Mpende tu !!!

Tetra

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
1,526
Reaction score
771
::
Alikuwa muungwana
Kijana mwenye afya
Mpole,mcheshi pia
Wengi alituvutia
Waschana tulimpenda
Moyoni aliniingia.
::
Bahati ikanijia
Kumbe nae alinipenda
Bila kupoteza muda
Mipango tukaipanga
Wazazi kuwajulisha
Ili tuifunge ndoa!
::
Nilifurahi sana mie
Kujipatia mwanaume
Mwenye sifa zote
Zilizonipendeza mie
Ili nifurahie milele
::
Tulianzia nyumbani
Kila mtu alitubariki
Kwao mume tarajali
Mama mkwe jamani
Kaniwekea kizuizi
Kasema hanipendi !
::
Atamchangulia mke
Kuwa mwenga wake
Eti niachane nae
Hatuendani na yeye
Akanikataa mie
Acha chozi linitoke !
::
Lakini kwa upendo
Ndoa tukafunga kwao
Tufike kule tuendako
Mama mkwe kikwazo
Akanikaba koo
Akawa haishi vituko!
::
Kanichongea mdomo
Anitusi eti mi mchoyo
Et nimemrogea mtoto
Eti nampa tu mzigo
Naufilisi huo ukoo
Nikavunjika moyo
::
Nami nikaanza mjibu
Akaleta ukali ajabu
Vikao vikaleta suluhu
Lakini haikudumu
Mama mkwe kaja juu
Ataka ndoa isidumu.
::
Kesi zikawa haziishi
Ndoa ikakosa amani
Ma mkwe hanipendi
Kututenga lake kusudi
Eti mwanae na mimi
Anasema hatuendani
::
Uadui ukajulikana
Kila njia na jumuiya
Watu wakatuhurumia
Nikataka kuachika
Mume wangu kakataa
Nikaishi kwa mashaka
::
Wazo likanijia
Kwetu ninae mjomba
Yeye ni mganga
Kwa tiba ajulikana
Mume nikamuaga
Naenda kwetu salimia
::
Nikafika kwa mjomba
Mjomba nipe dawa
Nataka niende kuua
Ma mkwe kanichosha
Huyo atakapokufa
Ndoa yangu itapona
::
Mjomba akaniambia
Dawa nitakupa
Maelekezo sikiliza
Utaiweka ktk chakula
Atakapokula chakula
Taratibu sana atakufa
Sharti hili sikiliza
::
Uadui unafahamika
Kwa ndugu na jamaa
Sasa hakikisha kabisa
Ujioneshe unampenda
Shukuru akikutukana
Jibu wema kwa ubaya
Cheka akinuna
Ili akifa wasijue umeua
::
Yote nikayatimiza
Dawa nikamuwekea
Chakula akakila sana
Akilaumu napongeza
Nikamsifu kila mahala
Nashukuru akitukana
::
Siku moja nilishangaa
Ailinifuata analia
Akiniomba msamaha
Eti namtendea mema
Eti yeye ndiye mbaya
Akaita kila aliyetujua
Kaapa atakuwa mwema
::
Ma mkwe kabadilika
Akanipenda sana
Akanisifu kila mahala
Akawa Mama mwema
Mtetezi aliyenilinda
Upendo ukatutawala.
::
Mimi amani ikaisha
Moyoni nilitambua
Muda wowote atakufa
Ile dawa ya mjomba
Itamchukua mpendwa
Nitakosa furaha
::
Nikamfuata mjomba
Huku nikilia
Yote nikamweleza
Mwisho nikamwomba
Anipe dawa ya kuzuia
Ile dawa ya kwanza
Isimuue Mama mkwe!
::
Mjomba akacheka
Kisha akaniambia
Ile dawa aliyonipa
Haikuwa ya kuua
Ingekuwa ya kuua
Zamani sana angekufa
::
Mjomba akaniambia
Dawa aliyonipa
Ni sharti alilonipa
Tujitahidi kuwapenda
Wale wasiotupenda
Tujifanye kwamba
Kesho watakufa
Hivyo tunachowapa
NI UPENDO WA MWISHO
::
Nami nikajifunza
Upendo ni dawa
Upendo ni silaha
Upendo ni kujitoa
Upendo ni gharama
Upendo ni faraja.
=
(FRØM ØLD STÖRÍES)
 
Story yako nzuri. Ulihadithiwa na nani?

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
yataka moyo aisee ila ukiweza hili hakuna atakayekusumbua duniani, kila la heri kwenye implementation
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…