Mpango wa kuagiza gesi ya kupikia majumbani utasaidia kweli kushusha bei?

tereweni

JF-Expert Member
Aug 15, 2012
618
362
Wakuu habarini.
nimesikia kwamba serikali ina mpango huu
"Serikali itaanza kutumia mfumo wa uagizaji wa pamoja wa nishati ya gesi ya kupikia (LPG), kama inavyofanyika kwa mafuta ya ndege, petroli, dizeli na mafuta taa ifikapo Septemba mwaka huu. "
je? Hii itapunguza hizi bei za sasa za gesi za majumbani kama LAKE, ORYX , MIHAN n.k
 
zile mbwe mbwe za kuwa tuna gas ya kuuza miaka sijui 100 ya kitu gani? nadhani mpaka tunapoagiza wanatucheka kwa ujuha wetu
 
Ile gas ya Mtwara haijaweza kutengenezwa ifanane na ile yya LPG tunayotumia. Kwa sasa hivi ndio kiwanda kipo mbioni. Ikiwa tayari, miti itapumzika kwa kuni maana nchi zenye mafuta bei ni nafuu sana kwenye mafuta na tunategemea kwenye gesi nasi itakuwa hivyo.
 
Serikali waweke incentives kwenye gesi
Mkaa upigwe marufuku ili uwe bidhaa adimu kama madawa ya kulevya
Ukikamatwa nao jela kidogo

Gesi iwe bei ndogo
 
Sema ni siasa tu ndio zinaongoza nchi hii ila kitaluma gas mpaka ianze kutumika na kuona faida yake inachukua mda kidogo#kuhusu kuagiza ili ishuke kama hilo litafanyika maana dah oryx wako juu sana mpaka gas inakuwa kama anasa afu usambazaji wao kando ya mji ni wa kusuasua sana
 
Duh nilidhani gas ya Ntwara ingesaidia kuondoa au kupunguza maumivu ya gas za kupikia majumbani.
 
Back
Top Bottom