngu kuna nafas ya mtu mmoja.
 
Aahhhaaaaaa....John alianza jealous eeehee kasahau kama Love is blind loooh...aahhhhaaa .. Haya I'm waiting to hear if you two found a room and legally married ( hhhaaaaaaahhhaa) or mliishia kwa misitu na Ndoa ya mkeka ..aahhaaaa.. Kazi kweli kweli ... Nice story .. Good work bro . I will be here waiting for the part 3.. Thanks.
 


Majukumu yanabana, ntajitahidi P3 ishuke fasta! Enjoy your weekend
 
Hongerah! mtunzi mzuri usiisahau ile ''based on a true story" ya yule mdada wa ajali!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…