Mpasuko wa CUF, ni matokeo ya kuvimbishwa kichwa kwa kadi # 1? je, nani kapoteza?

X-bar

JF-Expert Member
Mar 20, 2019
1,002
1,146
Hakuna ubishi kwamba kutokana na ushindani wa kisiasa nchini, ustawi/uimara wa chama kimoja kwa namna moja au nyingine huleta athari mbaya kwa vyama vingine. Kutokana na ukweli huu, hakuna chama ambacho kipo tayari kujenga ustawi wa chama kingine au hata kuona vyama vingine vikistawi. Badala yake, mbali na jitihada za kujijenga kwa kuvuna wanachama wapya, baadhi ya vyama vya siasa viko tayari kuchukua hatua au mbinu yoyote ile kuhakikisha vyama vingine havijengi nguvu dhidi yake. Na huu ndio msingi wa fitna miongoni mwa vyama vya siasa. Hadi sasa tayari kuna vyama vimeshapitia fitna zilizosababisha migogoro na kubomoka au kudumaa kwa ustawi wa vyama hivyo kama vile NCCR-Mageuzi, TLP na sasa CUF.
Pamoja na ukweli huu, chama adui hakiwezi kuwa chanzo cha migogoro ndani ya vyama vingine. Hata ikitokea kuna kada au kiongozi wa chama ameshawishiwa au kutumwa na chama kingine aanzishe mgogoro katika chama chake, bado mtu huyo hatafanikisha alichotumwa endapo wanachama wote wako katika utulivu wa itikadi na msimamo mmoja kwa mujibu wa katiba na taratibu za chama chao. Kwa maneno mengine, kinachoweza kufanywa na chama adui si kupandikiza, bali kutumia fursa ya mivutano ya kiitikadi na misimamo inayojitokeza miongoni mwa viongozi wa chama kingine kuingiza fitna za kuchochea migogoro hiyo na kuhakikisha inazaa mpasuko kamili. Siku zote adui ni “opportunistic” na mbinu yake ni ile ile; “divide and conquer”. Hivyo basi, chama adui kinachofanya ni kujifanya rafiki wa upande mmoja baina ya pande zinazovutana.

Tunapoutazama mpasuko wa CUF hatuoni sabubu mpya za mpusuko huo zaidi ya hizi zilizotajwa hapo juu. Kimsingi chanzo cha mpasuko huu ni mvutano wa kimisimamo miongoni mwa viongozi na wanachama wake ambao hauna msingi wowote kwa mujibu wa katiba ya chama hicho. Katiba ya chama hicho haikatazi kiongozi kujizulu na vile vile haisemi kwamba aliyejiuzulu uongozi hana haki ya kutengua maamuzi yake au kugombea tena nafasi hiyo. Bali, katiba ya chama hicho inatoa HAKI SAWA kwa kila mwanachama kugombea nafasi ya uongozi. Kilichotokea katika mgogoro wa CUF ni kwamba Lipumba hakujiuzulu uwanachama, bali uwenyekiti tu. Bali kujiuzulu kwake haikuwa “from no reason” japo watu wanajaribu kupuuza hoja ya kujiuzulu kwake. Licha ya ukweli huu baadhi ya wajumbe wa vikao vya maamuzi walionesha msimamo wa kumkataa Lipumba kwamba hawezi kuwa mwenyekiti tena kwavile alijiuzulu mwenyewe huku wakijua katiba inatoa haki hiyo kwavile ni bado ni mwanachama halali.

Kwakuwa msimamo wa kumkataa Lipumba hakuwa na msingi wa kikatiba wa chama kulikuwa na haja gani ya kukomaa nao hadi kupelekana mahakamani? Kama kweli hoja kwamba Lipumba alikuwa mzigo na hakubaliki kuendelea na uwenyekiti wa chama hicho kwanini wasingemvumilia na kumpa haki yake kama mwanachama ya kugombea tena ili wamkatae kikatiba na kidemokrasia kwa kutomchagua tena kutokana na huo usaliti wake? Matokeo ya kukosa uvumilivu na busara ya “ku-deal” na “msaliti” Lipumba ikawa ni kutoa mwanya kwa maadui wa CUF kupenyeza fitina zao na kuchochea (siyo kupandikiza) mgogoro hadi ukaishia mpasuko kamili.

Kwakuwa hukumu juu ya mvutano wa kimsimamo umeshatolewa, na kwakuwa walalamikaji hawakuwa tayari kupokea hukumu inayompa ushindi “msaliti” na wakaamua kuachana na chama hicho moja kwa moja, sasa hatuzumgumzii mgogoro tena bali tunajadili ni nani alaumiwe maana mpasuko umeshatolewa. Hapa kuna fikra kuna makundi manne ya fikra.
Mosi, kuna watu wanaamini kwamba Lipumba alitumwa na CCM afanye maamuzi ya kung’ang’ania kurejea uwenyekiti ili asababishe kero kwa wasiomkubali ili waanzishe harakati za kumpinga au kumkimbia na kuibomoa CUF. Waliokuwa wanamkataa Lipumba ndani ya chama ni miongoni mwa wanaoshikilia fikra hii. Mathalani tulimsikia Maalim Seif pale aliposema ni heri tukae meza moja na adui CCM kuliko msaliti Lipumba. Maana yake ni kwamba kurejea kwa Lipumba ni sawa na kutia najisi misingi ya CUF ambayo huyo Lipumba alishirik kuijenga kwa miaka yote aliyodumu katika siasa. Bilas haka mtazamo huu wa Maalimu Seif juu ya Lipumba ni wazi kwamba ulimfanya akose shabaha sahihi wapi aelekeze nguvu zake katika kushughulika na changamoto iliyokuwa inakikabili chama chake. Yeye akaona kupambana na Lipumba kisheria au kumkimbia Lipumba ndo njia sahihi na pekee ya kuitetea CUF. Lakini kwa mtu mwenyekufikiri sidhani anaweza kuhoji kuondoka kwa Maalim Seif na wafuasi wake CUF kumelenga kukitetea chama hicho au maslahi yao binafsi? Lakini ikiwa wanaamini CCM imetumia kibaraka wake kuharibu CUF je wanaweza kutuhakikishia kwamba kuhamia kwao ACT kunawafanya wawe salalama na kwamba CCM hawataweza tena kufanya kile walichoifanyia CUF? Na ikitokea hivyo kwa ACT watahamia vyama vingine?

Pili, wapo wanaoamini wakulaumiwa katika mpasuko huu ni Maalimu Seif kutokana na msimamo wake mkali dhidi ya Lipumba. Lakini kama alivyobainisha mwenyewe kwamba hakuwa tayari kukaa meza moja na Lipumba bila kujali kwamba Lipumba alikuwa tayari wakae na “kuyajenga”. Ikiwa ni kweli kwamba Lipumba alimualika Seif wafanye mapatano ili kuijenga CUF, hatuna budi kuasema kwamba Maalim ana roho mbaya, mbinafsi, mtu mwenye chuki, hasira, kiburi na majivuno. Wanasema hasira hasara. Kwa misimamo hii sidhani kwamba Maalim Seif atapata mafanikio makubwa katika safari yake ya kisiasa huko alikokimbilia. Lakini historia katika siasa ya nchi hii inaonesha wanasiasa wengi waliowahi kukengeuka katika vyama vyao (waliokatwa mikia) hawajaweza kupata umaarufu na mafanikio makubwa ya kisiasa Zaidi ya yale waliyowahi kuyapata wakiwa katika vyao vya asili. Mfano wake ni Lyatonga Mrema, Fatma Maghimbi, Rashid Mohamed Rashid, Mpendazoe, Frank Magoba, Makongoro Mahanga, Marehemu Hizza Tambwe na John Shibuda.

Pia wapo wanaoamini kwamba dola kwa maana ya Msajili wa vyama vya siasa na RITA zilitumia mbereko ya chuma kumbeba Lipumba dhidi ya wale waliomkataa katika chama chake. Sidhani kwamba hoja hii ina mashiko sana kwasababu zifuatazo. Kwanza mgogoro huu ulishughulikiwa na kuamulia kisheria/kimahakama. Maana yake waliolalamika waliamini wangeshinda mashauri waliofungua dhidi ya Lipumba na mamlaka za usajili za vyama. Pili kwakuwa walioshindwa kesi wameshindwa kukata rufaa juu ya hukumu zilizotolewa ni dhahiri kwamba walikosa hoja za kisheria za kupinga hukumu hizo. Kwahiyo anayeendelea kuamini fikra ya mbereko ya chuma ya dola hawana hoja bali ni prorojo tu za kuendeleza ubishi.

Mwisho ni wale wanaoamini CHADEMA inapasa kulaumiwa kwa kuchangia mpasuko wa CUF. Sababu inayowafanya waamini hivyo ni kutokana na misimamo, kauli na matendo walioonesha juu ya mgogoro wa CUF. Mathalani tulisikia na kuona pale kada wa chama hicho Saed Kubenea alipouleza wanahabari kwamba walikusudia kufanya Opesheni Ondoa Msaliti Buguruni. Mbali na Kubenea pia tulimsikia mwenyekiti wa jumuiya ya wazee wa chama hicho wakimwalika na Maalim Seif ajiunge na chama na chama hicho na kwamba wangempa heshima ya kugombea urais kupitia chama hicho kama walivyomfanyia Lowassa. Jitihada hizi za CHADEMA inatoa mfano hai wa chama kimoja kuhujuma kingine ili kupunguza ushindani. Mbinu iliyotumika na CHADEMA ni kujiweka upande wa kundi la Maalim Seif dhidi ya lile la Lipumba. CHADEMA waliamini kwa kufanya hivyo wangevuna wakimbizi wa chama hicho pindi kikimegeka. Hata hivyo waswahili wanasema mwenzio anapoharibikiwa haimaanishi ndo kufanikiwa kwako. Ukweli huu umethibiti kwani ingawa tunaambiwa wote waliomkataa Lipumba wameungana na Maalim Seif kuhamia ACT na hakuna mmoja aliyeingia CHADEMA. Hapa kuna maswali kadhaa kwa CHADEMA kujitathimini kwa nini imetokea tofauti na walivyotarajia. Maalim Seif anaposema tuliongea na vyama vingi lakini tumependezwa na ACT maana yake nini? Je, Maalim kapewa au kaahidiwa nini na ACT ambacho angekikosa endapo angejiunga CHADEMA? Kwani kadi # 1 ya uwanachama ina maana gani katika chama cha siasa? Je, ACT ilisimama nafasi gani ya maana juu ya mgogoro wa CUF ukilinganisha na CHDEMA? Je, wazee wa CHADEMA walichelewa kufanya “booking” ya wakimbizi wa CUF? Kama vyama vyote vya CHADEMA na ACT wako katika makubaliano ya “UKWAWA MPYA” kwanini Maalim hakutoa wito kwa wafuasi wake kujiunga na chama chochote rafiki na badala yake anawaomba wamfuate yeye ACT?

Lakini si vyema kujua ni nani anapasa kulaumiwa kutokana na mpasuko wa CUF. Ni muhimu pia kujua ni nani kapoteza na nani kapatia. Nasema ni muhimu kujua nani mshindi na nani mshindwa kwa sababu mgogoro huu ulichukuliwa kwa hisia za kishabiki na wafuatiliaji wa masuala ya siasa. Mashabiki wa Maalim walibaki kusema subiri maamuzi ya mahakama tuone Lipumba atakavyoaibika.

Maoni ya watu wengi kupitia mitandao ya kijamii yanaonesha kwamba CCM impefeli katika malengo yake ya “kumuhujumu” Maalim. Bila shaka hawa ni miongoni mwa kundi lile lenye fikra kwamba mpasuko wa CUF ni matokeo ya hujuma za CCM. Kuna kitu kinatakiwa kiwekwe sawa hapa. Kwani kumuhujumu Seif maan yake nini? Ni kumzuia asigombee urais wa Zanzibar au asigombee kupitia CUF? Ikiwa CCM walihitaji kuona Seif hagombei urais tunawezaje kusema “CCM wamefeli” wakati hakuna uchaguzi uliofanyika baada ya huyo Seif kuhama CUF? Tunajuaje kwamba Seif anahitaji kugombea urais kwa mara nyingine? Lakini ikiwa lengo la CCM ni kumzuia Seif asigombee kupitia CUF kwani hiyo CUF ina kitu gani cha muhimu kwa CCM? Lakini je tuamini kwamba CCM wamelikosa akili ya kujua kwamba vyama vya kutumia kamia kama jukwaa la kugombea urais ni vingi na kwamba Maalim anaweza kuvitumia au hata kuanzia chama kipya? Hayo yote tisa, kumi ni je kada gani wa CCM tuliyemuona anatolea msimamo, kauli na matendo ya kumsaidia Lipumba katika kuihujumu CUF kama tuliviona kwa CHADEMA?

Watu wengine pia husema Lipumba ndiye aliyepoteza juu ya mgogoro. Swali litakuja je Lipumba kapoteza nini? Lipumba katika kadhia hii ndo muhanga kutokana na kupingwa na kukataliwa na Team Maalim. Lakini wapinzani wake ndo waliomshitaki mahakamani. Je walichokitaka kitokee kwa mpinzani wao kimetokea? Je, hukumu iliyotolewa na mahakama inamkwamisha Lipumba kufanya kazi zake kama mwenyekiti? Je, kutambulika kwake na mahakama kuwa ni mwenyekiti halali wa chama hicho hakumpi Lipumba heshima yake? Au kitendo cha team Maalim kuhamishia mali za CUF kwenda ACT ndo maana yake Lipumba kapoteza? Kama ni hivyo mbona tunamemsikia mwenyewe akitoa onyo dhidi ya kitendo hicho na kwamba atawafikisha mahakamani. Je, tunajua nani atapoteza ikiamuliwa na mahakama endapo atafanya hivyo?

Na kwa wanaosema team Seif wameshinda nao tuwaulize. Mshindi gani anayekimbia vita? Kwani maamuzi ya mahakama yanaishuritisha au kuishauri team Seif kuhamia vyama vingine? Ukweli kwamba waliopoteza ni CUF kama chama cha siasa kutokana kugawanyika rasmi kwa makada wake.

Kwa kumalizia, hadi sasa hakuna chama hata kimoja miongoni mwa vyama vya siasa hapa nchini ambacho kiko tayari kufa kwa kuungana na chama/vyama vingine na kujenga chama kimoja. Bali, kila chama ni adui wa kingine. Mtu asivimbe kichwa kwa hadaa za “support” kutoka chama “rafiki” kinachosimama upande wake dhidi ya mwenzie anayevutana naye ndani ya chama chake. Maadui wanaweza kudhoofisha chama kwa kutumia mivutano ya wenyewe kwa wenyewe inayokitokeza ndani ya chama kama fursa ya kuchochea mpasuko. Kuhitilafiana kimsimamo ndani ya chama ni jambo la kawaida na inapotokea hivyo hakuna bora kuleta mapatano wenyewe kwa wenyewe ndani ya chama.
 
Andiko refu pumba tupu, hata mkijitetea vipi maji yameshamwagika ukizoa utazoa na matope.

eti hakuna kiongozi wa CCM aliyetoa tamko, utatufanya wengine wajinga sana kuwa hatuoni mkono wa serikali ya CCM kupitia msajili wa vyama, RITA, mahakama na polisi, kajipange upya usituletee historia sisi tunaangalia matokeo mlichotegemea mmekikosa Maalimu kasepa na kijiji kawaachia Lipumba wenu na mihuri ya CUF.

Mmeiua CUF, msaidieni puppet wenu Lipumba kukijenga chama chenu kipya maana soon kinakwenda kuungana na TLP na UDP, huku Lipumba mkimuunganisha kwenye club ya wazee wa CCM kina Mrema na Cheyo.
 
Andiko refu pumba tupu, hata mkijitetea vipi maji yameshamwagika ukizoa utazoa na matope.

eti hakuna kiongozi wa CCM aliyetoa tamko, utatufanya wengine wajinga sana kuwa hatuoni mkono wa serikali ya CCM kupitia msajili wa vyama, RITA, mahakama na polisi, kajipange upya usituletee historia sisi tunaangalia matokeo mlichotegemea mmekikosa Maalimu kasepa na kijiji kawaachia Lipumba wenu na mihuri ya CUF.

Mmeiua CUF, msaidieni puppet wenu kukijenga chama chenu kipya maana soon kinakwenda kuungana na TLP na UDP, huku Lipumba mkimuunganisha kwenye club ya wazee wa CCM kina Mrema na Cheyo.
Mutamaliza maneno yote,ndio hivo Tena maalim kawaachia chama,Sasa Kama unasema atakuwa Kama mrema basi jitazame Tena,naona huyo lipumbavu lenu ndio litaungana na mrema kwa maalim mutasubiri sana anguko lake.
 
Nisome tena.
 
Kimsingi CUF ni kama imeshakufa rasmi, na kuthibitisha hilo subiri mwakani. Wako watu wanaosema hata chadema hawatapata mbunge hata mmoja, , kitu mbacho wachambuzi wa masuala ya siasa na kiusalama wanapingana nacho. Hoja yao imekaa katika kuhoji kwamba huo ulinzi utakao saidia kuiba kura nchi nzima watautoa wapi, na pili iko mikoa na majimbo yenye historia ya vurugu kama mara mbeya na miji mikubwa mingineyo, maeneo kama hayo kufanya dhuruma ya uhujumu ni magumu sana.msingi wao wa hoja umejikita katika hoja kwamba si kweli ccm ilipenda kupoteza majimbo ya Dsm kirahisi rahisi, ukwelu ni kwamba walibanwa na mbinu zao , kwenye chaguzi ndogo ilikuwa rahisi kwa sababu ulinzi unahamia huko sehemu moja, tofauti na uchaguzi mkuu kila mtu anapambana na eneo lake
 
Subira ni mwalimu anayetufundisha mengi sana. Na pia tukumbuke katika siasa wenyewe wana kamsemo kao kwamba hakuna adui wa kudumu bali kuna maslahi ya kudumu.
 
Inavyoonekana CCM na CHADEMA wamehusika sana katika mgogoro wa CUF. Wamekikoroga na kukidhoofisha mwishowe CUF wako taabani. CCM wamelifiri Maalim ataacha siasa baada ya kuchanganywa huku CHADEMA wakiamini kwamba baada ya Maalim kukorogwa CUF atahamia kwao. Lakini kinyume na woooote walivyofikiri amewaacha hoi watu na kuibua mijadala mingi baada ya kuhamia ACT Wazalendo. CHADEMA bado hawajaamini kilichotokea.
Punde kuna watu wameshaanza kumpa indhari Maalim kwamba Zitto haaminiki na msaliti na ndiye M1. Dah, siasa ni mchezo wa ajabu sana, Zitto amekaribishwa UKAWA lakini sasa yameshaanza kuibuliwa mavi ya kale dhidi yake! Jamani tuwaache wenyewe wajijenge ili tuanze kuona huu muunganiko kati ya Mliberali na Mjamaa wa Kidemokrasia watavyozifanya siasa zao. Ni mchanyato wa aina yake.
 
"Pathognomonic" signs za uhusika wa ccm na serekali yake ni
1). Lipumba aliendelea kupewa ruzuku pamoja na kuwepo kesi mahakamani.
2) Lipumba aliendelea kufanya mikutano popote pale alipo taka wakati upande wa pili wakizuiwa.
3) Polisi ililinda mikutano/vikao vyote vya Lipumba ili asisumbuliwe na yeyote.

Hayo 3 hapo juu yalikuwa ya wazi kwa kila mmoja mwenye akili tambuzi, kwayo waweza kuhisi mengine yalofanyika mafichoni yakiwa ya kweli.
 
Uchambuzi makini sana ,hongera!
Hakuna ubishi kwamba kutokana na ushindani wa kisiasa nchini, ustawi/uimara wa chama kimoja kwa namna moja au nyingine huleta athari mbaya kwa vyama vingine. Kutokana na ukweli huu, hakuna chama ambacho kipo tayari kujenga ustawi wa chama kingine au hata kuona vyama vingine vikistawi. Badala yake, mbali na jitihada za kujijenga kwa kuvuna wanachama wapya, baadhi ya vyama vya siasa viko tayari kuchukua hatua au mbinu yoyote ile kuhakikisha vyama vingine havijengi nguvu dhidi yake. Na huu ndio msingi wa fitna miongoni mwa vyama vya siasa. Hadi sasa tayari kuna vyama vimeshapitia fitna zilizosababisha migogoro na kubomoka au kudumaa kwa ustawi wa vyama hivyo kama vile NCCR-Mageuzi, TLP na sasa CUF.
Pamoja na ukweli huu, chama adui hakiwezi kuwa chanzo cha migogoro ndani ya vyama vingine. Hata ikitokea kuna kada au kiongozi wa chama ameshawishiwa au kutumwa na chama kingine aanzishe mgogoro katika chama chake, bado mtu huyo hatafanikisha alichotumwa endapo wanachama wote wako katika utulivu wa itikadi na msimamo mmoja kwa mujibu wa katiba na taratibu za chama chao. Kwa maneno mengine, kinachoweza kufanywa na chama adui si kupandikiza, bali kutumia fursa ya mivutano ya kiitikadi na misimamo inayojitokeza miongoni mwa viongozi wa chama kingine kuingiza fitna za kuchochea migogoro hiyo na kuhakikisha inazaa mpasuko kamili. Siku zote adui ni “opportunistic” na mbinu yake ni ile ile; “divide and conquer”. Hivyo basi, chama adui kinachofanya ni kujifanya rafiki wa upande mmoja baina ya pande zinazovutana.

Tunapoutazama mpasuko wa CUF hatuoni sabubu mpya za mpusuko huo zaidi ya hizi zilizotajwa hapo juu. Kimsingi chanzo cha mpasuko huu ni mvutano wa kimisimamo miongoni mwa viongozi na wanachama wake ambao hauna msingi wowote kwa mujibu wa katiba ya chama hicho. Katiba ya chama hicho haikatazi kiongozi kujizulu na vile vile haisemi kwamba aliyejiuzulu uongozi hana haki ya kutengua maamuzi yake au kugombea tena nafasi hiyo. Bali, katiba ya chama hicho inatoa HAKI SAWA kwa kila mwanachama kugombea nafasi ya uongozi. Kilichotokea katika mgogoro wa CUF ni kwamba Lipumba hakujiuzulu uwanachama, bali uwenyekiti tu. Bali kujiuzulu kwake haikuwa “from no reason” japo watu wanajaribu kupuuza hoja ya kujiuzulu kwake. Licha ya ukweli huu baadhi ya wajumbe wa vikao vya maamuzi walionesha msimamo wa kumkataa Lipumba kwamba hawezi kuwa mwenyekiti tena kwavile alijiuzulu mwenyewe huku wakijua katiba inatoa haki hiyo kwavile ni bado ni mwanachama halali.

Kwakuwa msimamo wa kumkataa Lipumba hakuwa na msingi wa kikatiba wa chama kulikuwa na haja gani ya kukomaa nao hadi kupelekana mahakamani? Kama kweli hoja kwamba Lipumba alikuwa mzigo na hakubaliki kuendelea na uwenyekiti wa chama hicho kwanini wasingemvumilia na kumpa haki yake kama mwanachama ya kugombea tena ili wamkatae kikatiba na kidemokrasia kwa kutomchagua tena kutokana na huo usaliti wake? Matokeo ya kukosa uvumilivu na busara ya “ku-deal” na “msaliti” Lipumba ikawa ni kutoa mwanya kwa maadui wa CUF kupenyeza fitina zao na kuchochea (siyo kupandikiza) mgogoro hadi ukaishia mpasuko kamili.

Kwakuwa hukumu juu ya mvutano wa kimsimamo umeshatolewa, na kwakuwa walalamikaji hawakuwa tayari kupokea hukumu inayompa ushindi “msaliti” na wakaamua kuachana na chama hicho moja kwa moja, sasa hatuzumgumzii mgogoro tena bali tunajadili ni nani alaumiwe maana mpasuko umeshatolewa. Hapa kuna fikra kuna makundi manne ya fikra.
Mosi, kuna watu wanaamini kwamba Lipumba alitumwa na CCM afanye maamuzi ya kung’ang’ania kurejea uwenyekiti ili asababishe kero kwa wasiomkubali ili waanzishe harakati za kumpinga au kumkimbia na kuibomoa CUF. Waliokuwa wanamkataa Lipumba ndani ya chama ni miongoni mwa wanaoshikilia fikra hii. Mathalani tulimsikia Maalim Seif pale aliposema ni heri tukae meza moja na adui CCM kuliko msaliti Lipumba. Maana yake ni kwamba kurejea kwa Lipumba ni sawa na kutia najisi misingi ya CUF ambayo huyo Lipumba alishirik kuijenga kwa miaka yote aliyodumu katika siasa. Bilas haka mtazamo huu wa Maalimu Seif juu ya Lipumba ni wazi kwamba ulimfanya akose shabaha sahihi wapi aelekeze nguvu zake katika kushughulika na changamoto iliyokuwa inakikabili chama chake. Yeye akaona kupambana na Lipumba kisheria au kumkimbia Lipumba ndo njia sahihi na pekee ya kuitetea CUF. Lakini kwa mtu mwenyekufikiri sidhani anaweza kuhoji kuondoka kwa Maalim Seif na wafuasi wake CUF kumelenga kukitetea chama hicho au maslahi yao binafsi? Lakini ikiwa wanaamini CCM imetumia kibaraka wake kuharibu CUF je wanaweza kutuhakikishia kwamba kuhamia kwao ACT kunawafanya wawe salalama na kwamba CCM hawataweza tena kufanya kile walichoifanyia CUF? Na ikitokea hivyo kwa ACT watahamia vyama vingine?

Pili, wapo wanaoamini wakulaumiwa katika mpasuko huu ni Maalimu Seif kutokana na msimamo wake mkali dhidi ya Lipumba. Lakini kama alivyobainisha mwenyewe kwamba hakuwa tayari kukaa meza moja na Lipumba bila kujali kwamba Lipumba alikuwa tayari wakae na “kuyajenga”. Ikiwa ni kweli kwamba Lipumba alimualika Seif wafanye mapatano ili kuijenga CUF, hatuna budi kuasema kwamba Maalim ana roho mbaya, mbinafsi, mtu mwenye chuki, hasira, kiburi na majivuno. Wanasema hasira hasara. Kwa misimamo hii sidhani kwamba Maalim Seif atapata mafanikio makubwa katika safari yake ya kisiasa huko alikokimbilia. Lakini historia katika siasa ya nchi hii inaonesha wanasiasa wengi waliowahi kukengeuka katika vyama vyao (waliokatwa mikia) hawajaweza kupata umaarufu na mafanikio makubwa ya kisiasa Zaidi ya yale waliyowahi kuyapata wakiwa katika vyao vya asili. Mfano wake ni Lyatonga Mrema, Fatma Maghimbi, Rashid Mohamed Rashid, Mpendazoe, Frank Magoba, Makongoro Mahanga, Marehemu Hizza Tambwe na John Shibuda.

Pia wapo wanaoamini kwamba dola kwa maana ya Msajili wa vyama vya siasa na RITA zilitumia mbereko ya chuma kumbeba Lipumba dhidi ya wale waliomkataa katika chama chake. Sidhani kwamba hoja hii ina mashiko sana kwasababu zifuatazo. Kwanza mgogoro huu ulishughulikiwa na kuamulia kisheria/kimahakama. Maana yake waliolalamika waliamini wangeshinda mashauri waliofungua dhidi ya Lipumba na mamlaka za usajili za vyama. Pili kwakuwa walioshindwa kesi wameshindwa kukata rufaa juu ya hukumu zilizotolewa ni dhahiri kwamba walikosa hoja za kisheria za kupinga hukumu hizo. Kwahiyo anayeendelea kuamini fikra ya mbereko ya chuma ya dola hawana hoja bali ni prorojo tu za kuendeleza ubishi.

Mwisho ni wale wanaoamini CHADEMA inapasa kulaumiwa kwa kuchangia mpasuko wa CUF. Sababu inayowafanya waamini hivyo ni kutokana na misimamo, kauli na matendo walioonesha juu ya mgogoro wa CUF. Mathalani tulisikia na kuona pale kada wa chama hicho Saed Kubenea alipouleza wanahabari kwamba walikusudia kufanya Opesheni Ondoa Msaliti Buguruni. Mbali na Kubenea pia tulimsikia mwenyekiti wa jumuiya ya wazee wa chama hicho wakimwalika na Maalim Seif ajiunge na chama na chama hicho na kwamba wangempa heshima ya kugombea urais kupitia chama hicho kama walivyomfanyia Lowassa. Jitihada hizi za CHADEMA inatoa mfano hai wa chama kimoja kuhujuma kingine ili kupunguza ushindani. Mbinu iliyotumika na CHADEMA ni kujiweka upande wa kundi la Maalim Seif dhidi ya lile la Lipumba. CHADEMA waliamini kwa kufanya hivyo wangevuna wakimbizi wa chama hicho pindi kikimegeka. Hata hivyo waswahili wanasema mwenzio anapoharibikiwa haimaanishi ndo kufanikiwa kwako. Ukweli huu umethibiti kwani ingawa tunaambiwa wote waliomkataa Lipumba wameungana na Maalim Seif kuhamia ACT na hakuna mmoja aliyeingia CHADEMA. Hapa kuna maswali kadhaa kwa CHADEMA kujitathimini kwa nini imetokea tofauti na walivyotarajia. Maalim Seif anaposema tuliongea na vyama vingi lakini tumependezwa na ACT maana yake nini? Je, Maalim kapewa au kaahidiwa nini na ACT ambacho angekikosa endapo angejiunga CHADEMA? Kwani kadi # 1 ya uwanachama ina maana gani katika chama cha siasa? Je, ACT ilisimama nafasi gani ya maana juu ya mgogoro wa CUF ukilinganisha na CHDEMA? Je, wazee wa CHADEMA walichelewa kufanya “booking” ya wakimbizi wa CUF? Kama vyama vyote vya CHADEMA na ACT wako katika makubaliano ya “UKWAWA MPYA” kwanini Maalim hakutoa wito kwa wafuasi wake kujiunga na chama chochote rafiki na badala yake anawaomba wamfuate yeye ACT?

Lakini si vyema kujua ni nani anapasa kulaumiwa kutokana na mpasuko wa CUF. Ni muhimu pia kujua ni nani kapoteza na nani kapatia. Nasema ni muhimu kujua nani mshindi na nani mshindwa kwa sababu mgogoro huu ulichukuliwa kwa hisia za kishabiki na wafuatiliaji wa masuala ya siasa. Mashabiki wa Maalim walibaki kusema subiri maamuzi ya mahakama tuone Lipumba atakavyoaibika.

Maoni ya watu wengi kupitia mitandao ya kijamii yanaonesha kwamba CCM impefeli katika malengo yake ya “kumuhujumu” Maalim. Bila shaka hawa ni miongoni mwa kundi lile lenye fikra kwamba mpasuko wa CUF ni matokeo ya hujuma za CCM. Kuna kitu kinatakiwa kiwekwe sawa hapa. Kwani kumuhujumu Seif maan yake nini? Ni kumzuia asigombee urais wa Zanzibar au asigombee kupitia CUF? Ikiwa CCM walihitaji kuona Seif hagombei urais tunawezaje kusema “CCM wamefeli” wakati hakuna uchaguzi uliofanyika baada ya huyo Seif kuhama CUF? Tunajuaje kwamba Seif anahitaji kugombea urais kwa mara nyingine? Lakini ikiwa lengo la CCM ni kumzuia Seif asigombee kupitia CUF kwani hiyo CUF ina kitu gani cha muhimu kwa CCM? Lakini je tuamini kwamba CCM wamelikosa akili ya kujua kwamba vyama vya kutumia kamia kama jukwaa la kugombea urais ni vingi na kwamba Maalim anaweza kuvitumia au hata kuanzia chama kipya? Hayo yote tisa, kumi ni je kada gani wa CCM tuliyemuona anatolea msimamo, kauli na matendo ya kumsaidia Lipumba katika kuihujumu CUF kama tuliviona kwa CHADEMA?

Watu wengine pia husema Lipumba ndiye aliyepoteza juu ya mgogoro. Swali litakuja je Lipumba kapoteza nini? Lipumba katika kadhia hii ndo muhanga kutokana na kupingwa na kukataliwa na Team Maalim. Lakini wapinzani wake ndo waliomshitaki mahakamani. Je walichokitaka kitokee kwa mpinzani wao kimetokea? Je, hukumu iliyotolewa na mahakama inamkwamisha Lipumba kufanya kazi zake kama mwenyekiti? Je, kutambulika kwake na mahakama kuwa ni mwenyekiti halali wa chama hicho hakumpi Lipumba heshima yake? Au kitendo cha team Maalim kuhamishia mali za CUF kwenda ACT ndo maana yake Lipumba kapoteza? Kama ni hivyo mbona tunamemsikia mwenyewe akitoa onyo dhidi ya kitendo hicho na kwamba atawafikisha mahakamani. Je, tunajua nani atapoteza ikiamuliwa na mahakama endapo atafanya hivyo?

Na kwa wanaosema team Seif wameshinda nao tuwaulize. Mshindi gani anayekimbia vita? Kwani maamuzi ya mahakama yanaishuritisha au kuishauri team Seif kuhamia vyama vingine? Ukweli kwamba waliopoteza ni CUF kama chama cha siasa kutokana kugawanyika rasmi kwa makada wake.

Kwa kumalizia, hadi sasa hakuna chama hata kimoja miongoni mwa vyama vya siasa hapa nchini ambacho kiko tayari kufa kwa kuungana na chama/vyama vingine na kujenga chama kimoja. Bali, kila chama ni adui wa kingine. Mtu asivimbe kichwa kwa hadaa za “support” kutoka chama “rafiki” kinachosimama upande wake dhidi ya mwenzie anayevutana naye ndani ya chama chake. Maadui wanaweza kudhoofisha chama kwa kutumia mivutano ya wenyewe kwa wenyewe inayokitokeza ndani ya chama kama fursa ya kuchochea mpasuko. Kuhitilafiana kimsimamo ndani ya chama ni jambo la kawaida na inapotokea hivyo hakuna bora kuleta mapatano wenyewe kwa wenyewe ndani ya chama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
First class crap.
Lipumba ana makaratasi ya CUF hana uungwaji mkono. Wanachama waliokuwa chama cha CUF wamemwachia Lipumbavu CUF yake.
Usijfanye hujui kilichotokea kuvuruga upinzani kwa Lipumbavu na Dr Mihogo kujiuzulu nafasi zao kwa kitita cha madola wakiamriwa na kusimamiwa na CCM.
Ungeweka kipengele cha hoja ya sisi wanachama wenye itikadi za vyama vyetu; bandiko lako lingekuwa tofauti. Propaganda za kuwa na watu fulani ndiyo chama na ndio siasa ni huko huko.
Napongeza na kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli na CCM kwa kujiweka na kujionyesha hadharani kuchukia upinzani. Imetuwezesha kupata viashiria vya kuwatambua wasiotutakia mema wananchi kupitia siasa.
 
Tunaopenda kusoma mabandiko marefu umetutesa tu. Hii ina faida gani wakati msiba umeshaisha na Marehemu yupo mbele ya kiti cha hukumu. Acheni watu waendelee na maisha yao. Marehemu mlimtumia kutenda matendo maovu sana kwa wenzake leo mnataka kusema kifo chake nyie mliokuwa mnamtumia hamhusiki!?
 
Back
Top Bottom